Kigwangalla: Uelewe Mgogoro na Maasai, siyo uvamizi wa Wakenya

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Na Dkt. Hamisi Kigwangalla.

Kimsingi kiini cha mgogoro huu ni mabadiliko ya falsafa na hatimaye Sheria za uhifadhi. Ni mabadiliko ya ufahamu na umuhimu wa uhifadhi kadri muda unavyopita. Ni mabadiliko ya demografia, maendeleo ya watu kiuchumi na kijamii.

Wala siyo uvamizi wa wakenya kwenye ardhi ya Tanzania ama ujio wa kampuni ya wawekezaji wa kiarabu wala wa kizungu pekee.

Wapiga propaganda za upande wa wananchi wa Ngorongoro wanatafuta sababu za uongo kuituhumu serikali wakati wapiga propaganda wa serikali wanatafuta sababu za uongo kuwatuhumu wananchi na ku-justify hatua wanazotaka kuchukua. Propaganda zote hizi hazitotusaidia kupata suluhu ya kudumu na ya uhakika.

Mgogoro unaanzia pale ambapo serikali za kikoloni ziliona umuhimu wa kuhifadhi maliasili ya wanyamapori. Ikatungwa Sheria ya uhifadhi wanyamapori ya Mwaka 1940, na baadaye Sheria ya hifadhi za Taifa ya Mwaka 1948 (ambayo ilianzisha Serengeti National Park). Sheria ya hifadhi za Taifa ililazimisha wakazi wa asili wa Serengeti wakiwemo waikoma, wamasai, wasukuma na wengine walazimishwe kuhama.

Wamasai walihamishiwa Ngorongoro, Loliondo na Sale. Wasukuma walisukumwa Maswa, Bariadi na Bunda na Waikoma walisukumwa Butiama, Musoma na Bunda. Kipindi hicho idadi ya watu ilikuwa ndogo sana na maeneo yalikuwa makubwa mno.

Ikaja ikatungwa Sheria mpya ya uhifadhi wanyamapori ya Mwaka 1959, na ikaonekana itungwe Sheria ya kuhifadhi kreta ya Ngorongoro, Kreta za Olmoti na Empakai na eneo la nje ya hapo (jumla kilometa za mraba 8292 - Tarafa ya Ngorongoro ya sasa). Enzi hizi idadi ya watu ilikuwa 8000 tu. Note that leo hii idadi ya watu ni zaidi ya 92,000.

Pori tengefu la Loliondo lilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya Wanyamapori ya Mwaka 1959. Lilianzishwa kwenye ardhi ya vijiji, ambavyo kimsingi vilikuwepo toka Mwaka 1923, kutokana na kifungu namba 9 cha Sheria hiyo.

Sheria ya uhifadhi wa Wanyamapori ya Mwaka 1959 iliyoanzisha mapori tengefu (game controlled areas - GCAs) iliacha umiliki wa ardhi kwenye vijiji, iliruhusu matumizi ya ardhi ya maeneo hayo kwa shughuli za kibinadamu ikiwemo Kilimo, ufugaji, uvuvi na maendeleo ya watu, ililenga tu kuwalinda na kuwahifadhi wanyamapori waliopo kwenye maeneo haya. Pia ililenga kuwaachia wananchi fursa ya kutumia raslimali hii kiasili (kwa yale makabila yanayotumia nyamapori, mizizi, matunda na asali kama chakula). Sema sheria ililenga tu kuweka utaratibu maalum wa namna ya kutumia maliasili hiyo.

Baada ya Uhuru kulitungwa Sheria mpya ya uhifadhi wa wanyamapori (sheria namba 12 ya 1974). Hata hivyo, sheria hii ilirithi msingi wake kwenye Sheria za kikoloni zilizotangulia, ambapo kwenye mapori tengefu ardhi ilibaki kuwa kwenye milki ya vijiji (kwa hati kabisa) na serikali ilisimamia tu raslimali ya wanyamapori waliopo kwenye maeneo haya.

Kadri idadi ya watu ilivyoongezeka, mila na desturi zilivyobadilika, shughuli za kibinadamu zilivyoongezeka, sayansi ya mazingira na uhifadhi ilivyokua, illionekana hatari kubwa kutokea mbele ya safari, kwa ikolojia kuharibika na species za mimea na wanyama kupotea.

Hapa sasa ikatungwa sheria ya uhifadhi wa wanyamapori Namba 5 ya Mwaka 2009. Sheria hii ikitambua wazi kuwa mapori tengefu zaidi ya 80% yameanzishwa kwenye ardhi ya vijiji, kwenye kifungu cha 16(4) na 16(5) iliweka masharti ya, kwanza kuzuia matumizi ya shughuli za kibinadamu kwenye mapori tengefu, na kwa minajili hiyo Waziri mwenye dhamana alielekezwa kufanya tathmini ya mapori tengefu yote nchini (ndani ya miezi 12) na kuyatangaza upya, ilimradi tu asitangaze pori tengefu kwenye ‘ardhi ya vijiji’!

Kimsingi ardhi ya Tarafa ya Loliondo na Tarafa ya Sale ni ardhi ya vijiji. Kisheria hakuna shaka yoyote juu ya hili.

