La Ultima Letra - (Tahadhari: Picha zilizomo zinaogofya)

Habibu B. Anga

JF-Expert Member
May 7, 2013
6,557
25,671
Muhimu: Makala hii ndani yake ina maelezo na picha zenye kuogofya na ukatili. Soma kwa tahadhari binafsi. (reader’s discretion is strongly advised)

LA ULTIMA LETRA.


maxresdefault.jpg


C:\Users\Tanga\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image002.jpg



Sasa, unaweza kupata nakala za Kitabu changu cha "NYUMA YA ULIMWENGU WA SIRI NA UJASUSI".
kitabu kina kurasa 442 na ndani yake kuna makala 17.
Bei ya kitabu hiki ni Tsh 50,000/-

Pia waweza kupata kitabu changu cha "OPARESHENI ZA KIJASUSI ZILIZOFANIKIWA ZAIDI"
Kitabu hiki kina kurasa 214 na ndani yake nimechambua Oparesheni 6 tofauti.
Bei ya kitabu hiki ni Tsh 15,000/-

Wasiliana nami kwa namba 0759 181 457


Katika wiki ambayo Taifa zima la Mexico likiwa limeingia katika hofu kuu kutokana na wafungwa 130 ambao wanatambuliwa na serikali kama "watu hatari kupindukia" (extremely dangerous) wakiwa wametoroka kutoka kwenye gereza lenye ulinzi mkali la Matamoros katika mji wa Tamaulipas, ndipo papo hapo ambapo pia Mwendesha mashitaka wa serikali Bw.Ricardo Castillo anapokea simu kutoka kwa askari waliopo eneo la Nuevo Laredo wakimtaarifu juu ya tukio lingine la kuogofya ambalo kwa hakika lazima nalo litalitumbukiza zaidi nchi ya Mexico katika hofu kuu.

Polisi walimtaarifu Bw. Castillo kuwa asubuhi hiyo wananchi wamekuta miili ya watu 9 ambayo kati yao wanne wakiwa wanawake ikiwa imening'inizwa darajani pasipo uhai.

Kitu cha kuogofya zaidi miili hii ilining'inizwa bila vichwa kuwepo katika viwili wili vyake. Pia miili ilikuwa imetobolewa tumboni pamoja na kukatwa katwa mabegani kiasi cha mifupa kutokeza nje.
Pia miili ya maiti hizo za wanaume ilikuwa imenyofolewa sehemu za siri.

Castillo akawauliza polisi kama kulikuwa na kitu chochote eneo la tukio kinachowawezesha kung'amua watekelezaji wa tukio hilo na polisi wakamjibu kuwa kuna ujumbe wa maandishi yameandikwa kwa damu katika kuta za daraja.

Kabla polisi hawajamueleza Kikichoandikwa kwenye kuta za daraja, Castillo anapigiwa simu nyingine na kamanda wa polisi kutoka eneo la Monterrey kumuarifu kuwa usiku wa kuamkia siku ya leo katika klabu maarufu ya usiku ya mjini hapo imevamiwa na watu 52 wameuawa kikatili.

Kamanda huyo wa polisi akaendelea kumueleza zaidi kwamba mauaji hayo ni ya kutisha na kuogofya kwani miili yote hiyo 52 imekutwa ikiwa imefungwa kamba mikononi na yote haina vichwa.

Castillo akakumbwa na mshituko na kuishiwa nguvu na akamuuliza kamanda wa polisi kama kulikuwa na chochote zaidi eneo la tukio, na kamanda wa polisi akamjibu kuwa kulikuwa na maandishi ukutani ndani ya klabu yameandikwa na damu. Lakini pamoja na hilo miili yote ilikuwa imechorwa kwa kisu kifuani herufi 'Z'.
Castillo akapigwa na bumbuwazi zaidi akakata simu akimuahidi kamanda wa polisi kuwa anampigia baada ya dakika chache.

Baada tu kukata simu Castillo akapiga simu kwa afisa wa kwanza wa polisi aliyeko Nuevo Laredo ambaye alimpigia simu ya kwanza.

