Ladies understand your men (Wadada tu, wanaume marufuku) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ladies understand your men (Wadada tu, wanaume marufuku)

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Husninyo, Dec 16, 2011.

 1. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280


  Thread hii ni maalum kwa wadada hasa waliopo kwenye mahusiano ila bado hawajaolewa na wana mpango endelevu na wenza wao

  Wadada wengi wanashindwa kutambua wapi wanapendwa na wapi wanadanganywa. Vigezo vifuatavyo vitakusaidia kutofautisha mwanaume anayekupenda na mwenye mpango wa kukuoa na Yule anaekutumia tu ila hana mpango na wewe.
  Mawasiliano:
  Mwanaume anaekupenda hawezi kumaliza siku bila kuwasiliana na wewes (kama hakuna external factors zinazosababisha mawasiliano yawe mabovu). Kama wewe ni mtu wa kupiga simu kila siku, kutuma emails lakini mwenzio haoneshi ushirikiano ujue hapo kuna utata.
  Ushirikishwaji:
  Anaekupenda ni lazima atakushirikisha mambo yake mengi yawe makubwa au madogo. Unaweza shirikishwa kwa namna ya kuombwa ushauri au kupewa taarifa. Kama upo kwenye uhusiano ila unashangaa mambo yanafanyika tu bila kuelewa ujue haupo myoni mwake, haoni kama waweza mshauri la maana na haoni kuna umuhimu wa wewe kujua.
  Utambulisho.
  Jiangalie kama unatambulika kwa ndugu, rafiki na jamaa zake wa karibu. Kama muda wa kutambulishana rasmi kwa wazazi haujafika, vipi kwa marafiki, wafanyakazi wenzie au makaka na madada!!. Unawafamu marafiki zake wawili wakati anao 30? Utambulisho huwa ni swala gumu kama mwanaume hakupendi na hajivunii kuwa na wewe. mwanaume ambae tayari ana mpenzi mwingine na anatambulika kwa watu wake wa karibu ni mzito kukutambulisha na wewe. inabidi ustuke hapo.
  Mazingira.
  Unapafahamu anapoishi? Anapofanya kazi? Maeneo anayopenda kutembelea? Kama jibu ni hapana, unahisi ni kwa nini? Kuna sababu nje ya uwezo wenu zinazosababisha usifahamu hayo ulishamwomba ufahamu ila alikataa? Hapa nakuachia utafakari mwenyewe.
  Anakufahamu kiasi gani?
  Kama upo na mpenzi lakini haoneshi interests za kutaka kukufahamu zaidi inabidi ujiulize mara mbili mbili. Kwa mfano, mpenzi wako anajua jina lako na mahali unapoishi tu. Hajui mazingira unayoishi, kazi unayofanya, hajui ndugu zako hata kwa kuwasikia ujue huyo mwanaume hakupendi. Anaekupenda ataandika kitabu kizima kukudescribe lakini asiyekupenda hata page 1 haitojaa.
  Ubahili/ubinafsi
  Hapa ni kwa wenye wapenzi wenye uwezo mzuri kifedha. Angalia kama anasikiliza shida zako na kujaribu kuzitatua. Inawezekana hakujali na hakuhudumii kipesa kwa sababu ana mpenzi mwingine ambae ameelekeza huko matumizi yake. Pengine hakuamini, anahisi hata akikuhudumia utamtosa; ila kama anashindwa kukuamini anawezaje kukupenda? Mtu wa hivyo hata upendo wake ni wa mashaka. Kama hana uwezo kifedha je anakuwa na wewe bega kwa bega unapokuwa na shida? Anayekupenda atakujali wakati wa shida na raha.
  Ameoa.
  Kama Unahitaji life partner halafu una date mume wa mtu ujue umepotea. Cha mtu ni cha mtu na mwanaume haoi kwa bahati mbaya. Probability ya kuolewa na huyo mwanaume ni 0.000000000000001. hapa huitaji kuambiwa jua linawaka au mvua inanyesha. Akili kichwani mwako.
  NB: kigezo kimoja hakitoshi kuconclude kuwa hupendwi. Usisubiri mpaka mwanaume akutamkie kuwa hakupendi. Katika vigezo vyote hivyo nina mifano ya ukweli ambayo imewahi kunikuta mimi, ndugu zangu na marafiki.
  KWA WALIOOLEWA:
  Mnaweza kutuambia mlipima vipi upendo wa wenzi wenu hadi kuona kuwa wanafaa kuwa husbands.
  KWA WANAUME:
  Haina ubishi kwamba mmekuja kuchungulia, haya semeni kama una date na binti ambae huna mpango wa kumuoa huwa mnabehave vipi? Au kaka zenu na marafiki wanawatreat vipi wapenzi wao wa mpito( najua huwa mnahadithiana. Lol)
  Nakaribisha maoni, nyongeza, masahihisho etc. karibuni, jisikieni kama mmeuanza mwaka mpya wa2012, anaetaka vinywaji achukue kwenye jokofu.
   