Hata hivyo, kwa maslahi ya umma kitaifa na kimataifa, kutokana na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu ardhi hii haiwezi kuachwa bila usimamizi endelevu. Why? Sababu kubwa ni hizi: moja, Safu za milima iliyopo eneo hili ni chanzo kikuu cha maji yanayoingia hifadhi ya Taifa ya Serengeti; mbili, mzunguko wa nyumbu na wanyama wahamao hupitia eneo hili wanapotoka Masai Mara - Kenya.

(NB: Ikolojia ya Serengeti-Mara haikamiliki bila Loliondo. Kwenye eneo hili nyumbu zaidi ya 600,000 huzaliwa kila mwaka! Maana kwa upande wa Magharibi ya Loliondo kuna Serengeti National Park, kwa Kaskazini kuna hifadhi ya Masai-Mara ya Kenya na kwa Kusini yake Kuna Ngorongoro Conservation Area, na kwa Mashariki yake Kuna Pori Tengefu la Ziwa Natron!)

Kwa kuwa kadri tunavyozidi kuhifadhi maeneo na kuzuia baadhi ya matumizi tunapunguza malisho ya mifugo (rangelands) na kubadilisha mila na desturi za watu wetu. Mfano, Tarafa ya Loliondo na Sale zina wakazi ambao ni wafugaji (nomadic pastoralists) kwa takriban 80%, ambao walizoea kuhama hama (kama ambavyo wanyamapori wanavyohama hama) na kujenga maboma ya muda mfupi kulingana na majira ya mvua na majira ya ukame. Imagine; kwa zaidi ya miaka 200 walifanya hivyo kwenye eneo lote la iliyojulikana kama Maasai land (sehemu kubwa ya Serengeti, Wilaya yote ya Ngorongoro, Wilaya yote ya Longido, Wilaya yote ya Simanjiro na Wilaya yote ya Monduli. Kwa kiasi kikubwa eneo hili ni kame mno, bila kuhama hama wafugaji hawawezi kutosha katika eneo dogo tulilowaachia.

Hivi ukiwaminya kwenye eneo dogo zaidi (baada ya kutangaza baadhi ya maeneo kuwa hifadhi za Taifa) na ukachanganya na ongezeko la idadi ya watu na mifugo unategemea wataishije?

Ni sawa na kusema, ni lazima tutafakari kwanza ‘livelihood’ yao kabla ya kuchukua uamuzi wowote ule wa kubadilisha matumizi ya eneo hili, hata kama tuna mamlaka ya kufanya hivyo. Na hili ndiyo jukumu kubwa na la msingi la serikali ya watu.

Tunatokaje hapa tulipo? Moja, ni kuanzisha Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori (WMA) kwenye eneo la Loliondo GCA. Ama, mbili, kuanzisha namna maalum ya kulisimamia kwa pamoja eneo hili huku maslahi ya makundi mbalimbali ya wadau yakizingatiwa. Ama ukifikiria Kwa kelele zaidi, suluhisho ni kuwahamisha wakazi wote wa eneo hili…hivi wako wangapi? Wanapelekwa wapi? Na gharama yake ni kubwa kiasi gani?

Wengi ndani ya serikali wanaamini ikianzishwa WMA itatatua mgogoro kwa kiasi fulani lakini uhifadhi (ambao ndiyo azma kuu ya serikali na dunia nzima ili kuhakikisha Serengeti haifi, yaani “Serengeti shall never die”, na the only existing ‘natural migration of wildlife’ inalindwa, hautokuwa salama chini ya mfumo wa WMA!)

Tunaamini kwamba, serikali ni lazima iwe na mkono wake kwenye uhifadhi, ulinzi na matumizi ya eneo hili. Tunaona tuwashirikishe wananchi kwenye uamuzi huu na kimsingi hawana shida sana na hili. Na ndiyo Uamuzi tulioweka kwenye maandishi. Nadhani uamuzi huu utaleta suluhu yenye tija.

Ili uamuzi huu utekelezeke ni lazima eneo ambalo ni muhimu zaidi kiikolojia litambulike, ambalo kutokana na tafiti mbalimbali linafikia kilometa za mraba 1500, kati ya kilometa za mraba 4000, liwekewe alama zinazoonekana; iundwe mamlaka yenye uwakilishi wa wadau wote, na mamlaka hii iwekwe chini ya ulezi wa Mamlaka ya Uhifadhi wa Eneo la Ngorongoro (NCAA), hii mamlaka itajulikana kama Loliondo Special Conservation Area Authority, itakuwa na Baraza lake la utawala na litakuwa linasimamiwa na Bodi ya NCAA.

Cha kusikitisha ni kwamba, wapiga propaganda za kuzuia kazi ya serikali kwenye eneo hili wamekuwa, toka Mwaka 1992 wakidai kuwa waarabu wameuziwa eneo hili na serikali (ukitaka kumuua paka anza kwanza kwa kumpa jina baya!) Yote hii ni kutafuta namna ya kupata utetezi wa wazungu. Hata hivyo, eneo hili limekuwa na mashamba makubwa ya wawekezaji wa kizungu toka miaka ya 1980, na mengi yamegeuzwa kuwa lodge za kitalii, kama vile AndBeyond, Buffalo Luxury Tented Camp, Thomson’s Safaris na nyingine.

