Lafudhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lafudhi

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Swts, Mar 17, 2012.

 1. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  >Nini chanzo cha lafudhi?
  >Kwanini lafudhi ya watu wa mkoa fulani hutofautiana na mkoa mwingine?ilhali tu nchi moja
  Mfano,wamakonde,wachaga,wapemba,wazaramo,wangon, wanalafudhi tofaut kabisa,kwanin,nin tatizo ama tuseme chanzo
   
 2. mtu kitu

  mtu kitu JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 316
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  hii hutokana na lugha mama ama lahaja ya mtu anayozungumza. sio kwenye kiswahili pekee, mfano : wataliano wa Napoli hawatamki sawa na wataliano wa Milan
  Tanzania ni moja ila haina kabila moja ...kumbuka hilo
  Kiswahili ni lugha moja ila ndani yake kuna lahaja nyingi sana, na kila lahaja ina namna yake ya kutamka. mfano watu wa tanga na mombasa wanafanana kiasi kimatamshi. Dar na Unguja pia hufana kiasi fulani.(kwa kuwa Dar ni mji kubwa na kuna watu wa makabila mengi ,kwa hiyo pana mchanganyiko wa lafdhi)
   
 3. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Mtu kitu,dah asante man..kwel umejaa vitu kama hivyo sasa..
   
 4. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2013
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Athari ya lugha ya kwanza-au lugha mama ndio hufanya kuwepo na lafudhi mbalimbali. Na tofauti hizi zitaonekana tu pale wazungumzaji wenye lugha mama tofauti wanapozungumza lugha ambayo si yao kwa asili.
   
 5. Bisansaba

  Bisansaba JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2014
  Joined: Sep 4, 2013
  Messages: 327
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu ndo wewe ninaye kufahamu?
   
 6. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2014
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Mimi ndiye...
   
 7. Bisansaba

  Bisansaba JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2014
  Joined: Sep 4, 2013
  Messages: 327
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Aaah! Nakuona u mkongwe huku.
   
 8. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2014
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Kitambo sana poti, zamani kilikuwa kisima cha maarifa lakini sasa hivi uhanithi mtupu...
   
 9. Bisansaba

  Bisansaba JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2014
  Joined: Sep 4, 2013
  Messages: 327
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa nini mkuu?
   
 10. sajumo

  sajumo JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2014
  Joined: Nov 20, 2013
  Messages: 1,556
  Likes Received: 654
  Trophy Points: 280
  mie naona lafudhi inatokana na mazoea yanayorithishwa toka kizazi hadi kizazi, hii inatokana na hali ya jamii ilivyo mfano wamarekani lugha yao ni ya mkato mkato haraka na jazba iliyojificha.
  ingawa ni kiingereza kile kile jamaika pia wanakaribiana nao ingawa jamaika wamezidi ilitokana na kutokuelewana ambapo watu mara nying waliongea kwa kubishana na kurushiana maneno. tukiangalia watu wa mwambao walipata lugha laini kwa vle hawakuwa wafanya kaz ngumu pia waliishi maisha mazur kukaza kwa herufi imepatikana maeneo ya kaskazini kujionesha kuwa wao ni mashujaa hata kupitia sauti angalia hata wazulu wakiongea urithi wa hz lafudhi toka kizazi hadi kizaz umetufikisha hapa leo na ndio maana unakuta kuna watu wana lugha laini za kukaza za mkato na za kutirika na nyingne charehani watu wa vijiji kama bungu na maeneo kuizunguka rufiji na baadhi ya watu wa badgamoyo kifupi vijiji vya jirani na dar kupita coment nahs utafikiri beyound the ordinary.
  nahs lugha mama sio 7bu ya kuzuka kwa lafudhi
   