 2. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  asante husninyo kwa somo zuri.ila hicho kipengele sijakuelewa ni sehemu gani mwanaume wako anatakiwa akuhudumie ili uone kweli huyu sio bahili ? maana kuna wapenzi wengine mwanamke nae ana uwezo,wa kuvaa .kwenda saluni etc au anatakiwa tu akuhudumie haijalishi una hela au lah?
   
 3. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mimi sijachungulia ila nimesoma between line na hii Post yako ni useful kwa kila mtu, unajua kwa upande wangu huwa nina date na msichana mwingine ninapoona kero na maudhi yamezidi kwa GF wangu wa ukweli kwa hiyo huwa nafanya hivyo kupunguza stress... na muda mwingine kuna mabinti ambao huwa wanazimika wenyewe ingawa wanajua mimi nina kifaa changu tayari huwa najitahidi sana kuwapotezea lakini inakua ni ishu mwisho wake hua tunajikuta kwenye maugomvi na chuki zisizo na msingi.
  Mimi ni mstaarabu kwa GF hata kama na date na demu wa nje siwezi kupotelea huko kabisa
   
 4. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #4
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Dah! Genuinely I am lost at words...... Husny my niece... I LOVE this post... MARVELOUS!!!
   
 5. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ubahili wakti mwingine unaleta maana kuna mshikaji wangu ana demu wake, demu mam safi mshikaji mambo yake kawaida anategemea mshahara halafu na mzigo wa kuwatunza ndugu na jamaa zake upo juu yake lakini demu wake ana matumizi ya ovyo ile mbaya lakini demu hajali, unakuta demu anaomba elfu 50 kwa ajili ya kwenda kununua top ya kuvaa, mshikaji ana mdogo wake anaomba elfu 20 ya tuition inakua ishu.
   
 6. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  siamini kama upo ivo
  daaah nalog off umenisikitisha
   
 7. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Acha kudanganya wenzako! As it has always been, katika mahusiano MEN ARE AND WILL ALWAYS BE UNPREDICTABLE linapokuja swala la mahusiano!

  Samahani kwa kusoma post ya "wadada tu"!
   
 8. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  jamani sweetie usinifanyie hivyo, historia inaweza badilika vipi sikukuu ya Xmass tunaenda wapi sasa?
   
 9. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  he he he umenifuma kweli nilkuwa nachungulia....kwangu mimi umehit the right spots.ambaye simpendi huwa namtafuta tu pale ninapohitaji tunda tu,mida mingine namkaushia na akimaindi namwambia nipo bize sana
   
 10. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #10
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Baba_E IMO sababu they are unpredictable si ndio bora wazangatie hayo juu ili walau nafasi ya lack of predictability iwe minimized...
   
 11. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mimi ni mwanamke ila ukweli kutoka ndani ya moyo wangu sipendi wanawake wenye tabia ya kuomba pesa kwa wenzi wao.... Kwani yeye haoni umuhimu wa kukupa mpaka uombe?


  'Wanawake na maendeleo tufanye kazi, tusonge mbele'
   
 12. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #12
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sasa na wewe kero na maudhi zikizidi/yakizidi si muyaweke mezani muyamalize? Kudate na mwanamke mwingine ndio kumrekebisha mwenzio kama kakosea? Atajirekebishaje wakati huwi wazi?
   
 13. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #13
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  watoto wa dot com sie hata ukiyaweka mezani yataisha lakini baada ya siku kumi 3 hali ni ile ile.
   
 14. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #14
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Useful post.
   
 15. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #15
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  asante-source sred ya Lizzy
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Mbona hueleweki?? Title inasema ........(wadada tu, wanaume marufuku)..
  Enewei ngoja nijisevie kinywaji....!!
   
 17. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #17
  Dec 16, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Naruhusiwa kujibu kwa niaba ya Lizzy maana ndio mtarajiwa wangu...
   
 18. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #18
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Alijua kwa vyovyote vile wapiga chabo kama wewe Katavi lazima mzamie...lol
   
 19. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #19
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Ni hatari kuvaa kiatu kinachokubana kitaumiza mguu wako.Ni hatari zaidi kuvaa kiatu kikubwa zaidi yako utakiacha njiani.Ni mbaya sana kwenda dukani ukiwa hujui size ya kiatu chako unaweza kuchukua size si yako!Haipendezi kwenda dukani ukiwa unajua size yako kwani sio unayoifikiria!Vp haielewekieeee!Usiogope ndivyo ilivyo!Samawani najua nimeingingia choo cha kike!
   
 20. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #20
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hairuhusiwi manake bado hamjawa mwili mmoja...
   
Loading...