Laana ya Wachezaji wa Yanga SC Yaendelea Kuitafuna Azam FC

Bila ya kua na hao wachezaji wa Yanga,ni mwaka gani Azam walifika mbali Kimataifa na walifika hatua gani ?
Yanga acheni wachezaji waende kwa amani bado mnawaandama tu ?
Azam wanafeli wenyewe yule kocha wao hana mbinu yoyote
Azam FC hajawahi kuanza msimu pasi na kuwa na mchezaji wa Yanga SC kwenye official squad yao.

Bisha kwa kuleta uthibitisho.
 
Historia huwa haidanganyi hata siku moja. Unaweza ukawa unajiuliza tatiza la Azam FC ni lipi. Mpaka sasa na usiwe na jawabu la swali hilo.

Historia inatuambia kuwa kila nyakati au msimu ambao Azam FC wanamchezaji mmoja au zaidi walio wahi kucheza Yanga SC basi msimu huo huwa hawafiki mbali kimataifa.

Hakuna msimu ambao Azam FC aliwahi kuwa na mchezaji wa Yanga SC kwenye kikosi chao wakafanya vizuri kimataifa.

Na sio kimataifa tu, bali.hata kwenye LigiKUU Tanzania Bara.

Azam FC watafanikiwa endapo wataachana na wachezaji walio wahi kupitia Yanga SC.

Vinginevyo wawe tayari kuzoea hii laana ambayo itaendelea kuwatafuna mpaka kiama chao.

Asanteni Azam FC kwa kushiriki, sasa rudini kambini mkapande mikakati ya kutetea nafasi ya 2 kwa sababu Simba SC, Singada FG nao wanaitamani.

Alamsiki.
Mbona hao wa Yanga ndio wamefunga hizo penati bangala ,na feisal wamepata.acha wivu roho ya mkaanga sumu
 
Mbona hao wa Yanga ndio wamefunga hizo penati bangala ,na feisal wamepata.acha wivu roho ya mkaanga sumu
Inahitaji akili kubwa kung'amua point kusudiwa hapi juu kwenye uzi.

Akili za panya haziwezi kujadili hoja ngumu kama hizi.

Rudi MMU.
 
Huyo kocha ni kiazi kabisa.... Anamtoa Akamiko anamuacha Fei uwanjani?, Unamtoa Nado ambaye alikuwa anawapa taabu mabeki?. Hapa sio swala la wachezaji wa yanga Wala nini, huyu kocha hovyoo kabisa. Feisal hapaswi kuanza kwenye kikosi Cha Azam Hana fitness ni kuzurula uwanjani tu.
 
Its actual beyond your thinking vacuum.

There is a curse in them.
 
Utopolo bhana kwa hiyo mnataka wachezaji wote wanaocheza hapo utopoloni wawe na akili kama za Ngasa ambae alitanguliza mapenzi kwa uto kuliko maisha yake. Mpira ni ajira na mchezaji anacheza popote penye masilahi.Kwa uchumi wa Utopolo sio timu kwa mchezaji kusema amefika bali ni njia tu.
 
Yeah ni kweli aisee Azam FC na Yanga SC wote wako sawa.

Wanazidiwa kabisa na Namungo FC, kwa sababu Namungi FC aliwahi kucheza Fainali ya CAFCC ila Azam FC na Yanga SC hawajawahi kufika hatua hiyo kimataifa.
Ndani ya kipindi cha miaka mitano Yanga SC amekusanya point msimu ulioisha kwenye michuano CAF,
huku. AZAM FC hana point hata moja.. Bora Namungo alivuna point 0.5 alipoingia makundi msimu 2021-2022
 
Azam FC hajawahi kuanza msimu pasi na kuwa na mchezaji wa Yanga SC kwenye official squad yao.

Bisha kwa kuleta uthibitisho.
Sina lengo la kubishana bali kuweka kumbukumbu sawa.
Andiko linasema Azam hawajawahi kufanya vizuri iwe kimataifa au ligi ya ndani wakiwa na wachezaji toka Yanga.
Hapa hapa unasema Azam hawajawahi kuanza msimu pasi na kua na mchezaji toka Yanga kwenye official squad yao.
Historia inanikumbusha kuwa Azam walikua mabingwa wa Ligi kuu Tanzania mwaka 2013/2014. Kwa mantiki hii hili andiko liko sawa ?
 
Historia huwa haidanganyi hata siku moja. Unaweza ukawa unajiuliza tatiza la Azam FC ni lipi. Mpaka sasa na usiwe na jawabu la swali hilo.

Historia inatuambia kuwa kila nyakati au msimu ambao Azam FC wanamchezaji mmoja au zaidi walio wahi kucheza Yanga SC basi msimu huo huwa hawafiki mbali kimataifa.

Hakuna msimu ambao Azam FC aliwahi kuwa na mchezaji wa Yanga SC kwenye kikosi chao wakafanya vizuri kimataifa.

Na sio kimataifa tu, bali.hata kwenye LigiKUU Tanzania Bara.

Azam FC watafanikiwa endapo wataachana na wachezaji walio wahi kupitia Yanga SC.

Vinginevyo wawe tayari kuzoea hii laana ambayo itaendelea kuwatafuna mpaka kiama chao.

Asanteni Azam FC kwa kushiriki, sasa rudini kambini mkapande mikakati ya kutetea nafasi ya 2 kwa sababu Simba SC, Singada FG nao wanaitamani.

Alamsiki.
Post ya kipumbavu ya mwaka
 
Hizo ni porojo na kelele ,Azam FC haijawahi kuwa na rekodi nzuri kimataifa na haitofautiani na YangaSC , bora hata Namungo waongee.
We acha kabisa kuifananisha timu iliyocheza final CAFCC kwa mara ya kwanza na viru vya hovyo mkuu
 
Kwahyo nyie ndo mnaowapiga juju...
Hapana.
20230517_210651.jpg
 
Back
Top Bottom