Baada ya afisa huyo wa polisi kupokea simu akamuuliza haraka kwamba ukiachikia mbali maandishi yaliyoandikwa kwa damu kwenye kuta za daraja je kulikuwa na kitu kingine chochote kwenye miili ya maiti hizo. Afisa wa polisi akamjibu "ndio maiti zote zimechorwa kwa kisu kifuani herufi 'Z'"

Castillo akashikwa na hofu kubwa na mshangao na akamjibu kwa kifupi tu afisa huyo wa polisi "Niko njiani nakuja, nadhani nimeshafahamu waliotekeleza tukio", afisa wa polisi akamuuliza "ni nani?" castillo akamjibu kwa ufupi.. "Los Zetas

C:\Users\Tanga\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image003.jpg




zzzz 1.jpg

Moja ya maeneo ya tukio ambapo wapinzani wa Gulf Cartel waliuwawa kwa ukatili wa kutisha na kukatwa katwa kila kiuongo mahali pake.



1999: Tamaulipas, Mexico

Bw. Cardenas Guillen, miezi michache baada ya kukabidhiwa uongozi wa genge la mihadarati la Gulf Cartel lengo la kwanza alilo jiwekea ilikuwa ni kutwaa tena upya maeneo yao ya kibiashara katika miji yote ambayo hapo zamani yakikuwa chini ya himaya yao lakini wakapokonywa na genge la Sinaloa Cartel.

Ili kufanikisha azma hii Cardenas aling'amua wazi kuwa inahitaji kikosi maalumu cha Ulinzi kwa ajili ya kulinda viongozi wa genge lake, kulinda 'biashara' yao pamoja kusambaratisha mawakala wote wa Sinaloa Cartel katika miji ambayo atailenga.

Ni hapo ambapo aliwasiliana na Ruben Salinas Luteni mstaafu wa kitengo maalumu cha Operation za weledi wa hali ya juu cha Jeshi la Mexico kilichoitwa GAFE (Grupo Aeromovil de Feurzas Especiales).

Baada ya kuwasiliana naye na kufanikiwa kufanya naye kikao maalumu akamueleza juu ya azma yake na kumuomba kumsaidia kutengeneza kutengo maalumu cha kijeshi ndani ya genge lake la Gulf Cartel, kwa ajili ya ulinzi na kusambaratisha wapinzani wake kibiashara.

Luteni Salinas akakubaliana na ombi la Boss Cardenas wa Gulf Cartel na akamuahidi kuunda kikosi cha kijeshi chenye weledi na ufanisi kuliko kikosi chochote cha uhalifu dunia ilichowahi kukiona.

Luteni Salinas akatumia uzoefu wake wa kijeshi kushawishi wanajeshi wengine 30 kutoka vitengo vya kijeshi vya weledi na oparesheni maalumu katika jeshi la Mexico, wakajiunga naye kuunda kikosi maalumu cha kijeshi kwa ajili ya ulinzi wa viongozi wa Gulf Cartel na kusambaratisha washindani wote wa Gulf Cartel.

Huo ndio ukawa mwanzo wa kikundi ambacho kilikuja kuwa tishio kwa ukanda mzima wa Amerika ya kusini, kutawala biashara nzima ya mihadarati nchini Mexico na kuingiza hofu isiyomithirika katika jamii Mexico kiasi kwamba hata muandishi wa habari au mtu mtaani aliogopa kutamka jina lao.

Wenyewe walijiita "Los Zetas"



zzzzz 3.jpg
C:\Users\Tanga\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image005.jpg

Masalia ya viungo vya Wanachama wa Sinaloa Cartel walio katwa katwa viande kama wanyama.



La Ultima Letra

Ndani ya miezi miwili luteni Salinas alikuwa amefanikiwa kuwasiliana na wanajesh 30 ambao walikubali kujiunga naye na kutengeneza kitengo cha kijeshi ndani ya genge la Gulf Cartel.
Wanajeshi hawa ambao luteni Salinas aliwachagua walikuwa ni wale pekee ambao walikuwa wamepatiwa mafunzo ya weledi wa hali ya juu katika jeshi la Mexico.

Kwa mfano, kulikuwa na wanajeshi ambao walikuwa wamepata mafunzo yao kutoka katika kikosi maalumu cha kijeshi cha nchi ya Israel (Israel Special Forces Units) na wengine mafunzo yao waliyapata kutoka katika vikosi maalumu vya jeshi la Marekani (American Special Forces).

