DOKEZO Kyerwa, Kagera: Kinachofanywa na viongozi kitaleta mgogoro mkubwa mbeleni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kuna jipu kubwa ambalo likiiva litaleta hatari kubwa sana pale mkoa wa kagera wilaya ya kyerwa.

Kuna jamii ya wasukuma imeenda wilayani humo inawahonga viongozi ngazi ya vijiji na viongozi wanawapatia maeneo ya serikali waishi na kuwapa baadhi ya maeneo binafsi ya wenyeji kwa ajili ya kilimo cha mpunga.

Wenyeviti wanapewa pesa ndefu sana na kuahidiwa pesa nyingine baada ya mavuno. Mwananchi yeyote anayelalamika anatishiwa maisha hatari.

Viongozi wa Serikali na chama wote wanajua hili ila wanasubiri jipu lilipuke kutokee ugomvi wa wananchi wenyeji na wageni ndipo wachukue hatua.

Mwenye dhamana aingilie kati.
 
Hii ni hatari sana, pamoja na mifumo yote ya serikali hawajui kinachoendelea? Mh Mbunge nae? Mambo ya ardhi ni sensitive sana na Taifa hili moja ya sababu za umoja ni umakini kwenye mambo hayo pamoja na udhaifu uliopo.
 
Sasa kama ardhi haitumiwi vzr, si Bora wapewe wanaoweza kuindeleza? Cha msingi ilasimishwe tu,
 
Back
Top Bottom