Maelezo haya yandhirisha kuwa hakuna mtu anayezaliwa akiwa na uwezo fulani hivyo hakuna kipaji.
Big no! Yaan Hapana kubwa, mfano wa kiziwina kipofu hauthibitishi kwamba hakuna kipaji, hapo umebakanisha mambo!!
Unasiganisha mambo kati ya kipaji cha asili (nature) na mazingira au mafunzo (nurture) katika kukuza uwezo wa mtu.
Uwezo wa binadamu unaweza kuendelezwa kwa kiasi kikubwa kupitia mazingira, mazoezi, na mahitaji lakini kipaji kina nafasi ya juu kabsa..
Ubongo wa binadamu una uwezo mkubwa wa kubadilika kulingana na hali, kwa hiyo mtu anaweza kufikia kiwango cha ustadi hata bila “kipaji cha kuzaliwa,” endapo tu ataweka juhudi sahihi, lakini mwenye kipaji atafikia kiwango cha ustadi cha juu zaidi akiweka hizohizo juhudi zilizotumiwa na asiye na kipaji✍️✍️
Kipaji bado kina nafasi yake. Kuna watu wanaozaliwa wakiwa na:
Uwezo wa kipekee wa kumbukumbu
Hisia kali zaidi (kama kusikia kwa undani au kuona kwa haraka)
Uwezo wa kujifunza haraka zaidi kuliko wengine
Yote hiyo ni ishara kwamba baadhi ya watu wana vipaji vya asili.
Maelezo yako ya awali hayakanushi uwepo wa vipaji, bali yanaonyesha kuwa mazoezi, mazingira, na hali ya maisha vinaweza kukuza uwezo mkubwa hata kwa watu ambao hawakuonyesha kipaji mwanzoni.
Vipaji vya kuzaliwa vipo, lakini haviwezi kustawi bila juhudi, motisha, au mazingira sahihi.
Kwahiyo ni kipaji kwanza ndo kinachoshawishi scouts wakijua lazma wataenda kuluendeleza kwa mazoezi
Na kukufundisha kuwa na juhudi