Baada ya kukutana na kujadiliana kuhusu namna watakavyo endesha shughuli zao ndani ya genge la Gulf Cartel, moja ya washiriki aliyeitwa Arturo Decena akapendekeza kwa wenzake kwamba, kwa kuwa watakuwa wanaendesha shughuli zao katika mtindo wa kijeshi basi ni vyema hata kikosi chao wajiite jina la kijeshi na akapendekeza waitwe 'Los Zetas' (The Z's).

Ni kwamba, Katika mfumo wa mawimbi ya simu ya kijeshi (military radio airwaves) nchini mexico, kamanda mwenye ngazi ya juu kabisa kwenye eneo husika huwa anatambuliwa kama 'Z' katika mawasiliano ya simu za jeshi.
Ndio kusema kwa mfano kamanda wa ngazi ya juu kabisa ataitwa 'Z 1' anayemfuatia kwa cheo atakuwa 'Z 2' anayefuatia 'Z 3' vivyo hivyo na kuendelea.

Hii ndio ilikuwa maana halisi ya wao kujiita 'Los Zetas' (The Z's) wakimaanisha kuwa kikosi chao wanakifananisha na mkusanyiko wa wanajeshi makamanda wa ngazi za juu kabisa wenye weledi wa kutosha.
Pia wao wenyewe ndani kwa ndani walipenda kuitana jina la utani 'la ultima letra' (herufi ya mwisho).




Angelitos (Malaika Wadogo)

Baada ya kikosi cha Los Zetas kuwa kimezinduliwa rasmi baada ya kikao hicho, Arturo Decena ambaye alipewa jina la fumbo (code name) Z 1, alipewa wadhifa wa kuwa kamanda Mkuu wa Los Zetas.
Kisha kila mwanachama kati ya wanachama wote 31 akaamuriwa kutafuta vijana wasiopungua 8 wenye uzoefu au waliowahi kupitia jeshi au polisi.

Kila mmoja kati ya wanachama hao 31 akaleta vijana hao wasiopungua 8 hivyo wakapata vijana waliokaribia 300.
Gulf Cartel ikatengeneza kituo kijeshi maeneo ya mpakani na Guatamala kinachofanana kabisa na kituo cha kijeshi cha serikali. Kituo kilikuwa na kila kitu kinachohitajika kukidhi matakwa ya kuwa kituo cha kijeshi.
Kisha vijana hawa wapatao 300 wakapelekwa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo.

Kumbuka vijana hawa karibia wote walikuwa na uzoefu wa polisi au jeshi lakini katika kituo hiki walipatiwa mafunzo maalumu ili kuwapatia weledi ju kazi watayoenda kufanya kwa "mwajiri" wao mpya, Gulf Cartel.

Mafunzo hayo yalihusisha ushushu (intelligence gathering),utekaji (kidnaping), ulinzi maalumu, utesaji (torturing) na namna ya kudhibiti serikali za mitaa (local authorities).

Baada ya vijana kuwiva katika mafunzo waligawanywa tena kwa makamanda wakuu 31 ambao waliwatafuta na kuwaingiza Gulf Cartel. Kila kamanda alipatiwa vijana wasiopungua 8 na yeye kamanda pamoja na vijana wake wakapangiwa sehemu ndani ya mexico ambayo wataenda "kufanya kazi".

Makamanda hawa 31 waliwaita vijana wao waliopewa 'Angelitos' (little angels (malaika wadogo)).

Baada ya Makamanda na 'malaika' wao kugawanywa kwenye maeneo waliyopangiwa kwenye miji tofauti tofauti ndani ya mexico, kazi ikaanza.



zzzz 2.jpg
.
Mmoja wa Angelitos. Kijana mdogo mpiganaji chini ya makamanda wa Los Zetas.


Agizo kuu ambalo walikuwa wamepewa ilikuwa ni kusambaratisha mawakala wote wa Sinaloa Cartel ambayo ilikuwa chini ya El Chapo.
Makamanda wa Los Zetas walipoingia katika miji waliyopangiwa walifanya kazi kama Kikosi maalumu cha kijeshi cha wanamaji wa marekani (Navy SEALs) kutokana na mbinu walizotumia na ufanisi wa hali ya juu katika kutekeleza matukio yao.

