Muke Ya Muzungu
JF-Expert Member
- Jun 17, 2009
- 3,444
- 264
Amini msiamini, naona mchuano mkali kati ya Lameck Airo na Bwna mdogo John MAshaka 2015. Lameck aligusa nyoyo za watu na hata kumshinda mpinzani wake mkubwa Prof. Monyo. Lameck alitoa kituko cha mwaka, kwa kusema kwamba, Darasa la saba mpo??? basi umati mkubwa ukaitika tupo... Basi hiyo ndio ikawa signature yake kwenye kampeni.......Darasa la saba ukawa ndio wimbo wake. .... Ila kwenye uchaguzi wa 2015, kuna tetesi za uhakika kwamba atapambana na mwanaharakati John Mashaka ambaye anaheshimika na kukubalika siyo kawaida kwenye jimbo la Rorya. Vile vile kuna tetesi kwamba mashaka ambaye amekulia Ukonga, anaweza kugombea Segerea. Tunasubiri tuone ni wapi, ila Lameck atakuwa na wakati mgumu sana 2015
Hakuna Mbunge wa hovyo kama Lameck Airo. Aliwahonga wakurya na wajaluo gongo akaingia Bungeni akidhani atatumia mali zake kuleta maendeleo Rorya lakini hadi sasa ameshindwa kabisa kuleta maendeleo na wala hana changamoto yotote Bungeni. Hata sijui kama huwa anahudhuria. Kuna vijiji huko Rorya vina miundombinu ya maji kwa maana ya ntandao wa mabomba lakini havipati maji toka ziwani eti kwa sababu mashine ya kusukuma maji imeharibika. Airo anashindwa hata kupigania hilo tu acha matatizo lukuki ya Rorya. Airo ni afadhali angekimbia mapema na kuwaaachia wanarorya jimbo lao.
Unakumbuka lile sakata la yeye (lameck Airo) kulalamikia viongozi wa chama chake kumwekea kauzibe asilete maendeleo jimboni nao wakaufyata? Rorya ni zaidi ya unavyoifahamu...usije shangaa 2015 anarudi bungeni...wewe na mimi hatufahamu
Mkuu Bobuk naona huijui Rorya wewe. Gaudencia Kabaka anataka kugombea Tarime siyo Rorya. Pia ufahamu kwamba Rorya kuna ukabila wa kufa mtu. Lile jimbo ni la wajaluo hivyo hakuna mkurya ama kabila lingine abayeweza kupata ubunge pale hasa kwa sasa.Ukweli ni kwamba Lameick Airo ameshatangaza kwamba hatagombea tena ubunge Rorya. kwasababu pamoja eti na kuwaletea maendeleo kwa kutumia pesa yake (barabara, madawati, visima vya maji) Lakini wanarorya wanamtukana eti hakusoma darasa la saba (ambayo BTW ndiyo ilikuwa slogan yake wakati wa kampeini 2010).
Sasa hivi CCM wanamuandaa Waziri wa Vijana na Ajira Mh. Gaundesia Kabaka. Sijui CDM wanamundaa nani? Ninakumbuka Mabere Nyaucho Marando aliwahi kulichukia hilo jimbo 1995 alipokuwa NCCR Mageuzi.
Kimbunga kwa unafikiHakuna Mbunge wa hovyo kama Lameck Airo. Aliwahonga wakurya na wajaluo gongo akaingia Bungeni akidhani atatumia mali zake kuleta maendeleo Rorya lakini hadi sasa ameshindwa kabisa kuleta maendeleo na wala hana changamoto yotote Bungeni.
Hata sijui kama huwa anahudhuria. Kuna vijiji huko Rorya vina miundombinu ya maji kwa maana ya ntandao wa mabomba lakini havipati maji toka ziwani eti kwa sababu mashine ya kusukuma maji imeharibika.
Airo anashindwa hata kupigania hilo tu acha matatizo lukuki ya Rorya. Airo ni afadhali angekimbia mapema na kuwaaachia wanarorya jimbo lao.