Laana na kuacha(kupiga kibuti)

Laana na kuacha(kupiga kibuti)

mayenga

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2009
Posts
4,118
Reaction score
1,973
Bandugu,

Nimekuwa nikijiuliza swali hili sipati jibu.Hivi kuna uhisiano wa mkosi na kumuacha au kuachwa na yule ambaye mlishakubaliana kuwa atakuwa au angekuwa ubavu wako?Wengi wetu tumekuwa tukidhani na pengine kuwa na fikra kuwa,kitendo cha kumbwaga yule mtu aliyeweka matumaini juu yako kinaweza kuleta mkosi na pengine laana katika maisha yako ya mahusiano.
 
100% we mtu kakuamini , kakufanyia maombia afu we kiraihisiii unakimbia, acha izo wewe mtu akiwa na kinyongo na wewe ni dhambi kwa Mungu...
 
Mimi naamini. Kama ulimwaminisha mwenzako kwamba wewe ndiye mwenza wake wa maisha na akakuamini halafu ukampiga kibuti bila ya sababu za msingi, laana itakuhusu.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Bandugu,

Nimekuwa nikijiuliza swali hili sipati jibu.Hivi kuna uhisiano wa mkosi
na kumuacha au kuachwa na yule ambaye mlishakubaliana kuwa atakuwa au
angekuwa ubavu wako?Wengi wetu tumekuwa tukidhani na pengine kuwa na
fikra kuwa,kitendo cha kumbwaga yule mtu aliyeweka matumaini juu yako
kinaweza kuleta mkosi na pengine laana katika maisha yako ya
mahusiano.

lazima ulaanike tu bora umwambie ukweli
 
kama ndoa inavunjika ambayo mtu aliapa kwenye madhabahu sembuse promise to marry tehe tehetehe,dua la kuku halimpati mwewe,ila inategemeana na viapo vyenu mlivyowekeana kama mlichanjiana damu hapo kazi ipo.
 
Bandugu,

Nimekuwa nikijiuliza swali hili sipati jibu.Hivi kuna uhisiano wa mkosi na kumuacha au kuachwa na yule ambaye mlishakubaliana kuwa atakuwa au angekuwa ubavu wako?Wengi wetu tumekuwa tukidhani na pengine kuwa na fikra kuwa,kitendo cha kumbwaga yule mtu aliyeweka matumaini juu yako kinaweza kuleta mkosi na pengine laana katika maisha yako ya mahusiano.

Hakuna uhusiano wowote hapa nadhani ni imani zetu tu.
 
kama ndoa inavunjika ambayo mtu aliapa kwenye madhabahu sembuse promise to marry tehe tehetehe,dua la kuku halimpati mwewe,ila inategemeana na viapo vyenu mlivyowekeana kama mlichanjiana damu hapo kazi ipo.

Eeeeh! Kuchanjiana damu tena?! Mbona unanitisha? Ndo inakuwaje hiyo? Naomba ujuzi wako kwenye hiyo kitu ili nione kama itanifaa.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
---> Kumchagua 'life partner' ni project muhimu sana na yenye changamoto...si muhimu kwanyie wawili mliokubaliana tu bali ni muhimu kwa jamii nzima. kwa sababu mtazaa watoto watakaoishi kwenye jamii hii, sisi ni marafiki, ndugu, wazazi na jamaa zenu so ni kazi kubwa kiukweli.

---> Binadamu hufanya makosa na kitu kikubwa Mungu alichotupa ni uwezo wa kurekebisha makosa tuliyofanya...make things right again.

--->SASA umefanya kosa katika kumchagua mwenza, ukaona ili kurekebisha ni kumuacha kwa manufaa yenu wawili na ya jamii...Hata akiacha laana na wewe ukakaa upande wa Mungu...Hatoacha kamwe zikupate. Period!!
 
Bandugu,

Nimekuwa nikijiuliza swali hili sipati jibu.Hivi kuna uhisiano wa mkosi na kumuacha au kuachwa na yule ambaye mlishakubaliana kuwa atakuwa au angekuwa ubavu wako?Wengi wetu tumekuwa tukidhani na pengine kuwa na fikra kuwa,kitendo cha kumbwaga yule mtu aliyeweka matumaini juu yako kinaweza kuleta mkosi na pengine laana katika maisha yako ya mahusiano.

Mkuu; unataka justification ya kusepa nini?
 
kama kweli laana ipo, huu mzigo wa laana nlojitwisha kuushusha....hadi winch!!!!
 
Sidhani kama kuna ukweli hapo...
Ndoa ni sehemu ambayo haipaswi kuwe na regrets, kama kuna mambo unaona hayajakaa sawa na hayawezi kaa sawa kwa nini ulazimishe ndoa hence kukosa upendo kwa muda wote uliobaki wa maisha.
 
Mimi naamini laana isiyo na sababu haimpati mtu,je sababu yenyewe ipi mfano mtu anamwacha mke kwasababu kapata nyumba ndogo anayo iona nzuri kuliko mkewe,kwa kweli hapo atapatikana na laana tu hata km si yy itakuwa kwa kizazi chake, mfano pia ukamuacha mke sbb ni mzinzi hapo hamna laana. Kwa wachumba kuna vitu mtu ulitakiwa kuvifanyia maamuzi toka mwanzo halafu unakuja kutolea maamuz wakati mwenzio keshatumbukia mwili wote aisee unaweza pata laana.kuna dada mmoja alipendwa na kijana mmoja hadi yule kijana kaenda kutoa mahali ktk harakati za maandalizi ya ndoa mwishoni yule msichana akambwaga sbb kwamba tu hajisikii kuwa naye kipindi hicho alikuwa na 23 yrs mpka leo huyo dada hajaolewa ana 45 yrs,yule mwanaume alioa mwingine na sasa ana watoto 3.Kama mtu hujampenda toka mwanzo mwambie kuliko ukamchuna wee/ukamchezea na kumzalisha juu halafu unammwaga,aisee hapo laana itakupata tu km si ww kizazi chako.
 
Ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga!Ni kweli laana inawezekana ipo,kuna dada mmoja alikua anafuatwa ili aoelewe.Kila aliyemuaprochi anamkatalia wakati yuko singo,wamwisho alikua tajiri mmoja hapa town.Nayeye alitoswa,alimuambia utanikumbuka.Mpaka sasa huyo dada kafika 42,bila mume wala mchumba. Sasa ana psychological problem,
 
mke/mume mwema hutoka kwa Mungu. Hamna laana hapo bcoz kila kitu hutokea kwa sababu chini ya jua. Ukiachwa ujue hukuandikiwa huyo.
 
kama umemwacha na umempa sababu ya mcingi naye kwa akili zake timamu akaliona hilo hakuna laana lakini ka ulienda kupast time then umtafutie sabau zisizokua na kichwa wala miguu wakati ye kajituliza itakukuta tu hutakiwi kumuacha binadam mwenzio na kinyongo
 
I would say inategemea sababu unayomwachia. Kama ni geniune haina laana, lakini kama ni ya kipuuzi kama kulewa penzi la kimada...u a in for it.
 
Back
Top Bottom