Laana iliyowapta waliokuwa wajenzi wa mnara wa babeli ndio laana inayopta watawala sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Laana iliyowapta waliokuwa wajenzi wa mnara wa babeli ndio laana inayopta watawala sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Jul 15, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,015
  Likes Received: 37,744
  Trophy Points: 280
  Ukitafakari mwenendo wa mambo juu ya uendeshaji wa serikali bila shaka utajikuta na maswali mengi kuliko majibu na unaweza kushindwa kuelewa nini kinawasumbua hawa watawala.Yaani kila siku ya mungu wamekuwa ni watu wa kuumbuka kutokana na kauli na matendo yao na hata ya wasaidizi wao.
  Nachoweza kusema zama zao zimefika mwisho na hii ni kutokana na laana wanayoitumikia kutokana na matendo yao ya kidhalimu kwa watu wao.Mwenyezi mungu kawachoka na sasa kawashushia laana kama ilivyokuwa kwa wale watu waliokuwa wanajenga mnara wa babeli kama vitabu vitakatifu vinavytueleza.Kama ilivyokuwa kwa wajenga mnara wa babeli viongozi wa sasa ni kama hawana tena uelewano,yaani kila mtu anaongea na kufanya lake kama sio serikali moja na mwisho wa siku wanaishia kuumbuka tu.Hembu rejea mifano hii ya kauli na matendo ya viongozi walioko ktk serikali moja na uone kama wanatofauti na wale wajenzi wa mnara wa babeli ambao walishindwa kuelewana baada ya laana kuwashukia na jinsi kauli na matendo yao yanavyowaumbua hivi sasa:-
  1.Bungeni kesi iko mahakamani ila serikali inaendelea kuchukua hatua kwa jambo lile lile la mgomo
  2.Kauli ya liwalo na liwe na baadae taarifa zinakuja daktari kiongozi wa mgomo kashambuliwa vibaya
  3.Kauli ikulu hatuhusiki na yaliyomkuta daktari hata kabla tume yenyewe haijatoa majibu
  4.Kauli ya polisi juu ya anaedaiwa kumteka ulimboka kuhusishwa na kanisa na baadae kanisa kukanusha taarifa hizo
  5.Serikali haiwajui wamiliki wa Dowans na wakati huo inawapeleka mahakamani
  6.Katibu mkuu kiongozi na AG wanasema Jaa hiro hana makosa na hapo hapo ikulu inawageuka na kumsimamisha kazi
  7.Kauli za kugongana juu ya kupadisha posho ya wabunge ktk ya viongozi wa bunge na serikali ambao ndio walipaji
  8.Waziri mkuu kuairisha kutoa tamko juu ya mgomo wa madaktari bungeni kwasababu jambo liko mahakamani ila baadae bosi wake anahutubia taifa na kuongelea sawala lile lile.
  9.Kusimamishwa kazi mkurugenzi mkuu wa TANASECO na barua zilizivuja za siri kutoka kwa katibu mku.Hapa kuna dalili ya bifu na sii makosa ya mkurugenzi kama wanavyodai
  Mifano na mingi mno.kwa kifupi wanachama wa chama hiki tawala hawana tofauti na wale wajenzi wa mnara wa babeli kwani kutokana na laana wanayoitumikia bila kijijua hawaongei tena lugha moja na mwishwo wa utawala ndio umefika.
  Tusubiri tuone kwani hii ni laana tu inawatafuna kwa matendo yao na ndio maana wamepoteza dira na watasambaratika tu kama wale wajenzi wa mnara wa babeli.
   
Loading...