 11. sajumo

  sajumo JF-Expert Member

  #11
  Jun 5, 2014
  Joined: Nov 20, 2013
  Messages: 1,556
  Likes Received: 654
  Trophy Points: 280
  angalia watu wa dar wamezimaster lafudh za mikoa na lugha zote h inatokana na wao walirithishwa kila lafudhi leo h mtu wa dar anaweza kupretend upemba uchaga hata umakonde na akaweza ila hawez kutirika (cherehani) kama mkolesa hii ni kwa sababu mkolesa amekimaster kiswahili peke yake hvyo ni mtu ambaye anaongea faster hapa tz cjawaona mfanowe
   
 12. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2014
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Mambo yasiasa za propaganda yameshika hatamu sana, hii imepelekea watu makini ambao zamani walikuwa wanatoa michango maridadi kulikimbia jukwaa.
   
 13. Bisansaba

  Bisansaba JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2014
  Joined: Sep 4, 2013
  Messages: 327
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mi nafikiri hoa ndo wanatakiwa walishape jukwaa, kukimbia inamaanisha wamekubali kushindwa?
   
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2014
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Ulimi mama (mother tongue) una nguvu sana, mie hata unilaze Manhatani miaka mia nane, nikiongea lazima ugeuke.
   
 15. Bisansaba

  Bisansaba JF-Expert Member

  #15
  Jun 5, 2014
  Joined: Sep 4, 2013
  Messages: 327
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kitaaluma tungesema hivi:

  Lafudhi ni matamshi ya msemaji wa lugha fulani ambayo yanatokana na athari za kimazingira. Mazingira hayo yanaweza kuwa eneo atokalo mtu, mahali alikosomea, kiwango chake cha elimu, tabaka lake la kijamii na kadhalika.

  Kwa hiyo hapa chanzo kikubwa cha lafudhi ni mazingira alimo huyo mtumiaji lugha, mazingira hayo ni kama yalivyotajwa hapo juu. Lugha mama pia inaweza kuwa chanzo cha lafudhi tofautitofauti, kwa mfano katika kiswahili, hawa watu wakizungumza wazungumzaji wa kiswahili watajua wanatoka mkoa gani au ni kabila gani:


  1. Usiniretee maswara ya ubaguzi wa kikabira hapa
  2. Amemupiga mutoto ya watu juu amemuibia mfaranga makumi mawili
  3. Ukikaa nchale, ukichimama nchale
  4. Wewe unakamuaga mang'ombe tu moja kwa moja
  5. Mbona unakuwa kinganganizi, nilishakwambia sikupendi lakini wewe bado unaningangania tu!
  Lafudhi sio kitu kibaya, lakini pia huweza kubadilika kwa kutambua au bila kutambua (hii inaweza kutokea hadi umri wa miaka ishirini na). Lakini chanzo kikubwa cha lafudhi ni mzaingira alimo huyo mzungumzaji.
   
 16. Bisansaba

  Bisansaba JF-Expert Member

  #16
  Jun 5, 2014
  Joined: Sep 4, 2013
  Messages: 327
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu hapo kwenye mkolezo ungesema Lugha mama
   
 17. Bisansaba

  Bisansaba JF-Expert Member

  #17
  Jun 5, 2014
  Joined: Sep 4, 2013
  Messages: 327
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ndo kabila gani hilo mkuu
   
 18. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #18
  Jun 5, 2014
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Hili jukwaa ni 'user generated', yaani watumiaji ndio huamua nini kiwepo humu kwa kuwa wao ndio waandikaji. Sasa unakuta mtu anatoa hija za msingi, mwingine anakuja kunanga na hoja za kantangaze, kama unavyoona Bunge la Muungano. Katika hali hiyo mtu na akili zake anaona bora alisuse jukwaa tu...
   
 19. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #19
  Jun 5, 2014
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda no. 2 ambayo ni ya Kongo Mashariki...
   
 20. stable woman

  stable woman JF-Expert Member

  #20
  Jun 5, 2014
  Joined: Nov 12, 2013
  Messages: 3,356
  Likes Received: 3,213
  Trophy Points: 280
  Ebo! Kwahiyo mnapiga stori kwenye thread ya mwenzenu?
   
Loading...