TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 11,235
- 22,581
Nyota huyo wa Barcelona anakabiliwa na uchunguzi huo kutokana na malalamiko ambayo mamlaka imesema imeyapokea kutoka kwa Chama Cha Mambilikimo nchini Uhispania kinachoitwa ADEE.
Duru za ndani zinaeleza kwamba Mbilikimo hao walikuwa katika sherehe hiyo iliyofanyika mwishoni mwa juma lililopita kama watumbuizaji.
Wizara ya Haki za Kijamii ya Uhispania imeitaka ofisi ya mwendesha mashtaka kuchunguza tukio hilo. Yamal alifikisha miaka 18 mnamo Julai 13 na tafrija yake hiyo ilihudhuriwa na wachezaji na watu wengi mashuhuri duniani.