Laana!!! Baba mzazi anatembea na mamkwe wangu

dume la kenge

Senior Member
Apr 12, 2017
177
250
I hope mko ok humu. Mwenzenu akili yangu imevurugika baada ya masikio yangu kusikia kishichosikika. Kwa wakati huu niko kwenye jiji moja maarufu hapa tz. Mzee wangu yuko kwenye his early 40's na mamkwe pia yuko kwenye age hizo hizo. Sasa tuko na mzee wangu tangia mwezi wa nne, kuna maswala yake fulani anazifuatilia hapa town. Mamkwe wangu pia ana kama wiki tatu sasa, alikuja baada ya binti yake kuugua kidogo na kuwaona wajukuu zake. Kwangu tumeshajenga nyumba yenye vyumba vingi tu vya kutosha , kwa hiyo mzee wangu analala kwenye chumba chake, mamkwe pia pamoja na housegirl naye analala kivyake. Sasa juzi baada ya taifa stars kuniharibia siku, nkaenda zangu kulala huku hawa wazazi wetu pendwa wakiendelea kucheki muvi pamoja na mjakazi wetu. Sikubahatika kupata usingizi haraka ikanibidi nizame jf kidogo ili nipunguze stress kidogo. Sasa ilipofika mida ya saa sita hivi nkapata warning ya betery low na chaja mpaka sebuleni. Sasa kipindi naenda sebuleni kwenye korido ya chumba anacholala mamkwe nkasikia sauti ile ya mahaba kwa mbaali. Yaani walikuwa kwenye climax. Mama yangu!!!! Nilijiuliza maswali mengi huku nikiganda pale pale. Gafla nkasikia sauti ya mzee akikohoa kwa mbali. Daaaaaah!!! Niliishiwa nguvu ghafla hata chaja nkashindwa kwenda kuchukuwa nkarudi zangu chumbani. Mke wangu alikuwa na shift ya usiku kwa hiyo hakwepo kwa muda huo. Sijamwambia chochote ila hii swala inanitesa kweli kweli. Mzee wangu huwa ni mhuni namjua vizuri ila kwa nini afanye kitu kama hii ndani mwangu? Alafu kwa mamkwe???? Nimuitaje sasa mamkwe? mamdogo? Au mzee wangu ndo hivo tena amekuwa bamkwe? Jamani naombeni ushauri wenu akili yangu haufanyi kazi.
 

Shunie

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
121,697
2,000
pole sana ndio umkalishe mzee wako chini ajue umejua kila kitu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom