Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,768
- 49,949
Siku za karibuni kumekuwa na mjadala mkali kuhusu ushoga. Walio wengi katika kutoa maoni yao wameegemea kwenye miongozo ya kidini na maadili ya Mtanzania.
Pia siku za karibuni Bunge la Ulaya na Marekani, wameukosoa utawala wa awamu hii kwa mambo 15. Yote yakilenga ukanyagaji wa haki za raia za kikatiba na maazimio ya mikataba ya kimataifa ambayo Taifa letu limeridhia.
Wameorodhesha mifano michache ya ugandamizaji wa haki za raia. Miongoni mwa hizo, ni:
1) Mauaji holela ya raia, kutekwa na kupotezwa kwa raia bila ya serikali kuonekana inaguswa na matukio hayo
2) Kukamatwa na kufungwa ovyo kwa watu wanaokosoa utawala
3) Kukamatwa na kufungwa ovyo kwa viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani
4) Kufungia Bunge ili wananchi wasione wala kusikia yale ambayo wawakilishi wao wanayaongea
5) Kuzuia wanafunzi wa kike kuendelea na masomo baada ya kupata ujauzito
6) Kuwadhalilisha wanaofanya mapenzi ya jinsia moja
7) Kufungia ovyo vyomba vya habari
Mimi naongelea kwa mtazamo wa kidini kuhusiana na mashoga, kama wale wanaolaani tamko la EU kuhusu mashoga, wanaoelezea kwa kuegemea mtazamo wa mafundisho ya dini.
Kwa Wakristo, Mkristo wa kweli hawezi kumdhalilisha wala kumhukumu mtu yeyote anayedhani ni mtenda dhambi.
Tumeonywa, tusihukumu tusije tukahukumiwa.
Kazi yetu ni kutoa mafundisho ya kweli, yaani kueleza nini ni sahihi kwa kadiri ya maelekezo na mpango wa Mungu, na nini siyo sahihu. Si kazi yetu sisi kumhukumu mwanadamu mwenzetu.
Papa Francis alipofanya ibada kubwa kule Brazil, aliulizwa na wanahabari, 'nini msimamo wa Kanisa Katoliki kuhusu ushoga?'. Wote walitegemea kauli kali dhidi ya mashoga, lakini Papa Francis alijibu kwa unyenyekevu, na kusema,
'Ni nani mimi basi hata niwe na mamlaka ya kumhukumu mwanadamu mwenzangu?. Kazi ya Kanisa ni kutoa mafundisho sahihi kwa kadiri ya mpango wa Mungu. Kazi ya kuhukumu ni ya Nungu Mwenyewe'.
Kwa mafundisho ya Mungu, ushoga, kama ilivyo uzinzi, uuaji, uasherati, uwongo, uabudu sanamu au wizi, zote ni dhambi. Na kwa mafundisho ya Mungu, katika dhambi hizi hakuna iliyo afadhali au ndogo kuliko nyingine. Dhambi kubwa kuliko zote ni kumkufuru Roho Mtakatifu.
Ushoga kama ulivyo uzinzi au uasherati, ulikuwepo, na upo mpaka sasa miongoni mwa watu wetu, na utaendelea kuwepo mpaka siku ya hukumu.
Watu wasipotoshe mafundisho ya Mungu kwaajili ya kutafuta kuungwa mkono kisiasa.
Tatizo letu kama Taifa, siyo ushoga, bali ni uonevu, kukosekana kwa haki, mauaji, utekaji, ufisadi, wizi, uminywaji wa uhuru na demokrasia, umaskini na kukosekana kwa utawala wa sheria. Haya yanatuathiri sote kama Taifa. Ushoga kama ulivyo uzinzi au ulevi, vinafanyika kwa mtu mmoja mmoja, kwenye nafsi na mwili wake, haufanyiki kwetu sote. Ndiyo maana, kama Taifa, hatuumizwi moja kwa moja na ushoga wa mtu au uzinzi wake.
Serikali ijibu hoja za msingi zilizoanishwa na Bunge la Ulaya, na ambazo, hata humu ndani ya Taifa letu, wanaolipenda Taifa hili wamelalamikia sana hayo mambo 14.
Na serikali itambue kuwa, Mtanzania yeyote mwenye mapenzi mema na Taifa hili, mzalendo wa kweli, mwenye kujitambua, hakuna hata mmoja anayeunga mkono mambo hayo 14 yaliyoanishwa na EU dhidi ya serikali. Na kama serikali itashupaza shingo, kwa lolote lijalo mbeleni, haitakuwa na watu makini wa kuiunga mkono kutetea uhalifu wa serikali dhidi ya wananchi wake yenyewe.
Swali:
Je, kama baba yangu anawatesa wadogo zangu, namshauri hanisikilizi. Naendelea kumshauri, baadaye anaamua kuwaua baadhi ya wadogo zangu, na wengine anawajeruhi vibaya, majirani wakaona, wanaamua kuwatetea wadogo zangu wanaoteswa, na wanataka Baba awajibike kwa kuwaua watoto wake, Mimi kama mtoto nitasimama na baba aliyewaua na kuwajeruhi wadogo zangu au nitaungana na majirani ili kuwaokoa wadogo zangu walio kwenye hatari ya kifo?
Hapo ndiyo unaweza kutambua mtoto mwenye akili na aliye taahira .
Kama hatuwadhalilishi wazinzi, kwa nini tuwadhalilishe mashoga?
Kama hatuwadhalilishi wauaji, watekaji na wanaopoteza watu, kwa nini tunadhani ni sahihi kuwadhalilisha mashoga?
Kama hatuwadhalilishi waongo, kwa nini tunadhani tuna haki ya kuwadhalilisha mashoga?
Kama waumini na kama Taifa, tunawajibu wa kuwatendea haki watu wote japo hatuwezi kuzitambua zinazoitwa haki za mashoga kama vile ndoa za jinsia moja.
Kwa mtazamo wa kiimani pia, anayekuonya ulipokengeuka ametimiza wajibu wake kama mtu wa Mungu. Hawa EU na US kuionya serikali dhidi ya uovu walioutaja katika mambo niliyoyaweka hapo juu, wametimiza wajibu wao kama wana wa Mungu. Serikali yetu kwa kuyatenda hayo mambo, hakika inatenda mapenzi ya ibilisi. Serikali ina maamuzi, au kusikia sauti yenye ujumbe wa Kimungu au kuendelea kumtumikia shetani lakini mwisho wake ni mauti. Shetani hampeleki mwanadamu mbinguni/ahera bali kwenye jehanamu
Mwenye Masikio na Asikie.