Blackcornshman
JF-Expert Member
- Aug 25, 2016
- 6,098
- 13,999
Hakukosea Tanzania hamna Corona, kuna changamoto za upumuaji alizopata Philip na kujitokeza live kwenye vyombo vya habari kukana kifo na uzushi wa Corona.Zidumu fikra za Magufuli.Magufuli hakuwa dikteta, na binafsi nadhani Tanzania imekosa kiongozi mzuri sana. Alikuwa na madhaifu machache, lakini alikuwa kiongozi mzuri na tabiti sana wa nchi. Dhaifu lake la kwanza ni alikuwa hapendi kukosolewa, na nadhani hilo ndilo lilikuwa dhaifu kubwa sana kwake ambalo lilizaa tatizo la kutaka kusifiwa tu. Dhaifu la pili lilikuwa ni lile la kupendelea sana kwao kupita kiasi mpaka kufanya jambo hilo liwe ni kwenye headlines, halafu tatizo la tatu ni kuwa hakuwa anajua kuchagua maneno mazuri ya kutumia katika kupinga jambo. Magufuli hakujua kupinga jambo diplomatically, hivyo alikuwa akisound kuwa kila jamboasilopenda yeye ilikuwa ni ugomvi kwake. Nyerere alijua sana kumwambia mtu kistaarabu kwa lugha ya kirafiki ambayo mtu aliyeambiwa hatarudia; Magufuli alikuwa anamtishia mtu aogope na asirudie kumwuliza.
Sasa tatizo la kutaka kusifiwa tu lilimfanya atoe uamuzi mmoja mbaya sana kuhusu korona kwa kuangalia matokeo ya uchumi zaidi, hasa ile miradi aliyokuwa ameanzisha. Hata kama uamuzi wake ulikuwa siyo mbaya, aliutoa kwa kutumia lugha iliyomfanya awe ni laughing stock duniani ingawa alikuwa na nia njema. Angechagua maneno mazuri ya kutumia, asingejulikana hivyo. Kwa mfano angesema kutu kuwa hili gonjwa lipo; wamamcho tupambane nalo kwa kadha kadha lakini tusijifugiea nadi, angeelewa kuliko kuitangazaia dunia kuwa Tanzania hatuna gonjwa hilo, na hiyo ndiyo alama ya muda mrefu aliyoacha kwenye legacy yake.
Friction zake na wanasiasa wenzake naziona jambo la kawaida kabisa kwani siasa ni kusihindana na kukabana; kila mmwanasiasa hutaka kufunga goli.