Pengine mgogoro huu umepewa chachu na uwepo wa hawa wawekezaji wengine ambao wanaendesha utalii wa picha na wanalipa moja Kwa moja kwenye serikali ya kijiji walipojenga na hawa wasingependa wanyama wawindwe kwa sababu wanakuwa na stress na hivyo kukwamisha utalii wa picha. Uwindaji wa kitalii haupeleki pesa kwenye serikali za vijiji, bali 75% ya mapato inaenda serikali kuu wakati 25% inaenda Halmashauri.

Wapiga propaganda za wenyeji hawamtaki mwarabu kwa kuwa hawalipi wao moja Kwa moja, analipa huko juu tu, tofauti na hao wengine wa picha. Na hata kama anawajengea miradi mizuri ya maendeleo wao bado wangetaka awe chini yao tu kwa sababu wangependa zaidi wapokee pesa kuliko miradi ya ujirani mwema (CSR) anayowapa!

Matumizi yote haya yamepunguza eneo la malisho zaidi na zaidi kwa wafugaji. Hivyo, eneo pekee wanalolitegemea ni hilo la kilometa za mraba 1500. Ukiwazuia kwenda huko 100% maana yake hakuna maisha tena hapo. Kama hautaki kuwahamisha Loliondo basi ni lazima uweke utaratibu wa wafugaji kuingia kulisha kwenye eneo hili walau kwa kipindi cha miezi minne ya majira ya ukame kila mwaka.

Mbinu za kiethnografia zinataka tusiiweke kando jamii kwenye maamuzi na hatua tunazochukua hususan kwenye mambo yanayohusu maisha yao ya kila siku. Bado naamini suluhu pekee ya mgogoro huu ipo kwenye ushirikishwaji wa wadau wote wa Loliondo na mazungumzo ya mezani.

Hakuna utalii na uwekezaji kama tunatajwa kimataifa kuwa miongoni mwa maeneo yenye fujo.

Tuwaite mezani viongozi wa kimila na kisiasa wa kimasai tukae nao, twende nao pamoja, tusiwatenge. Tusiwaone ni adui wa uhifadhi. La hasha.

Pia soma:
Waziri Kigwangalla aagiza kampuni ya Uwindaji ya OBC ya Loliondo kurudi walikotokea kabla ya Januari 2018
 
Wamasai sio Jamii ya kwanza kuhamishwa. Watu Kila siku wanahamishwa kwa sababu mbali mbali from ujenzi wa miundombinu, maeneo ya jeshi, hifadhi nk

Hawa mayeroo watahama tu kwa hiyari au shurti kama wanajiona wao ni special sana watakipata wanachokitafuta.
 
Umenikumbusha Uhamisho wa 1972 pale Iringa
 
Naona Kigwangala amejaribu kuwa neutral kwa kupeleka lawama kwa wapiga propaganda wa pande zote mbili ili kwa makusudi ailinde serikali kama ilivyo kawaida yake.

Binafsi naamini kwenye huu mgogoro wa Loliondo, kama kweli Kigwangala anakiri serikali inapiga propaganda hapo ndipo alipotakiwa atueleze kwanini serikali inaficha ukweli na kuwaonea aibu wananchi wake?

Tusidanganyane kwenye hili, huu mgogoro huibuka pale tu waswahili wa Pwani wanaposhika madaraka, hapo ndipo hizi kelele hujirudia, hivyo Kigwangala anapojaribu kudai sio serikali, au hao OBC wanaohusika kwenye huu mgogoro ANATUDANGANYA.

Hao waarabu wa kutoka Oman lazima wahusike, kama ameshakiri ndio huwahonga watendaji wa vijiji huko Loliondo, basi kwanini nisiamini OBC [mjomba] pia wameshawahonga watendaji wa serikali kuu ndio maana wako upande wao? hapa ndipo penye kiini cha tatizo.

Samia kimya, Kinana kimya, all eyes can see their ill motive on this.
 
Nimesoma mpaka mwisho lakini nimeshindwa kujua mleta mada amelenga kusimamia upande upi maana haueleweki kabisa. Je yupo kutetea upande wa wamasai au serikali?
Mleta mada kujifanya hauna upande (neutral) katila jambo lililo wazi kama hili ni unafiki wa 100%. Huenda hii ni mwendelezo wa mbinu za propaganda za watawala au ni kiki za Kigwangwala kutafuta ushujaa wa nitoke vipi.
 
Kigwangala alifaulu vipi na kuwa Daktari, anasema wanaopinga watafuta huruma ya Wazungu wakati huo huo anayetunza na kutoa hela kutunza Hifadhi zote Tanzania ni Mzungu sasa kwa nini huyo Mzungu awe na huruma na watu wanaotetea wavamizi wa hifadhi kama ni kweli Wamasai ni wavamizi na it’s about kulinda Hifadhi?

Very low IQ dude, bila ya Mzungu hakuna hata hifadhi moja Tanzania, Serengeti yenyewe yote inaendeshwa na Ujerumani bila ya Frankfurt zoo hakuna Serengeti sasa iweje Mzungu anayetoa fedha kutunza Hifadhi awe upande wa Wamasai ambao mnasema ni Waharibifu wa Hifadhi ?

