Tetra
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 1,526
- 771
Sofia alikuwa msichana mwenye tabasamu,mchangamfu na mwepesi sana wa kupata marafiki.
Katika umri wa miaka 16 umbile lake lilikuwa sawa na binti aliyetayari kuolewa na kuanza majukumu ya familia.Kisheria isingewezekana na pia kwa muda huo alikuwa bado yu masomoni,kidato cha pili
.........Ingawa Sofia alikuwa na furaha lakini furaha hiyo haikuwa ya kweli.Alikuwa na tatizo moyoni mwake.Tatizo ambalo ni mama yake tu alitakiwa kulijua.Hata rafiki yake wa karibu sana asingeweza kumweleza.Alimfuata mama yake,ambaye alikuwa sebuleni akiweka vizuri nywele zake,,huku akimwitikia bintiye Sofia pasipo kugeuka kumtazama maana alimwona kwenye kioo chake kikubwa cha kujitazama.
........Sofia alisema "Mama,naomba niwe na mazungumzo na wewe unishauri".Mama Sofi aliangalia mwanga wa jua na kuona muda hautoshi kuongea na binti yake.Alimjibu bintie kwa ufupi tu,"Subiri nikirudi".
......Naam Sofia alimsubiri mama yake akiwaza akilini mwake jinsi ya kumweleza tatizo lake.Hata Mama Sofia aliporudi hakukumbuka ahadi yake kwa bintie.Aliendelea tu kumalizia kazi za ofisini kwenye laptop yake na kupokea simu za rafiki zake.Mambo mengine ya jikoni aliyamaliza house girl
.....Sofia aliendelea kumkumbusha Mama yake ila majibu ya Mama yake yalikuwa rahisi tu "Baadae,subiri,kama ni pesa ntakuachia mezani'' Majibu haya hayakuwa msaada kwa binti huyu bali yalimsaidia mama yake.Na Sofia alikuwa amekata shauri kutosema tena.
......Majibu ya mkato,Kujifanya anajua tatizo alilokuwa anapitia,kulimfanya Sofia alie,asile wala asiende shule kwa muda pasipo Mama yake kujua.Naam aliamua sasa!
.......Mama Sofia ambaye alikuwa Sekretari wa Mkurugenzi,asubuhi ya saa 3,alikuwa ameamua kumsikiliza binti yake na Kumwonyesha Upendo wake ulivyo mkubwa kwa bintie.Kabla hajapiga simu kumuita bintie wakutane kwenye Lunch ili wazungumze,,alitabasamu alipoona jina la binti likiita ktk simu yake,alipoipokea sauti haikuwa ya bintie bali ya house girl aliyemtaarifu kuwa Sofia alikuwa amekunywa sumu na kujiua.Alizimia
......Mama Sofia alizinduka akiwa hospitalini,ktk wodi ya wanawake na binti yake akiwa kitanda jirani.Jitihada za madaktari kuokoa uhai wa binti Sofia ziligonga mwamba.Tayari alikuwa ametangulia mbele ya haki,na kuacha ujumbe mzito kwa jamii "NIMEJIUA KWA SABABU NINA MIMBA YA BABA YANGU"
......
Naam,Mama Sofia alitaka kuonyesha upendo kwa bintie,lakini Upendo wake ulikuwa umechelewa.
::
NAAM WAZAZI wakati mwingine tuna MUDA mwingi lakini hatuna muda wa kuzungumza na watoto wetu.Ofisini ni nyumbani na nyumbani ni ofisini.Tunawaletea watoto wetu zawadi nzuri lakini tunasahau kuwapa zawadi bora ya Muda wa kujua wanafikiri nini,wana hisia zipi na wanafikiri nini kuhusu sisi.
NAAM,,TUONYESHE UPENDO WETU kwa kutenga muda kwa watoto kabla hatujachelewa !!
=