Laana katika mchezo wa soka

Billy Kimber

Member
May 20, 2022
89
193
Japo laana ni suala la kiimani na vitu vya kiimani ni ngumu kuvithibitisha,lakini kwa namna flani haya mambo ya laana yapo.

Mwaka 1962 baada ya taji lake la pili la kombe la Ulaya alilowafunga Real Madrid 5-3 kwenye fainali, kocha mkuu wa Benfica Bela Guttmann aliomba nyongeza ya mshahara kwa mabosi wa klabu lakini ombi lake lilikataliwa licha ya mafanikio makubwa aliyoipatia klabu hiyo.

Pia mkataba wake ukakatishwa ghafla kwa kile kilichodaiwa kudai kwake nyongeza ni kosa la kinidhamu, inaelezwa baada ya hayo yote Guttmann alisema: "Not in a hundred years from now will Benfica ever be European champions." Akimaanisha kuwa Benfica haitabeba tena kombe la Ulaya kwa miaka 100 kutoka hapo.

Kilichofuata kutokea hapo ni kwamba Benfica imefika katika fainali tano za kombe la UEFA na fainali tatu za Kombe la UROPA tangu mwaka huo 1962, na fainali zote imeambulia kipigo. Jumla Benfica imefungwa katika fainali 8 za Ulaya, sio kawaida.

Laana kama hii iliikumba timu ya taifa ya Autralia. Australia lilimtumia mchawi kutoka zimbabwe ili wafuzu kucheza kombe la Dunia kwa mara ya 1 mwaka 1974 huko Germany, walifanikiwa lakini mtaalamu hawakumlipa. Toka hapo hawakufuzu tena hadi mwaka 2005 waliporudi Afrika kumsaka mtaalamu wamlipe.

Baada ya hapo Australia ilifanikiwa kufuzu kwenye kombe la dunia tena huko Ujerumani mwaka 2006 baada ya kutofuzu kwa miaka 32 tangu mwaka huo 1974, na imeendelea kufunzu kwa miaka yote ya mashindano hayo kuanzia 2010, 2014 na 2018 na 2022.

Laana kama hii pia inatajwa kumuandama kocha wa Man City Pep Guadiola kwa kumfanyia madharau aliyekuwa mchezaji wake Yaya Toure raia wa Ivory Coast. Inaelezwa kuwa masikitiko ya Toure yalimlenga Pep kutoshinda UEFA akiwa na klabu yeyote.

Wakala wa Toure Dimitry Seluk alisema kuwa mizimu ya Afrika haiwezi kumruhusu Pep ashinde kikombe cha ulaya akiwa na klabu yoyote ya soka mpaka amuombe radhi Toure.



images%20(11).jpg
View attachment 2283362
 
Kwa maana hiyo Chelsea ndio mwenye faida zaidi na hizi laana za kwenye mpira. Kumbuka ile fainali ya EUROPA mwaka 2013 Chelsea dhidi ya Benfica. Chelsea akashinda 2-1 pia fainali ya UEFA mwaka 2021 Chelsea dhidi ya Man City. Chelsea anashinda 1-0

Katika fainali hizo zote ilipigwa mbungi sio ya kitoto mpaka kuna muda unaona kabisa Chelsea anaenda kupoteza lakini wapi. Hii kitaalamu sijui tuiitaje Chelsea anatembelea laana za timu pinzani au ni uwezo wake tu
 
Mtu yeyote mwenye laana au timu yeyote yenye laana nawashauri waje kwa Yesu wapokee ukombozi na wokovu juu ya laana zao. Yesu Kristo alibeba laana zetu msalabani. Hili hufanyika halisi pale watakapoamua kumwamini Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao. Mtu yeyote anaweza kuwekwa huru mbali na laana kwa njia ya kumwamini Yesu Kristo. Karibuni sana kwenye Ufalme.



YESU KRISTO NI BWANA NA MWOKOZI
 
Kwa maana hiyo Chelsea ndio mwenye faida zaidi na hizi laana za kwenye mpira. Kumbuka ile fainali ya EUROPA mwaka 2013 Chelsea dhidi ya Benfica. Chelsea akashinda 2-1 pia fainali ya UEFA mwaka 2021 Chelsea dhidi ya Man City. Chelsea anashinda 1-0

Katika fainali hizo zote ilipigwa mbungi sio ya kitoto mpaka kuna muda unaona kabisa Chelsea anaenda kupoteza lakini wapi. Hii kitaalamu sijui tuiitaje Chelsea anatembelea laana za timu pinzani au ni uwezo wake tu
Hahahaa Chelsea anaombea laana ziongezeke UEFA
 
Back
Top Bottom