Logic iko wapi ?
 
Kigwangalla: Otterlo Business Corporation (OBC) wanahonga Watendaji wa Wizara ya Utalii. Leo katoa elimu na ufafanuzi kuhusu mgogoro wa Loliondo.
View attachment 2271956
====

UUELEWE MGOGORO WA LOLIONDO.

Na Dkt. Hamisi Kigwangalla.

Kimsingi kiini cha mgogoro huu ni mabadiliko ya falsafa na hatimaye Sheria za uhifadhi. Ni mabadiliko ya ufahamu na umuhimu wa uhifadhi kadri muda unavyopita. Ni mabadiliko ya demografia, maendeleo ya watu kiuchumi na kijamii.

Wala siyo uvamizi wa wakenya kwenye ardhi ya Tanzania ama ujio wa kampuni ya wawekezaji wa kiarabu wala wa kizungu pekee.

Wapiga propaganda za upande wa wananchi wa Ngorongoro wanatafuta sababu za uongo kuituhumu serikali wakati wapiga propaganda wa serikali wanatafuta sababu za uongo kuwatuhumu wananchi na ku-justify hatua wanazotaka kuchukua. Propaganda zote hizi hazitotusaidia kupata suluhu ya kudumu na ya uhakika.

Mgogoro unaanzia pale ambapo serikali za kikoloni ziliona umuhimu wa kuhifadhi maliasili ya wanyamapori. Ikatungwa Sheria ya uhifadhi wanyamapori ya Mwaka 1940, na baadaye Sheria ya hifadhi za Taifa ya Mwaka 1948 (ambayo ilianzisha Serengeti National Park). Sheria ya hifadhi za Taifa ililazimisha wakazi wa asili wa Serengeti wakiwemo waikoma, wamasai, wasukuma na wengine walazimishwe kuhama.

Wamasai walihamishiwa Ngorongoro, Loliondo na Sale. Wasukuma walisukumwa Maswa, Bariadi na Bunda na Waikoma walisukumwa Butiama, Musoma na Bunda. Kipindi hicho idadi ya watu ilikuwa ndogo sana na maeneo yalikuwa makubwa mno.

Ikaja ikatungwa Sheria mpya ya uhifadhi wanyamapori ya Mwaka 1959, na ikaonekana itungwe Sheria ya kuhifadhi kreta ya Ngorongoro, Kreta za Olmoti na Empakai na eneo la nje ya hapo (jumla kilometa za mraba 8292 - Tarafa ya Ngorongoro ya sasa). Enzi hizi idadi ya watu ilikuwa 8000 tu. Note that leo hii idadi ya watu ni zaidi ya 92,000.

Pori tengefu la Loliondo lilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya Wanyamapori ya Mwaka 1959. Lilianzishwa kwenye ardhi ya vijiji, ambavyo kimsingi vilikuwepo toka Mwaka 1923, kutokana na kifungu namba 9 cha Sheria hiyo.

Sheria ya uhifadhi wa Wanyamapori ya Mwaka 1959 iliyoanzisha mapori tengefu (game controlled areas - GCAs) iliacha umiliki wa ardhi kwenye vijiji, iliruhusu matumizi ya ardhi ya maeneo hayo kwa shughuli za kibinadamu ikiwemo Kilimo, ufugaji, uvuvi na maendeleo ya watu, ililenga tu kuwalinda na kuwahifadhi wanyamapori waliopo kwenye maeneo haya. Pia ililenga kuwaachia wananchi fursa ya kutumia raslimali hii kiasili (kwa yale makabila yanayotumia nyamapori, mizizi, matunda na asali kama chakula). Sema sheria ililenga tu kuweka utaratibu maalum wa namna ya kutumia maliasili hiyo.

Baada ya Uhuru kulitungwa Sheria mpya ya uhifadhi wa wanyamapori (sheria namba 12 ya 1974). Hata hivyo, sheria hii ilirithi msingi wake kwenye Sheria za kikoloni zilizotangulia, ambapo kwenye mapori tengefu ardhi ilibaki kuwa kwenye milki ya vijiji (kwa hati kabisa) na serikali ilisimamia tu raslimali ya wanyamapori waliopo kwenye maeneo haya.

Kadri idadi ya watu ilivyoongezeka, mila na desturi zilivyobadilika, shughuli za kibinadamu zilivyoongezeka, sayansi ya mazingira na uhifadhi ilivyokua, illionekana hatari kubwa kutokea mbele ya safari, kwa ikolojia kuharibika na species za mimea na wanyama kupotea.

Hapa sasa ikatungwa sheria ya uhifadhi wa wanyamapori Namba 5 ya Mwaka 2009. Sheria hii ikitambua wazi kuwa mapori tengefu zaidi ya 80% yameanzishwa kwenye ardhi ya vijiji, kwenye kifungu cha 16(4) na 16(5) iliweka masharti ya, kwanza kuzuia matumizi ya shughuli za kibinadamu kwenye mapori tengefu, na kwa minajili hiyo Waziri mwenye dhamana alielekezwa kufanya tathmini ya mapori tengefu yote nchini (ndani ya miezi 12) na kuyatangaza upya, ilimradi tu asitangaze pori tengefu kwenye ‘ardhi ya vijiji’!

