Land Rover Discovery 4 off road capabilities.


Mkuu kama umesoma vizuri nlisema the almighty Ranger rover is the best SUV so far ,ila kwa hayo matoleo mengine ya land rover kama 110,discovery Mimi na opt for a land cruiser
 

Sijasema kwamba defender ni gari mbaya Hapana, ila nimejaribu kuelezea sababu za Serikali kuachana nazo na kununua Toyota Land cruiser, na sababu hasa ni kwamba zinawasumbua na zina gharama kubwa ukilinganisha na toyota kumbuka Land Rover zilikuwa zinatumiwa kwa sababu ya mabakia ya Ukoloni wa Uingereza na ndiyo maana kila mahali kuanzia Kenya, Uganda zipo ila sasa hivi hata Kenya pia nilikuwa juzi huko wameacha kuzinunua tena na wanatumia Toyota Land Cruiser au Nissan Patrol na sababu kubwa ni kwamba Land Rover hawatoi tena ile version kama ya 109/110 ambayo ilitengenezwa maalumu kwa Afrika sasa hivi kuna hii new model nimeshaitumia sana Td 5 na iko juu ya mawe ingawaje ni mpya kabisa dereva wa Serikali walienda huko Mikoani wakaingia kwenye maji electronics zikafa na wanashindwa kuzirepair, kuhusu vumbi kuingia ni mwenyewe nilisafiri nayo Td5 na tulipata shida sana na ac kwa hasa kwa watu waliokaa nyuma na pia kuna openings nyingi zinazopitisha vumbi kuanzia kwenye milango hasa wa nyuma na chini!

Hivyo ukisikia watu wanasifu Land Rover ni zile za zamani 109, 119 mpaka defender za mwanzo kama miaka 10 iliyopita lkn hizi za toleo la mwisho kwa serikali yetu wamezishindwa na ndio maana idara nyingi wameacha kuzinunua!

Kuhusu ubora wa Toyota, jeshi la Polisi TZ hawajawahi kutumia Toyota land cruiser ndiyo mara ya kwanza ila nijuavyo JWTZ walikuwa na Nissan Patrol pick up ambazo mpaka leo baadhi bado zipo na zina miaka ishirini sasa tangu enzi ya Salim A.Salim lkn nijuavyo ndiyo gari inayotumiwa kwenye vita huko middle east kuanzia ISIS mpaka Libya kote hivyo kuna sababu hata UN hawanunui defender huku Afrika angalia gari zote zinazonunuliwa na UN ambazo zinatumika kwenye mazingira magumu ni Toyota Land Cruiser na labda cha kushangaza zaidi Waingereza wenyewe huwa wanatoa msaada wa magari ya kutumika hapa Tanzania kwenye miradi wanayoifadhili na hawatoi defender huwa wanatoa Toyota land cruiser hasa Hard Top!

Hivyo sijahoji ubora wa Land Rover kwa ujumla wake inawezekana ni moja kati ya gari bora Duniani kushinda Land Cruiser lkn kwa Tanzania zinawasumbua serikali kwenye gharama na ndio maana wameziacha sasa labda hatujui kuzitumia hilo sifahamu!
 

Kwa sisi wenye kazi nyingi za offroad tutaangalia uwezekano.
Ila kwasasa nadhani discovery 4 itakata kiu yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…