Kwanza kabisa walikusanya taarifa za muhusika (wakala wa Sinoloa Cartel na wenzanke katika mji husika) kwa mbinu za 'kishushushu'. Walikusanya taarifa na kujua kila nukta ya maisha ya mtu wanayemlenga. Walijua mahali anapoishi, familia yake, sehemu anazopenda kutembelea, mahusiano ya kimapenzi na wanawake wengine zaidi ya mke wake kama ameoa, n.k.

Baada ya kujipatia taarifa za kutosha, Kamanda wa Los Zetas na 'malaika wake' walimteka muhusika na kutokomea nae mahali kusikojulikana. Wakiwa huko, wanamtesa muhusika kwa siku kadhaa ili atoe siri za viongozi wa Sinaloa Cartel pamoja na washirika wao.

Baada ya mateso ya siku kadhaa kinafuata kitendo cha kinyama ambacho ndicho hasa kinaifanya nchi nzima ya Mexico kuwaogopa Los Zetes na kuifanya nchi kuwa kama Jehanum duniani.

Muhusika aliyetekwa pamoja na wenzake wanaingizwa kwenye chumba maalumu wakiwa wamefungwa vitambaa vyeusi usoni. Wanaongozwa mpaka kwenye ukuta mmoja wapo wa chumba hicho ambapo kwente ukuta kunakuwa na kitambaa kikubwa cheupe kimening'ninizwa kwenye kuta kikiwa na maandishi ya kuisifu Los Zetas.
Baada ya hapo mtu huyu na wenzake waliotekwa wanapigishwa magoti mbele ya kitambaa hicho na Camera ya kurekodi video inawashwa.

Baada ya Camera kuwashwa Makamnda wa Los Zetas wakiwa wameficha sura zao kwa kuvaa 'kininja' wanatoa maelezo ya kuwaonya wanachama wengine wa Sinaloa Cartel kuwa kitakachotokea muda huo ndicho hicho hicho pia kitawakuta wanachama wengine wote wa Sinaloa Cartel kwenye kila pembe ya Mexico.

Kisha Makamanda na 'malaika' wao wanachukua sime na kuwakata vichwa mateka wao mmoja baada ya mwingine kama wanachinja Kuku na tukio hili linarekodiwa kwa ufasaha kwenye video na baadae video hiyo inawekwa kwenye mtandao kufikisha Ujumbe kwa ulimwengu mzima na Mara nyingi miili ya waliochinjwa ulitupwa katika barabara kuu au kuning'inizwa kwenye madaraja.

Matukio haya yaliyotekelezwa na Los Zetas yalileta taharuki ndani ya Mexico kwani matukio yalitekelezwa katika tarikbani miji 15 ya Mexico ambapo makamanda hawa na 'malaika' zao walitawanywa.

Ndani ta miezi michache taharuki ilikuwa kubwa kiasi kwamba washirika na mawakala wa magenge mengine ya mihadarati walidiriki kuyakana magenge yao na kujiung na Gulf Cartel kwa kuogopa kuchinjwa hadharani Los Zetas na kikundi cha ulinzi cha Gulf Cartel.

Pamoja na mamilioni ya madola waliyokuwa wanalipwa Los Zetas kutoka kwa Gulf Cartel, wakaamua watumie mbinu na uwezo wao wa kijeshi kujiongezea mamilioni zaidi.

Los Zetas wakaanzisha mfumo ulioitwa "Pisos".
Mfumo ambao ulikuja kuigwa na magenge mengine karibia yote hapo baadae.



SEHEMU YA PILI.

Los Zetas wakaanzisha mfumo ulioitwa "Pisos".
Mfumo ambao ulikuja kuigwa na magenge mengine hapo baadae.
Pisos ulikuwa ni mfumo ambao, Los Zetas katika maeneo yote ambayo walipangiwa kwenda kusambaratisha magenge mengine, hawakuishia hapo tu bali walihakikisha kuwa katika miji yote waliyokuwepo wafanyabiashara wengine wote wanaofanya biashara za haramu (hata kama sio madawa ya kulevya) wanalipa 'kipande' kwao ili waendelee na biashara zao za haramu.

Yaani kwa mfano wamiliki wa madanguro ya makahaba, au watu waliouza bidhaa 'feki' ikikuwa ni lazima wapeleke kipande kwa Los Zetas kila mwisho wa wiki ili waendelee na biashara katika eneo hilo.

Na kwa upande wa biashara ya madawa ya kulevya ni mawakala wa mabosi wao wa Gulf Cartel pekee ndio waliruhusiwa kufanya biashara hiyo kwenye eneo ambalo Los Zetas walikuwepo.


