Laiti nisingeandika bandiko hili labda Ben Sanane asingepotea

Habari wanabodi

Leo nilikuwa nikipitia "threads" zangu mbalimbali ambazo niliwahi kuandika hapa JF. Nimejikuta nikisononeka baada ya kuiona "thread" yangu moja yenye kichwa hiki, "Nitapata wapi chapisho la kitaaluma la Dr. Joseph Pombe Magufuli?"

Nilipoandika uzi huu, wadau walinielekeza wapi ambapo ningeweza kupata nilichokuwa nakitafuta. Kweli niliipata "thesis" iliyompa Rais Magufuli PhD. Baada ya kuipata nikaisoma, nilikuja na uzi mwingine ambao ulikuwa na kichwa hiki "Nimelipata andiko la Dr. Joseph Pombe Magufuli" ambao ndani yake niliongelea kwa nini mheshimiwa Rais asiitafsiri "thesis" yake katika vitendo ili kuiongeza korosho thamani. Kwa maana kwamba sasa mbali na korosho yenyewe, tungeweza kupata mafuta ya kuzuia kutu kutokana na maganda yake. Ule uzi nadhani baadaye mods waliufuta baada ya kubeba sura nyingine kutokana na baadhi ya watu kuanza kuhoji uhalali wa PhD ya mheshimiwa.

Kilichonifanya nisononeke moyo wangu ni pale nilipowaza kuwa yawezekana nyuzi zangu hizo ndizo zilizokuwa chanzo cha mawazo ya kuhoji uhalali wa PhD za watu. Na matokeo yake ndiyo kutoweka kwa mtu aliyelishikia bango jambo hili. Naomba nieleweke vyema kuwa simaanishi kuwa waliompoteza Ben ni wale ambao alihoji uhalali wa PhD zao, la hasha, hata watu wengine wanaweza kumpoteza kwa kuwa tu alishajenga sura ya kuhoji jambo ambalo lingeweza kumletea matatizo.

Mwisho niombe jeshi la polisi litupe mrejesho wa wapi ulipofikia upelelezi wa upotevu wa Ben Sanane.
Usiogope kusema ukweli kuwa waliomsababishia umauti ndio wabaya tundu lissu
 
Too late to apologize. Asante lakini kwa mawazo haya.
 
Yaani kama wameshindwa waseme tuombe msaada interpol tu na kwengineko. Sidhani kama angepotea mtu ccm ingefika zaidi ya miezi 6
 
Kubenea alisema Ben ana onekana kwenye vijiwe vya kahawa...
 
Kweli niliipata "thesis" iliyompa Rais Magufuli PhD. Baada ya kuipata nikaisoma, nilikuja na uzi mwingine ambao ulikuwa na kichwa hiki "Nimelipata andiko la Dr. Joseph Pombe Magufuli" ambao ndani yake niliongelea kwa nini mheshimiwa Rais asiitafsiri "thesis" yake katika vitendo ili kuiongeza korosho thamani. Kwa maana kwamba sasa mbali na korosho yenyewe, tungeweza kupata mafuta ya kuzuia kutu kutokana na maganda yake. Ule uzi nadhani baadaye mods waliufuta baada ya kubeba sura nyingine kutokana na baadhi ya watu kuanza kuhoji uhalali wa PhD ya mheshimiwa.
72debee0f589d5f79866e49ce9b738bb.jpg

Kwa hisani ya Nonda
 
Habari wanabodi

Leo nilikuwa nikipitia "threads" zangu mbalimbali ambazo niliwahi kuandika hapa JF. Nimejikuta nikisononeka baada ya kuiona "thread" yangu moja yenye kichwa hiki, "Nitapata wapi chapisho la kitaaluma la Dr. Joseph Pombe Magufuli?"

Nilipoandika uzi huu, wadau walinielekeza wapi ambapo ningeweza kupata nilichokuwa nakitafuta. Kweli niliipata "thesis" iliyompa Rais Magufuli PhD. Baada ya kuipata nikaisoma, nilikuja na uzi mwingine ambao ulikuwa na kichwa hiki "Nimelipata andiko la Dr. Joseph Pombe Magufuli" ambao ndani yake niliongelea kwa nini mheshimiwa Rais asiitafsiri "thesis" yake katika vitendo ili kuiongeza korosho thamani. Kwa maana kwamba sasa mbali na korosho yenyewe, tungeweza kupata mafuta ya kuzuia kutu kutokana na maganda yake. Ule uzi nadhani baadaye mods waliufuta baada ya kubeba sura nyingine kutokana na baadhi ya watu kuanza kuhoji uhalali wa PhD ya mheshimiwa.

