Laana ya Wachezaji wa Yanga SC Yaendelea Kuitafuna Azam FC

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Historia huwa haidanganyi hata siku moja. Unaweza ukawa unajiuliza tatiza la Azam FC ni lipi. Mpaka sasa na usiwe na jawabu la swali hilo.

Historia inatuambia kuwa kila nyakati au msimu ambao Azam FC wanamchezaji mmoja au zaidi walio wahi kucheza Yanga SC basi msimu huo huwa hawafiki mbali kimataifa.

Hakuna msimu ambao Azam FC aliwahi kuwa na mchezaji wa Yanga SC kwenye kikosi chao wakafanya vizuri kimataifa.

Na sio kimataifa tu, bali.hata kwenye LigiKUU Tanzania Bara.

Azam FC watafanikiwa endapo wataachana na wachezaji walio wahi kupitia Yanga SC.

Vinginevyo wawe tayari kuzoea hii laana ambayo itaendelea kuwatafuna mpaka kiama chao.

Asanteni Azam FC kwa kushiriki, sasa rudini kambini mkapande mikakati ya kutetea nafasi ya 2 kwa sababu Simba SC, Singada FG nao wanaitamani.

Alamsiki.
 
Hizo ni porojo na kelele ,Azam FC haijawahi kuwa na rekodi nzuri kimataifa na haitofautiani na YangaSC , bora hata Namungo waongee.
Ngao ya jamii fc! Yanga imekipiga fainali Shirikisho Africa na kushinda ugenini japo goli halikutosha unasema Haina rekodi nzuri kimataifa?

Kweli Simba wote Mbumbumbu mwenye akili mmoja tu Rage!

We utakuwa unaishi Malinyi tv hamna huko!
 
Ngao ya jamii fc! Yanga imekipiga fainali Shirikisho Africa unasema Haina rekodi nzuri kimataifa? Kweli Simba wote Mbumbumbu mwenye akili mmoja tu Rage! We utakuwa unaishi Malinyi tv hamna huko!
Imechukua miaka mingapi hadi mkafika fainali? Rekodi zenu zilikuwa sawa na Azam FC na kilichotokea msimu jana mmeweka rekodi kwa mara ya kwanza toka kuasisiwa kwa YangaSC.
 
Hivi shida ni nini.Hivi awa wanajua kwamba Ubora wa Mpira wetu unatokana na Timu zinazoshinda hizi mechi za kimataifa.
 
Hizo ni porojo na kelele ,Azam FC haijawahi kuwa na rekodi nzuri kimataifa na haitofautiani na YangaSC , bora hata Namungo waongee.
Yeah ni kweli aisee Azam FC na Yanga SC wote wako sawa.

Wanazidiwa kabisa na Namungo FC, kwa sababu Namungi FC aliwahi kucheza Fainali ya CAFCC ila Azam FC na Yanga SC hawajawahi kufika hatua hiyo kimataifa.
 
Hivi shida ni nini.Hivi awa wanajua kwamba Ubora wa Mpira wetu unatokana na Timu zinazoshinda hizi mechi za kimataifa.
Kama wataendelea kuokota mabaki ya Yanga SC wakidhani mafanikio yako ndani ya Wachezaji wa Yanga SC....

Basi wataendelea kuwa janvi la wageni kimataifa.
 
Kwahyo Namungo Wana historia nzuri kimataifa kuliko YANGA?? Ipi hiyo??
Nimecheka mimi.
20230621_215254.jpg
 
Historia huwa haidanganyi hata siku moja. Unaweza ukawa unajiuliza tatiza la Azam FC ni lipi. Mpaka sasa na usiwe na jawabu la swali hilo.

Historia inatuambia kuwa kila nyakati au msimu ambao Azam FC wanamchezaji mmoja au zaidi walio wahi kucheza Yanga SC basi msimu huo huwa hawafiki mbali kimataifa.

Hakuna msimu ambao Azam FC aliwahi kuwa na mchezaji wa Yanga SC kwenye kikosi chao wakafanya vizuri kimataifa.

Na sio kimataifa tu, bali.hata kwenye LigiKUU Tanzania Bara.

Azam FC watafanikiwa endapo wataachana na wachezaji walio wahi kupitia Yanga SC.

Vinginevyo wawe tayari kuzoea hii laana ambayo itaendelea kuwatafuna mpaka kiama chao.

Asanteni Azam FC kwa kushiriki, sasa rudini kambini mkapande mikakati ya kutetea nafasi ya 2 kwa sababu Simba SC, Singada FG nao wanaitamani.

Alamsiki.
Bila ya kua na hao wachezaji wa Yanga,ni mwaka gani Azam walifika mbali Kimataifa na walifika hatua gani ?
Yanga acheni wachezaji waende kwa amani bado mnawaandama tu ?
Azam wanafeli wenyewe yule kocha wao hana mbinu yoyote
 
Back
Top Bottom