Nidhamu na Ufanisi wa Kijeshi

Ili kupanua zaidi ushawishi wao, Los Zetas wakaanzisha oparesheni maalumu ya kudhibiti eneo la mpaka kati ya Mexico na Guatemala.
Ieleweke kwamba Cocaine ya nchini Mexico kiasi kikubwa kinaingizwa kutoka nchi za Bolivia, Colombia na Peru. Na kutoka kwenye nchi hizo ili uingie nchini Mexico ni lazima upite nchini Guatemala.

Serikali ya nchi ya Guatemala ni Moja ya serikali dhaifu zaidi kutokana na rushwa na ukosefu wa rasilimali fedha za kutosha. Hii ni sababu nyingine kuifanya kama 'transit' ya kupitisha biashara haramu.

Kitendo cha Los Zetas kudhibiti mpaka wa Mexico na Guatemala hii ilimaanisha kuwa walikuwa na uwezo wa kudhibiti mizigo ya mabosi wao pekee ndiyo inayopita mpakani na hivyo kufanya magenge mengine yatetereke kibiashara kutokana na kukosa 'mizigo'.

Licha ya oparesheni za kikatili zilizokuwa zikifanywa na Los Zetas, lakini wanachama wa kikundi hiki walikuwa na nidhamu ya hali ya juu inayoakisi weledi wao wa kijeshi.
Los Zetas walikuwa hawajihusishi na vitendo vya wizi au ujambazi au kuua ama kuteka watu wasio na hatia.

Siku zote wenyewe wanajitanabaisha kuwa wnafanya matukio kwa watu maalumu ambao ni wapinzani wao kibiashara na kama hutaki kukutwa na madhira yao basi usijihusishe na biashara haramu.

Pia makamanda wa juu wa Los Zetas waliandaa nishani maalumu za kijeshi ambazo waliwatunuku wapiganaji wao ambao walitumikia Los Zetas kwa mafanikio makubwa.

Kutokana na ufanisi wa hali ya juu wa oparesheni za Los Zetas walifanikiwa kurudisha miji mingi kwenye himaya ya Gulf Cartel na kuonesha dalili kuwa Gulf Cartel wanaelekea kuwa vinara wa biashara ya mihadarati ndani ya America ya kusini wakiwapiku Sinaloa Cartel.

Katika miaka miwili ya mwanzo ya oparesheni za Los Zetas zilisaidia kurejesha zaidi ya miji 10 katika himaya ya kibiashara ya Gulf Cartel.




Ushindi wa Los Zetas katika Vita kuu II ya Magenge ya mihadarati.

Katika ulimwengu wa habari za kipelelezi hasa kuhusu magenge ya mihadarati, inaelezwa kwamba "vita kuu ya kwanza" ya magenge ya mihadarati ilitokea miaka ya 1980 kati ya Medellin Cartel na Cali Cartel.

"Vita kuu ya pili" ya magenge ya Mihadarati ilianza mwaka 2009 na ilikuwa kati ya Loz Zetas dhidi ya Gulf Cartel (mwajiri wa los zetas)

Walifikiaje katika vita hii???

Mwaka 2003 takribani miaka mitatu baada ya kuundwa kwa Los Zetas kikundi maalumu cha ulinzi ndani Gulf Cartel lilitokea tukio muhimu sana ambalo kilikuja kuwa na athari kubwa hapo baadae.

Maafisa wawili wa Kimarejani ambao mmoja aliitwa Dubois ambaye alikuwa ni afisa wa kitengo cha kudhibiti madawa ya kulevya cha Marekanj (DEA) na mwenzake aliitwa Fuentes ambaye alikuwa ni afisa wa shirika la upelelezi la marekani (FBI) wote wawili walikuwa ndani ya gari lenye namba za usajili za kidiplomasia lilikuwa linakatiza mitaa ya mji wa Tamaulipas ambao ndio makao makuu ya genge la Gulf Cartel.

Ndani ya gari hilo lenye vioo visivyoonyesha (tinted) kwenye siti ya nyuma walikuwa wamempakia mtoa taarifa wao (informant) ambaye walikuwa wanakatiza nae mitaa ya mji wa Tamaulipas akiwaekekeza namna ambavyo biashara ya madawa ya kulevya inavyofanyika na inavyopitishwa kwenda marekani.

