La viwanja linahitaji utanzania na si vyama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

La viwanja linahitaji utanzania na si vyama

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Anfaal, May 19, 2011.

 1. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi karibuni imeripotiwa kuwa Serikali imepima viwanja vipatavyo 20,000 huko Kinyerezi> Lengo kuu la uanzishwaji wa upimaji huu ni kuhakikisha kuwa Watanzania wanaacha ujenzi holela, wanakuwa na aseti zinazoweza kuwafanya wakopesheke lakini pia na serikali inapunguza gharama iingiazo za ubomoaji nyumba ambazo hazijengwi kwa mpangilio. Kwa hakika mpango huu ungekuwa bora kama malengo yake yangeweza kufikiwa. Lakini kwa bahati mbaya zaidi viwanja vile vinauzwa bei kubwa saaana. Kwa maana ya mita ya mraba ikiwa ni Tsh 10,000 na malipo yake hutakiwa kufanyika katika kipindi kifupi.
  yapo mwaswali kadhaa ambayo kuna haja ya kujiuliza;
  1. Wakina nani hasa walengwa wa viwanja vile?
  2. Serikali inaingia gharama kiasi gani wakati wa upimaji?
  3. Serikali inafanya biashara au inatoa huduma?
  4. Serikali hulipa pesa zinazofanana na hizo wakiwaamisha watu kutoka katika maeneo yanayofanana na hayo?
  5. Je, katika viwanja hivyo kuna huduma za msingi kama elimu, maji, barabara na afya?
  6. Ni upi mkakati wa kuhakikisha wale wafanyakazi wa serikali, mashirika binafsi, wajasiriamali na makundi mengine ya Watanzania wanaweza kununua viwanja vile?
  7. Wakati serikali ilikuwa inafahamika kwa kuuza viwanja kwa bei rahisi, lakini sasa hivi wanauza ghali kuliko watu binafsi na huku waking'anga'ana kuwapangia wafanyabiashara baadhi bei ya bidhaa. Je mchango wao kwenye suala la ardhi ni kuongeza mfumuko wa bei?
  Kuna haja ya sisi kama Watanzania kuungana kwa Utanzania wetu katika kuhakikisha hili linafanywa si mazoea. Serikali haitakiwi kukwepa majukumu yake. haiwezekani kwa idadi hii ya watu vinapimwa viwanja 20,000 kisha unapita msimu vinapimwa 20,000, je hiki si kiashirio cha kutengeneza demand kwa makusudi. Hivi tukisema haiwezekani, wao watatulazimisha? Nina hakika kwa Utanzania wetu hili haliwezekani ukizingatia hali halisi ya vipato vya Watanzania waliowengi.
  Watu wanachezea Utanzania wetu, wanawakamua Watanzania hata kwenye mahitaji yao ya msingi, kwa hili hata waiotaka kusema hapana na wao wajifunze kusema HAPANA.
  Nchi ni yetu sote na kila Mtanzania ana haki ya kuishi sehem bora na salama.
   
 2. Mutwale

  Mutwale Member

  #2
  May 19, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wengine maeneo yao yalichukuliwa na Serikali kwa ajili ya mradi huo na bado hawapewa fidia! lakini viwanja vinauzwa, je sasa huyo alokuwa na eneo si ndo amekosa kila kitu? na je akijalipwa hiyo fidia atapata wapi kiwanja? maana waliambiwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa, kwamba hataamishwa mtu yeyote, je inamaana wakazi wamaeneo hayo walikuwa wanapigwa sound?

  Wakati sasa umefika watanzania kuangalia mstakabali wetu na vizazi vijavyo! maana kwa bei hizo ni wazi Mfanyakazi(NYUNDO) na Mkulima(JEMBE) wakawaida hakuna atakayeweza kunua kiwanja hata mita za mraba 300 maana itakuwa ni shs 3,000,000! ni mfanyakazi yupi ataweza kulipa kiasi hicho ndani ya siku kumi na nne?

  Ufisadi Mtupu
   
 3. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hiyo ndiyo serikari ya ccm.
   
 4. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hapa ndio Watanzania tungeungana, serikali haituwezi. Kwanza wanapima viwanja vichache kisha bei kubwa! Wangeweza hata kupima viwanja laki 2 waone wanaojilimbikizia km watanunua vyote maana demand itakuwa hamna.
   
Loading...