Kimsingi ardhi ya Tarafa ya Loliondo na Tarafa ya Sale ni ardhi ya vijiji. Kisheria hakuna shaka yoyote juu ya hili.

Hata hivyo, kwa maslahi ya umma kitaifa na kimataifa, kutokana na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu ardhi hii haiwezi kuachwa bila usimamizi endelevu. Why? Sababu kubwa ni hizi: moja, Safu za milima iliyopo eneo hili ni chanzo kikuu cha maji yanayoingia hifadhi ya Taifa ya Serengeti; mbili, mzunguko wa nyumbu na wanyama wahamao hupitia eneo hili wanapotoka Masai Mara - Kenya.

(NB: Ikolojia ya Serengeti-Mara haikamiliki bila Loliondo. Kwenye eneo hili nyumbu zaidi ya 600,000 huzaliwa kila mwaka! Maana kwa upande wa Magharibi ya Loliondo kuna Serengeti National Park, kwa Kaskazini kuna hifadhi ya Masai-Mara ya Kenya na kwa Kusini yake Kuna Ngorongoro Conservation Area, na kwa Mashariki yake Kuna Pori Tengefu la Ziwa Natron!)

Kwa kuwa kadri tunavyozidi kuhifadhi maeneo na kuzuia baadhi ya matumizi tunapunguza malisho ya mifugo (rangelands) na kubadilisha mila na desturi za watu wetu. Mfano, Tarafa ya Loliondo na Sale zina wakazi ambao ni wafugaji (nomadic pastoralists) kwa takriban 80%, ambao walizoea kuhama hama (kama ambavyo wanyamapori wanavyohama hama) na kujenga maboma ya muda mfupi kulingana na majira ya mvua na majira ya ukame. Imagine; kwa zaidi ya miaka 200 walifanya hivyo kwenye eneo lote la iliyojulikana kama Maasai land (sehemu kubwa ya Serengeti, Wilaya yote ya Ngorongoro, Wilaya yote ya Longido, Wilaya yote ya Simanjiro na Wilaya yote ya Monduli. Kwa kiasi kikubwa eneo hili ni kame mno, bila kuhama hama wafugaji hawawezi kutosha katika eneo dogo tulilowaachia.

Hivi ukiwaminya kwenye eneo dogo zaidi (baada ya kutangaza baadhi ya maeneo kuwa hifadhi za Taifa) na ukachanganya na ongezeko la idadi ya watu na mifugo unategemea wataishije?

Ni sawa na kusema, ni lazima tutafakari kwanza ‘livelihood’ yao kabla ya kuchukua uamuzi wowote ule wa kubadilisha matumizi ya eneo hili, hata kama tuna mamlaka ya kufanya hivyo. Na hili ndiyo jukumu kubwa na la msingi la serikali ya watu.

Tunatokaje hapa tulipo? Moja, ni kuanzisha Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori (WMA) kwenye eneo la Loliondo GCA. Ama, mbili, kuanzisha namna maalum ya kulisimamia kwa pamoja eneo hili huku maslahi ya makundi mbalimbali ya wadau yakizingatiwa. Ama ukifikiria Kwa kelele zaidi, suluhisho ni kuwahamisha wakazi wote wa eneo hili…hivi wako wangapi? Wanapelekwa wapi? Na gharama yake ni kubwa kiasi gani?

Wengi ndani ya serikali wanaamini ikianzishwa WMA itatatua mgogoro kwa kiasi fulani lakini uhifadhi (ambao ndiyo azma kuu ya serikali na dunia nzima ili kuhakikisha Serengeti haifi, yaani “Serengeti shall never die”, na the only existing ‘natural migration of wildlife’ inalindwa, hautokuwa salama chini ya mfumo wa WMA!)

Tunaamini kwamba, serikali ni lazima iwe na mkono wake kwenye uhifadhi, ulinzi na matumizi ya eneo hili. Tunaona tuwashirikishe wananchi kwenye uamuzi huu na kimsingi hawana shida sana na hili. Na ndiyo Uamuzi tulioweka kwenye maandishi. Nadhani uamuzi huu utaleta suluhu yenye tija.

Ili uamuzi huu utekelezeke ni lazima eneo ambalo ni muhimu zaidi kiikolojia litambulike, ambalo kutokana na tafiti mbalimbali linafikia kilometa za mraba 1500, kati ya kilometa za mraba 4000, liwekewe alama zinazoonekana; iundwe mamlaka yenye uwakilishi wa wadau wote, na mamlaka hii iwekwe chini ya ulezi wa Mamlaka ya Uhifadhi wa Eneo la Ngorongoro (NCAA), hii mamlaka itajulikana kama Loliondo Special Conservation Area Authority, itakuwa na Baraza lake la utawala na litakuwa linasimamiwa na Bodi ya NCAA.