Wakiwa wanaendelea kukatiza mitaa ghafla ikatokea gari nyingine ikaanza kuwafuatilia kwa nyuma. Wakataka kuongeza mwendo ili kuiepuka gari hiyo lakini ikatokea gari ya Polisi ikaziba njia mbele yao.
Kufumba na kufumbua zikatokea gari nyingine tatu na kuwazunguka kila upande.

Kisha watu wenye silaha nzito za moto wakashuka kwenye magari hayo na kuwaamuru maafisa hao washuke kwenye gari. Dakika chache baadae ilikuja gari ya kifahafi aina ya Jeep ambayo alishuka Boss wa Gulf Cartel Bwa. Cardenas.

Cardenas alikuwa ameshikilia bunduki aina ya AK47 ambayo kitako chake kilitengenezwa kwa dhahabu.
Kwa utulivu na kujiamini Cardenas akawaeleza kuwa hana shida na wao maafisa wa serikali bali ana shida na mtu waliyemficha kwenye siti ya nyuma ya gari (yule informant).

Maafisa wakakataa kuwa kuna mtu yuko siti ya nyuma! Cardenas akawaamuru wasogee pembeni alipekue gari ili ahakikishe kama kweli hakuna mtu siti ya nyuma. lakini maafisa wakakataa kwa kumueleza kuwa gari hiyo ni mali ya serikali ya marekani hivyo hawawezi kumruhusu raia wa kigeni kulipekua.

Cardenas akashikwa na hasira na kuwaambia kuwa anawapa nafasi ya mwisho wamsalimishe mtu waliye mficha siti ya nyuma lakini maafisa hao wakaendela kukaidi.

Cardenas akaamuru vijana wake wawamiminie risasi maafisa hao. Vijana wake wakawaua maafisa wa marekani papo hapo mchana kweupe tena mita chache kutoka makao makuu ya polisi wa mji wa Tamaulipas na hakuna askari aliyethubutu kuingilia.

Kisha wakamteka informant aliyekuwa ameficha siti ya nyuma na kuondoka naye. Mwili wake ulikuja kuokotwa siku mbili baadae akiwa amekatwa kichwa.

Kitendo hiki cha maafisa wa marekani kuuawa kinyama kiliamsha hasira za serikali ya marekani na wakaanzisha oparesheni maalumu ya kumsaka.

Hatimaye mwaka 2007 walifanikiwa kumkamata Cardenas na akashitakiwa na kuhukumiwa miaka 25 gerezani.
Lakini licha ya kuwa gerezani Cardenas aliendeleza biashara zake za madawa ya kulevya akiwatumia washirika wake wa Gulf Cartel na kuwaangamiza maadui zake kwa kutumia kikundi cha Los Zetas.

Mwaka 2009 kulikuwa na sherehe zijulikanazo kama 'Day of The Child' (siku ya mtoto) huko nchini Mexico.
Katika siku hiyo kwenye mji wa Tamaulipas kuliandaliwa sherehe kubwa ya kifahari ambapo watoto zaidi ya 2000 pamoja na wazazi wao walialikwa. Mwishoni mwa sherehe hiyo ikatangazwa kuwa sherehe hiyo imedhaminiwa na Cardenas.

Kitendo hiki kiliwaudhi sana serikali ya Marekani kwani ilikuwa kana kwamba Cardenas alikuwa anawadhihirishia kuwa licha ya kumfunga gerezani yeye bado alibakia "mfalme" nchini Mexico.
Hivyo basi Marekani ikawapasa watumie Sheria maalumu ya 'Kingpins Act' kuomba serikali ya Mexico kumuhamishia Cardenas kwenye magereza ya Marekani.

Mexico wakakubali na Cardenas akahamishiwa nchini Marekani.


zzzzzzz 1.jpg

Special Forces wa Mexico wakiwa na Cardenas Guillen, boss wa Gulf Cartel siku alipokuwa anahamishwa kutoka katika magereza ya Mexico na kupelekwa nchini Marejani.




Hii ilimaanisha kwamba uongozi wake ndani ya genge la Gulf Cartel ulikuwa umeishia hapo.
Hapa ndipo mtafaruku ulipoanzia kati ya 'muajiri' Gulf Cartel na 'muajiriwa' Los Zetas.

