Laiti kama Magufuli angekuwa member wa JamiiForums...

Jimmy George

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
1,733
1,648
Habari wana-JF
Humu JF ni sehemu ambayo watu tunajifunza,tunaelimika,tunaburudika na mengineyo mengi. Mimi binafsi nimepata elimu kubwa na nimejifunza mengi niliyokuwa cyajui mwanzo.

Laiti kama Magufuli angekuwa member wa JF nadhani angenufaika na yafuatayo;
1.Angejua ukweli wa hali iliyopo mitaani kwetu na kujua mitazamo ya wananchi wake
- inawezekana wasaidizi/washauri wake wanamwambia mambo tofauti au kumshauri kwa kuogopa kutumbuliwa

2. Angekuwa anakubali kukukosolewa
-member akitoa uzi lazima kuna watu watakubali au kupinga hata kama yuko sahihi na hii kwa upande wa mhe. kungemsaidia kuzoea hali ya kukosolewa.

3.Angejua madhara ya kuongea kitu bila utafiti
-humu JF ukisema kitu usicho na uhakika utakumbana na shahidi mbalimbali na kama mhe angekuwa humu wala asingesema kuwa Italy haijawajengea watu wake nyumba.

4. Angekuwa anapima kauli zake kabla ya kuongea
-JF ukileta uzi utakaokera watu wengi lazima uwe banned na mhe angeizoea hali hii hata katika kauli angekuwa anapima ili asiwe banned kwenye akili zetu

5. Angejua ni kwa kiasi gani maisha ni magumu mtaani
-Vijana wengi wanaosubiri ajira huwa wanamchukia sana humu JF na hao ndiyo huanzisha mijadala vijiweni na kusababisha aonekane anachukiwa labda angejifikiria kutoa ajira mapema

6. Angejua kuwa si mtu mmoja anaweza kujua kila kitu
-JF kuna watu aina mbalimbali na wenye uelewa na ujuzi tofauti na ndiyo maana hata forums zipo tofauti na kila forum ina wenyewe wanaoiwezea.

7. Angeona umuhimu wa kuwapa uhuru wapinzani
-JF pale unapokosolewa ndipo unajua umekosea wapi na kipi urekebishe na hii ingemsaidia mhe kujua wapinzani wanakosoa mambo gani na yapi ayarekebishe

Na kuna mengine mengi ambayo yangemsaidia mtukufu
 
Awe member mara 2? Au kwa sababu hatumii verified user? Yupo sana huku jukwaani na anapachukia balaa maana humu watu wananyoosha maelezo ile mbaya. Huoni Mello anakutana na wakati mgumu?
Atulie tu apate elimu ya kuwa na busara kwa sababu bila hii JF hata kujisifia kwake sijui atakuwa anaweka wapi taarifa zake.
Kila siku barua za ikulu kuhusu kutumbua/teuzi tunaziona huku au hata hilo hataki
 
Bado anafanya mawasiliano na malaika wa mitandao.....sasa sijui mbingu bado zinatafakari umuhimu wa kumtuma malaika wa kuzima mitandao!!
 
Habari wana-JF
Humu JF ni sehemu ambayo watu tunajifunza,tunaelimika,tunaburudika na mengineyo mengi. Mimi binafsi nimepata elimu kubwa na nimejifunza mengi niliyokuwa cyajui mwanzo.

Laiti kama Magufuli angekuwa member wa JF nadhani angenufaika na yafuatayo;
1.Angejua ukweli wa hali iliyopo mitaani kwetu na kujua mitazamo ya wananchi wake
- inawezekana wasaidizi/washauri wake wanamwambia mambo tofauti au kumshauri kwa kuogopa kutumbuliwa

2. Angekuwa anakubali kukukosolewa
-member akitoa uzi lazima kuna watu watakubali au kupinga hata kama yuko sahihi na hii kwa upande wa mhe. kungemsaidia kuzoea hali ya kukosolewa.

3.Angejua madhara ya kuongea kitu bila utafiti
-humu JF ukisema kitu usicho na uhakika utakumbana na shahidi mbalimbali na kama mhe angekuwa humu wala asingesema kuwa Italy haijawajengea watu wake nyumba.

4. Angekuwa anapima kauli zake kabla ya kuongea
-JF ukileta uzi utakaokera watu wengi lazima uwe banned na mhe angeizoea hali hii hata katika kauli angekuwa anapima ili asiwe banned kwenye akili zetu

5. Angejua ni kwa kiasi gani maisha ni magumu mtaani
-Vijana wengi wanaosubiri ajira huwa wanamchukia sana humu JF na hao ndiyo huanzisha mijadala vijiweni na kusababisha aonekane anachukiwa labda angejifikiria kutoa ajira mapema

6. Angejua kuwa si mtu mmoja anaweza kujua kila kitu
-JF kuna watu aina mbalimbali na wenye uelewa na ujuzi tofauti na ndiyo maana hata forums zipo tofauti na kila forum ina wenyewe wanaoiwezea.

7. Angeona umuhimu wa kuwapa uhuru wapinzani
-JF pale unapokosolewa ndipo unajua umekosea wapi na kipi urekebishe na hii ingemsaidia mhe kujua wapinzani wanakosoa mambo gani na yapi ayarekebishe

Na kuna mengine mengi ambayo yangemsaidia mtukufu
Yupo.anatumia nick name.
 
we mtoa posti unasemaje mimi nipo au unataka na wewe nikutumbue nitalifunga hilo lijamii forum lenu
 
Mi nadhani kama yupo awe anatoa nyuzi kwa Id feki kuhusu mambo yanayohusu nchi na utawala akiwa anamtetea rais na kuyasema mawazo yake tujadili kisha ayafanyie kazi..Akifanya hivyo atakuwa na urahisi wa kuwasiliana na wananchi wa kawaida kwa urahisi zaidi,pasi na mtu yeyote kujua.
 
Ni kweli kabisa hayo uliyoyasema ni njia nzuri
 
Back
Top Bottom