Cha kusikitisha ni kwamba, wapiga propaganda za kuzuia kazi ya serikali kwenye eneo hili wamekuwa, toka Mwaka 1992 wakidai kuwa waarabu wameuziwa eneo hili na serikali (ukitaka kumuua paka anza kwanza kwa kumpa jina baya!) Yote hii ni kutafuta namna ya kupata utetezi wa wazungu. Hata hivyo, eneo hili limekuwa na mashamba makubwa ya wawekezaji wa kizungu toka miaka ya 1980, na mengi yamegeuzwa kuwa lodge za kitalii, kama vile AndBeyond, Buffalo Luxury Tented Camp, Thomson’s Safaris na nyingine.

Pengine mgogoro huu umepewa chachu na uwepo wa hawa wawekezaji wengine ambao wanaendesha utalii wa picha na wanalipa moja Kwa moja kwenye serikali ya kijiji walipojenga na hawa wasingependa wanyama wawindwe kwa sababu wanakuwa na stress na hivyo kukwamisha utalii wa picha. Uwindaji wa kitalii haupeleki pesa kwenye serikali za vijiji, bali 75% ya mapato inaenda serikali kuu wakati 25% inaenda Halmashauri.

Wapiga propaganda za wenyeji hawamtaki mwarabu kwa kuwa hawalipi wao moja Kwa moja, analipa huko juu tu, tofauti na hao wengine wa picha. Na hata kama anawajengea miradi mizuri ya maendeleo wao bado wangetaka awe chini yao tu kwa sababu wangependa zaidi wapokee pesa kuliko miradi ya ujirani mwema (CSR) anayowapa!

Matumizi yote haya yamepunguza eneo la malisho zaidi na zaidi kwa wafugaji. Hivyo, eneo pekee wanalolitegemea ni hilo la kilometa za mraba 1500. Ukiwazuia kwenda huko 100% maana yake hakuna maisha tena hapo. Kama hautaki kuwahamisha Loliondo basi ni lazima uweke utaratibu wa wafugaji kuingia kulisha kwenye eneo hili walau kwa kipindi cha miezi minne ya majira ya ukame kila mwaka.

Mbinu za kiethnografia zinataka tusiiweke kando jamii kwenye maamuzi na hatua tunazochukua hususan kwenye mambo yanayohusu maisha yao ya kila siku. Bado naamini suluhu pekee ya mgogoro huu ipo kwenye ushirikishwaji wa wadau wote wa Loliondo na mazungumzo ya mezani.

Hakuna utalii na uwekezaji kama tunatajwa kimataifa kuwa miongoni mwa maeneo yenye fujo.

Tuwaite mezani viongozi wa kimila na kisiasa wa kimasai tukae nao, twende nao pamoja, tusiwatenge. Tusiwaone ni adui wa uhifadhi. La hasha.
Asante kwa elimu Dr Kigwa.
Ila ya Qnet yalikuwaje tena?! 🤔🤔🤔
 
Nimesoma mpaka mwisho lakini nimeshindwa kujua mleta mada amelenga kusimamia upande upi maana haueleweki kabisa. Je yupo kutetea upande wa wamasai au serikali?
Mleta mada kujifanya hauna upande (neutral) katila jambo lililo wazi kama hili ni unafiki wa 100%. Huenda hii ni mwendelezo wa mbinu za propaganda za watawala au ni kiki za Kigwangwala kutafuta ushujaa wa nitoke vipi.
Mimi sina upande bali wewe unaweza kuwa na upande. Asante
 
Kuhama itabidi wahame wala wengi wetu hawaoni tatizo la hilo...

Kinacholeta ukakasi na maswali ni wanahama ili kupisha nini ?

Je tunaondoa wachafuzi ili kuleta wachafuzi ?
 
Hili jambo sio la kukurupukia.

Busara inapaswa kutumika.

Hakuna namna mgeni anapewa kipaumbele kwa mwenyeji.

Sijui viongozi wa sasa wanafikiri nini ila kumuonea mtu ambaye hawezi kujitetea ni hatari mno.

Leo mnawaonea wamasai kwakua mna mamlaka lakini nawaambieni mtalipa machozi yao ipo siku mtalipa.
 
Kigwangalla: Otterlo Business Corporation (OBC) wanahonga Watendaji wa Wizara ya Utalii. Leo katoa elimu na ufafanuzi kuhusu mgogoro wa Loliondo.
View attachment 2271956
====

UUELEWE MGOGORO WA LOLIONDO.

Na Dkt. Hamisi Kigwangalla.

Kimsingi kiini cha mgogoro huu ni mabadiliko ya falsafa na hatimaye Sheria za uhifadhi. Ni mabadiliko ya ufahamu na umuhimu wa uhifadhi kadri muda unavyopita. Ni mabadiliko ya demografia, maendeleo ya watu kiuchumi na kijamii.

Wala siyo uvamizi wa wakenya kwenye ardhi ya Tanzania ama ujio wa kampuni ya wawekezaji wa kiarabu wala wa kizungu pekee.

Wapiga propaganda za upande wa wananchi wa Ngorongoro wanatafuta sababu za uongo kuituhumu serikali wakati wapiga propaganda wa serikali wanatafuta sababu za uongo kuwatuhumu wananchi na ku-justify hatua wanazotaka kuchukua. Propaganda zote hizi hazitotusaidia kupata suluhu ya kudumu na ya uhakika.