Baada ya Cardenas kuhamishiwa nchini marekani mwaka 2010 uongozi wa juu ndani ya Gulf Cartel ukapendekeza kuwa Mdogo wake Cardenas aliyeitwa Antonio arithi nafasi ya kaka yake kama kiongozi wa genge.

Suala hili halikukubaliwa na Los Zetas kwani wao walitaka kamanda wao mkuu Lazcano ndiye achukue mikoba ya Cardenas. Mabishano hayo yaliendelea kwa miezi kadhaa na kufanya uhusiano wao udorore kiasi.

Wakiwa katika kipindi hiki cha sintofahamu, Kuna siku ilitokea moja kiongozi wa 'kamati' za juu ndani ya Gulf Cartel aliyeitwa Flores Borrego walikuwa wanabishana na moja ya maluteni wa Los Zetas aliyeitwa Pena Mendoza. Baada ya mabishano makali, Borrego alishikwa na hasira na kutoa bastola akamtandika risasi Mendoza.

Taarifa hii ilipowafikia makamanda wa Los Zetas wakaamuru viongozi wa Gulf Cartel wamkabidhi muuaji wa Mendoza kwao ili walipe kisasi.
Viongozi wa Gulf Cartel wakakataa.

Siku hii ilikuwa ni mwezi September mwaka 2010 na ndiyo siku rasmi ambayo Los Zetas walijitenga na Gulf Cartel na kuanzisha genge lao linalojitegemea.



Vita kuu II

Mara tu baada ya kujitenga, kwakuwa Gulf Cartel walikuwa wanafahamu uwezo wa kijeshi wa Los Zetas ikabidi wajihami mapema ili wasije kumalizwa na Los Zetas.
Hivyo basi wakawasiliana na adui yao mkuu wa siku nyingi El Chapo kiongozi wa Sinaloa Cartel na kumuomba waunganishe nguvu kwadhibiti Los Zetas.

Sinaloa Cartel wakakubaliana na ombi la Gulf Cartel kwa sababu mbili kuu.
Moja, walikuwa na kinyongo na Los Zetas kwani toka kikundi hicho kimeanzishwa walikuwa wameua wanachama wao wengi.
Pili, walikubali kwasababu Gulf Cartel walikuwa tayari kukabidhi baadhi ya miji iliyoko chini ya himaya yao ya kibiashara wanaitoa iwe chini ya Sinaloa Cartel.

Suala hili lilikuwa ni jema machoni kwa El Chapo. Akakubali washirikiane kuwatokomeza Los Zetas.

Wakati wao wanapanga mipango hiyo, Los Zetas wakaweka makao yao makuu katika mji wa Nuevo Laredo mji uliopo mpakani kati ya Mexico na Marekani. Kisha wakaanzisha kampeni ya kusajili wanachama wapya na kuwapeleka katika kambi zao za mafunzo ya kijeshi.

Mwishoni mwa mwaka 2010 vita ikaanza rasmi ambapo Los Zetas walivamia mji wa Tamaulipas ambao ndio makao makuu ya Gulf Cartel mchana kweupe na kuendesha oparesheni ya kuwasaka wanachama wa Gulf Cartel nyumba kwa nyumba.

Ndani ya siku kadhaa mji wa Tamalipas ukageka uwanja wa vita risasi zikirushwa nje nje baina ya wanachama wa magenge hayo. Nyumba zilichomwa moto. Biashara ziliharibiwa. Mji wa Tamaulipas ukageka kama magofu yaliyoachwa miaka ya kale.


zzzzz 3.jpg

Mpiganaji wa LOs Zetas akiwa anamchinja mwanachama wa genge pinzani. Pembeni yake mkono wa kulia unaonekana mwili wa mtu ambaye amekwisha kuchinjwa tayari.




Ultima.

Vita hii Kali iliendelea kwa zaidi ya miaka miwili katika miji mbali mbali ndani ya Mexico na imegharimu maisha ya zaidi ya watu 35,000 na mpaka sasa vita hii bado inaendelea.

Mpaka sasa ni dhahiri kuwa Los Zetas ndio mshindi wa hii vita kwani kwasasa wao ndio wenye miji mingi chini ya himaya yao. Takwimu za ofisi za DEA ya nchini Marekani zinaonyesha kuwa Los zetas wana miji 26 ukilinganisha na miji 11 ya Gulf Cartel.

