Laiti nisingeandika bandiko hili labda Ben Sanane asingepotea

Laiti nisingeandika bandiko hili labda Ben Sanane asingepotea

Mkuu, you can kill my body but you can't kill my spirit

Kwa sasa ishi kwa tahadhari ndugu yangu Tanzania si salama wauaji wako kila kona.Hawajali kama unamali au Haina.Wako tayari kukufilisi hata kama una hodhi Mpaka wako mmoja tu
 
Ni kosa kubwa sana walilofanya watekaji wa Ben Saanane.

Nina uhakika kuna watu wengi tu hatari zaidi ya Ben ambao hata hawajihusishi na siasa, watakuwa wameguswa na hilo jambo.

Kwakifupi ni sawa na kuzalisha Ben Saanane wengi na hatari zaidi.

Ni hulka ya binadamu kutokutaka kuona uonevu au ukandamizaji dhidi ya binadamu wengine.

Kuna siku damu za wanaouawa zitajipigania maana kwa.watanzania hakuna atakayethubutu kuwatetea wanaouawa leo kwa visingizio mbali mbali.Ila siku moja.unakuja ambao wataipigania haki yao kuendelea kuishi kwenye nchi yao
 
Mkuu sio fair kabisa wazazi wake wako pain wewe unaleta utani

Usishangae huyo. Kwake Chama ni bora kuliko uhai wa Mtanzania ambaye wanatofautiana Itikadi.

Ukishakuwa na itikadi tofauti na CCM haki yako ni Kaburi.Hope siku moja Mungu aliyehai atatupa Uhuru wa kweli wa Taifa letu
 
Hakuna kitu kibaya kama kujivika Ukiristu huku ukiwa muuaji. Inauma sana hasa nikizisoma amri kumi za mungu na majina ya watakatifu akiwemo mtakatifu Paul, Papa John Paul II
 
Habari wanabodi

Leo nilikuwa nikipitia "threads" zangu mbalimbali ambazo niliwahi kuandika hapa JF. Nimejikuta nikisononeka baada ya kuiona "thread" yangu moja yenye kichwa hiki, "Nitapata wapi chapisho la kitaaluma la Dr. Joseph Pombe Magufuli?"

Nilipoandika uzi huu, wadau walinielekeza wapi ambapo ningeweza kupata nilichokuwa nakitafuta. Kweli niliipata "thesis" iliyompa Rais Magufuli PhD. Baada ya kuipata nikaisoma, nilikuja na uzi mwingine ambao ulikuwa na kichwa hiki "Nimelipata andiko la Dr. Joseph Pombe Magufuli" ambao ndani yake niliongelea kwa nini mheshimiwa Rais asiitafsiri "thesis" yake katika vitendo ili kuiongeza korosho thamani. Kwa maana kwamba sasa mbali na korosho yenyewe, tungeweza kupata mafuta ya kuzuia kutu kutokana na maganda yake. Ule uzi nadhani baadaye mods waliufuta baada ya kubeba sura nyingine kutokana na baadhi ya watu kuanza kuhoji uhalali wa PhD ya mheshimiwa.

Kilichonifanya nisononeke moyo wangu ni pale nilipowaza kuwa yawezekana nyuzi zangu hizo ndizo zilizokuwa chanzo cha mawazo ya kuhoji uhalali wa PhD za watu. Na matokeo yake ndiyo kutoweka kwa mtu aliyelishikia bango jambo hili. Naomba nieleweke vyema kuwa simaanishi kuwa waliompoteza Ben ni wale ambao alihoji uhalali wa PhD zao, la hasha, hata watu wengine wanaweza kumpoteza kwa kuwa tu alishajenga sura ya kuhoji jambo ambalo lingeweza kumletea matatizo.

Mwisho niombe jeshi la polisi litupe mrejesho wa wapi ulipofikia upelelezi wa upotevu wa Ben Sanane.
Igeni siasa za mbowe huwa hakashifu viongozi!!! Sasa ninyi Vijana munaotafuta umaarufu mnapayuka, ndo maana yanawakuta hayo mnayotafuta
 
Kwaiyo unajifanya una guilty conscience,umeandika ili tukuhurumie,,au unatafuta tu credit ,i dont understand the motive of this post,is this a history lesson,or maybe you want to rise the issue of the mheshimiwa's edu-history,,,;au lbda unatest kuona kama kuoņgea tena na ww utapotea kama Ben....fafanua mzazi,nn kimekusukuma?
Wakati mwingine tumia akili yako kuelewa, kama hujaelewa unaweza kumuuliza jirani yako unayemkubali kuwa ana IQ kubwa kuliko yako. Nadhani utakuwa ulifundishwa huko shule ya msingi kutafuta kichwa cha habari katika kipengele cha ufahamu.
 
Back
Top Bottom