Mgogoro unaanzia pale ambapo serikali za kikoloni ziliona umuhimu wa kuhifadhi maliasili ya wanyamapori. Ikatungwa Sheria ya uhifadhi wanyamapori ya Mwaka 1940, na baadaye Sheria ya hifadhi za Taifa ya Mwaka 1948 (ambayo ilianzisha Serengeti National Park). Sheria ya hifadhi za Taifa ililazimisha wakazi wa asili wa Serengeti wakiwemo waikoma, wamasai, wasukuma na wengine walazimishwe kuhama.

Wamasai walihamishiwa Ngorongoro, Loliondo na Sale. Wasukuma walisukumwa Maswa, Bariadi na Bunda na Waikoma walisukumwa Butiama, Musoma na Bunda. Kipindi hicho idadi ya watu ilikuwa ndogo sana na maeneo yalikuwa makubwa mno.

Ikaja ikatungwa Sheria mpya ya uhifadhi wanyamapori ya Mwaka 1959, na ikaonekana itungwe Sheria ya kuhifadhi kreta ya Ngorongoro, Kreta za Olmoti na Empakai na eneo la nje ya hapo (jumla kilometa za mraba 8292 - Tarafa ya Ngorongoro ya sasa). Enzi hizi idadi ya watu ilikuwa 8000 tu. Note that leo hii idadi ya watu ni zaidi ya 92,000.

Pori tengefu la Loliondo lilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya Wanyamapori ya Mwaka 1959. Lilianzishwa kwenye ardhi ya vijiji, ambavyo kimsingi vilikuwepo toka Mwaka 1923, kutokana na kifungu namba 9 cha Sheria hiyo.

Sheria ya uhifadhi wa Wanyamapori ya Mwaka 1959 iliyoanzisha mapori tengefu (game controlled areas - GCAs) iliacha umiliki wa ardhi kwenye vijiji, iliruhusu matumizi ya ardhi ya maeneo hayo kwa shughuli za kibinadamu ikiwemo Kilimo, ufugaji, uvuvi na maendeleo ya watu, ililenga tu kuwalinda na kuwahifadhi wanyamapori waliopo kwenye maeneo haya. Pia ililenga kuwaachia wananchi fursa ya kutumia raslimali hii kiasili (kwa yale makabila yanayotumia nyamapori, mizizi, matunda na asali kama chakula). Sema sheria ililenga tu kuweka utaratibu maalum wa namna ya kutumia maliasili hiyo.

Baada ya Uhuru kulitungwa Sheria mpya ya uhifadhi wa wanyamapori (sheria namba 12 ya 1974). Hata hivyo, sheria hii ilirithi msingi wake kwenye Sheria za kikoloni zilizotangulia, ambapo kwenye mapori tengefu ardhi ilibaki kuwa kwenye milki ya vijiji (kwa hati kabisa) na serikali ilisimamia tu raslimali ya wanyamapori waliopo kwenye maeneo haya.

Kadri idadi ya watu ilivyoongezeka, mila na desturi zilivyobadilika, shughuli za kibinadamu zilivyoongezeka, sayansi ya mazingira na uhifadhi ilivyokua, illionekana hatari kubwa kutokea mbele ya safari, kwa ikolojia kuharibika na species za mimea na wanyama kupotea.

Hapa sasa ikatungwa sheria ya uhifadhi wa wanyamapori Namba 5 ya Mwaka 2009. Sheria hii ikitambua wazi kuwa mapori tengefu zaidi ya 80% yameanzishwa kwenye ardhi ya vijiji, kwenye kifungu cha 16(4) na 16(5) iliweka masharti ya, kwanza kuzuia matumizi ya shughuli za kibinadamu kwenye mapori tengefu, na kwa minajili hiyo Waziri mwenye dhamana alielekezwa kufanya tathmini ya mapori tengefu yote nchini (ndani ya miezi 12) na kuyatangaza upya, ilimradi tu asitangaze pori tengefu kwenye ‘ardhi ya vijiji’!

Kimsingi ardhi ya Tarafa ya Loliondo na Tarafa ya Sale ni ardhi ya vijiji. Kisheria hakuna shaka yoyote juu ya hili.

Hata hivyo, kwa maslahi ya umma kitaifa na kimataifa, kutokana na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu ardhi hii haiwezi kuachwa bila usimamizi endelevu. Why? Sababu kubwa ni hizi: moja, Safu za milima iliyopo eneo hili ni chanzo kikuu cha maji yanayoingia hifadhi ya Taifa ya Serengeti; mbili, mzunguko wa nyumbu na wanyama wahamao hupitia eneo hili wanapotoka Masai Mara - Kenya.

(NB: Ikolojia ya Serengeti-Mara haikamiliki bila Loliondo. Kwenye eneo hili nyumbu zaidi ya 600,000 huzaliwa kila mwaka! Maana kwa upande wa Magharibi ya Loliondo kuna Serengeti National Park, kwa Kaskazini kuna hifadhi ya Masai-Mara ya Kenya na kwa Kusini yake Kuna Ngorongoro Conservation Area, na kwa Mashariki yake Kuna Pori Tengefu la Ziwa Natron!)