Los Zetas haikuishia hapo tu kwani wamevuka mipaka ya nchi, na kwasasa wao ndio wanaotawala biashara haramu ya mihadarati nchini Guatemala na pia wamefungua matawa nchini marekani katika jimbo la Texas ambapo wanashirikiana na genge la MS-13 pia wana tawi nchini Italia ambako wanashirikiana na genge la Ndraghetta.

Ushawishi wa genge la Los Zetas umekuwa mkubwa kiasi kwamba katika miji mingi nchini Mexico hauwezi kuwa kiongozi wa serikali (hasa nafasi ya Gavana) pasipo kuwa kibaraka wao.

Weledi wao wa kijeshi wa hali ya juu unawafanya waendelee kuitawala biashara ya mihadarati. Ukatili wao unawafanya waogopwe hata na watawala wa serikali.
Hata waandishi wa habari nchini Mexico abadani hawawezi kuripoti habari inayoweza kuwaudhi Los Zetas na waandishi wengi wameamua kuto wazungumzia kabisa, kwa heri au ubaya.

Wenyewe wanajitetea kuwa hawafanyi ukatili kwa mtu asiye na hatia bali kila anayekumbwa na madhira yao basi alijiingiza kwenye mambo ambayo hakupaswa kujiingiza.
Huko Mexico vijana wenye kupenda maisha ya anasa na fedha za haraka wanajiunga kila uchwao na kikundi hiki cha kikatili.

Hakika, ulimwengu umeshuhudia magenge mengi ya kiharifu. Lakini linapofikia suala la weledi, ufanisi, na ukatili, wao wanasimama katika viwango vyao tofauti kama heruzi Z ilivyojitenga mwishoni mwa alfabeti na hakika inaakisi jina lao.

Herufi ya mwisho. La ultima letra. Los Zetas. The Zs.


Jiunge na Group langu la WhatsApp kusoma simulizi mpya kila siku. Kuna malipo ya 5,000/- kwa mwezi. Wasiliana nami 0759 181 457


Mwisho.

The Bold.
 
Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici T-@mij TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava
 
Till death nitakuwa supporter pekee mwenye imani asilimia 100 na D. Trump. Anaposema atajenga ukuta kutenganisha US na Mexico anamaanisha. Kupitia mgongo wa wakimbizi, watukutu htr walioshindikana wanapenyezwa na serikali ya Mexico ili kuhakikisha vijana wa wamarekani wanaharibiwa na ngada.

Mexican cartels ndio wasambazaji hatari zaidi duniani wa Heroin, Cocain, mandrax, na kila aina ya sembe, na wanapenya boarders za US, kisha wanaanzisha street-rats na gangs, wanafanya wizi, ubakaji, utapeli, na kuuza unga wawaharibu kina Chris Brown na Lil Wayne.

D. Trump kawashtukia mapema sana, na sidhani kama kakurupuka from sleep. Hakuna chumba tena kwa Wamekiko kusambaza sembe USA ndani ya utawala wa huyu bwashee. Watafute kijiwe kingine tu, otherwise wataishia kunyonyolewa kama nguruwe.
 
daaah mexico na colombia ni nchi ambazo zimeteswa sana na magenge ya mihadarati, lakini pia rushwa ilichangia sana haya makundi kujitanua maana kuanzia viongozi wa serikali mpaka polise walikuwa corrupted. atleast now wameweza kuyadhibiti kidogo baada ya kupata mbinyo toka mataifa makubwa kama marekani..big up The bold
 
Sijui ni kwa nini biashara yenye kuhusisha pesa nyingi huwa na Watu katili namna hii,pesa ni mbaya sana ..
 
Middle east kuna ISIS,Ugaidi

Amerika haya drug dealer


Haya majitu usiombee kuingia anga zao kwenye kamusi zao ni MSAMAHA hakuna

Wanachinja mtu.vbaya kama kuku.asie faa.kuliwa

Ila nawakubali kinoma ma drig dealer ...
 
Hii naona ni zaidi ya Sierra Lione Na Congo kwenye madini hivi inadhihilisha madawa yana pesa chafu hadi vigogo serikalini wanageuzwa makostebo...
Nipo mkao wa kusubiri hasa huyu El chapo nilimsikia kiduchu mno.
 
Back
Top Bottom