Kilichonifanya nisononeke moyo wangu ni pale nilipowaza kuwa yawezekana nyuzi zangu hizo ndizo zilizokuwa chanzo cha mawazo ya kuhoji uhalali wa PhD za watu. Na matokeo yake ndiyo kutoweka kwa mtu aliyelishikia bango jambo hili. Naomba nieleweke vyema kuwa simaanishi kuwa waliompoteza Ben ni wale ambao alihoji uhalali wa PhD zao, la hasha, hata watu wengine wanaweza kumpoteza kwa kuwa tu alishajenga sura ya kuhoji jambo ambalo lingeweza kumletea matatizo.

Mwisho niombe jeshi la polisi litupe mrejesho wa wapi ulipofikia upelelezi wa upotevu wa Ben Sanane.
Isomwe albadir nyingine ya kupotea kwa Ben halafu tusubirie majibu kwa hamu,atakaevaa chupi kichwani ndio mhusika.
 
Kwaiyo unajifanya una guilty conscience,umeandika ili tukuhurumie,,au unatafuta tu credit ,i dont understand the motive of this post,is this a history lesson,or maybe you want to rise the issue of the mheshimiwa's edu-history,,,;au lbda unatest kuona kama kuoņgea tena na ww utapotea kama Ben....fafanua mzazi,nn kimekusukuma?
 
Ni kosa kubwa sana walilofanya watekaji wa Ben Saanane.

Nina uhakika kuna watu wengi tu hatari zaidi ya Ben ambao hata hawajihusishi na siasa, watakuwa wameguswa na hilo jambo.

Kwakifupi ni sawa na kuzalisha Ben Saanane wengi na hatari zaidi.

Ni hulka ya binadamu kutokutaka kuona uonevu au ukandamizaji dhidi ya binadamu wengine.
 
Habari wanabodi

Leo nilikuwa nikipitia "threads" zangu mbalimbali ambazo niliwahi kuandika hapa JF. Nimejikuta nikisononeka baada ya kuiona "thread" yangu moja yenye kichwa hiki, "Nitapata wapi chapisho la kitaaluma la Dr. Joseph Pombe Magufuli?"

Nilipoandika uzi huu, wadau walinielekeza wapi ambapo ningeweza kupata nilichokuwa nakitafuta. Kweli niliipata "thesis" iliyompa Rais Magufuli PhD. Baada ya kuipata nikaisoma, nilikuja na uzi mwingine ambao ulikuwa na kichwa hiki "Nimelipata andiko la Dr. Joseph Pombe Magufuli" ambao ndani yake niliongelea kwa nini mheshimiwa Rais asiitafsiri "thesis" yake katika vitendo ili kuiongeza korosho thamani. Kwa maana kwamba sasa mbali na korosho yenyewe, tungeweza kupata mafuta ya kuzuia kutu kutokana na maganda yake. Ule uzi nadhani baadaye mods waliufuta baada ya kubeba sura nyingine kutokana na baadhi ya watu kuanza kuhoji uhalali wa PhD ya mheshimiwa.

Kilichonifanya nisononeke moyo wangu ni pale nilipowaza kuwa yawezekana nyuzi zangu hizo ndizo zilizokuwa chanzo cha mawazo ya kuhoji uhalali wa PhD za watu. Na matokeo yake ndiyo kutoweka kwa mtu aliyelishikia bango jambo hili. Naomba nieleweke vyema kuwa simaanishi kuwa waliompoteza Ben ni wale ambao alihoji uhalali wa PhD zao, la hasha, hata watu wengine wanaweza kumpoteza kwa kuwa tu alishajenga sura ya kuhoji jambo ambalo lingeweza kumletea matatizo.

Mwisho niombe jeshi la polisi litupe mrejesho wa wapi ulipofikia upelelezi wa upotevu wa Ben Sanane.
Kama ulimsikia Zitto kwenye BUNGE aliwahi kusema Polisi wamenawa Mikono kwamaana Upelelezi wao ulionyeshwa jamaa aliokotwa Usalama wa Taifa na haijakanushwa mpaka leo!
 
Back
Top Bottom