Kwa kuwa kadri tunavyozidi kuhifadhi maeneo na kuzuia baadhi ya matumizi tunapunguza malisho ya mifugo (rangelands) na kubadilisha mila na desturi za watu wetu. Mfano, Tarafa ya Loliondo na Sale zina wakazi ambao ni wafugaji (nomadic pastoralists) kwa takriban 80%, ambao walizoea kuhama hama (kama ambavyo wanyamapori wanavyohama hama) na kujenga maboma ya muda mfupi kulingana na majira ya mvua na majira ya ukame. Imagine; kwa zaidi ya miaka 200 walifanya hivyo kwenye eneo lote la iliyojulikana kama Maasai land (sehemu kubwa ya Serengeti, Wilaya yote ya Ngorongoro, Wilaya yote ya Longido, Wilaya yote ya Simanjiro na Wilaya yote ya Monduli. Kwa kiasi kikubwa eneo hili ni kame mno, bila kuhama hama wafugaji hawawezi kutosha katika eneo dogo tulilowaachia.

Hivi ukiwaminya kwenye eneo dogo zaidi (baada ya kutangaza baadhi ya maeneo kuwa hifadhi za Taifa) na ukachanganya na ongezeko la idadi ya watu na mifugo unategemea wataishije?

Ni sawa na kusema, ni lazima tutafakari kwanza ‘livelihood’ yao kabla ya kuchukua uamuzi wowote ule wa kubadilisha matumizi ya eneo hili, hata kama tuna mamlaka ya kufanya hivyo. Na hili ndiyo jukumu kubwa na la msingi la serikali ya watu.

Tunatokaje hapa tulipo? Moja, ni kuanzisha Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori (WMA) kwenye eneo la Loliondo GCA. Ama, mbili, kuanzisha namna maalum ya kulisimamia kwa pamoja eneo hili huku maslahi ya makundi mbalimbali ya wadau yakizingatiwa. Ama ukifikiria Kwa kelele zaidi, suluhisho ni kuwahamisha wakazi wote wa eneo hili…hivi wako wangapi? Wanapelekwa wapi? Na gharama yake ni kubwa kiasi gani?

Wengi ndani ya serikali wanaamini ikianzishwa WMA itatatua mgogoro kwa kiasi fulani lakini uhifadhi (ambao ndiyo azma kuu ya serikali na dunia nzima ili kuhakikisha Serengeti haifi, yaani “Serengeti shall never die”, na the only existing ‘natural migration of wildlife’ inalindwa, hautokuwa salama chini ya mfumo wa WMA!)

Tunaamini kwamba, serikali ni lazima iwe na mkono wake kwenye uhifadhi, ulinzi na matumizi ya eneo hili. Tunaona tuwashirikishe wananchi kwenye uamuzi huu na kimsingi hawana shida sana na hili. Na ndiyo Uamuzi tulioweka kwenye maandishi. Nadhani uamuzi huu utaleta suluhu yenye tija.

Ili uamuzi huu utekelezeke ni lazima eneo ambalo ni muhimu zaidi kiikolojia litambulike, ambalo kutokana na tafiti mbalimbali linafikia kilometa za mraba 1500, kati ya kilometa za mraba 4000, liwekewe alama zinazoonekana; iundwe mamlaka yenye uwakilishi wa wadau wote, na mamlaka hii iwekwe chini ya ulezi wa Mamlaka ya Uhifadhi wa Eneo la Ngorongoro (NCAA), hii mamlaka itajulikana kama Loliondo Special Conservation Area Authority, itakuwa na Baraza lake la utawala na litakuwa linasimamiwa na Bodi ya NCAA.

Cha kusikitisha ni kwamba, wapiga propaganda za kuzuia kazi ya serikali kwenye eneo hili wamekuwa, toka Mwaka 1992 wakidai kuwa waarabu wameuziwa eneo hili na serikali (ukitaka kumuua paka anza kwanza kwa kumpa jina baya!) Yote hii ni kutafuta namna ya kupata utetezi wa wazungu. Hata hivyo, eneo hili limekuwa na mashamba makubwa ya wawekezaji wa kizungu toka miaka ya 1980, na mengi yamegeuzwa kuwa lodge za kitalii, kama vile AndBeyond, Buffalo Luxury Tented Camp, Thomson’s Safaris na nyingine.

Pengine mgogoro huu umepewa chachu na uwepo wa hawa wawekezaji wengine ambao wanaendesha utalii wa picha na wanalipa moja Kwa moja kwenye serikali ya kijiji walipojenga na hawa wasingependa wanyama wawindwe kwa sababu wanakuwa na stress na hivyo kukwamisha utalii wa picha. Uwindaji wa kitalii haupeleki pesa kwenye serikali za vijiji, bali 75% ya mapato inaenda serikali kuu wakati 25% inaenda Halmashauri.

Wapiga propaganda za wenyeji hawamtaki mwarabu kwa kuwa hawalipi wao moja Kwa moja, analipa huko juu tu, tofauti na hao wengine wa picha. Na hata kama anawajengea miradi mizuri ya maendeleo wao bado wangetaka awe chini yao tu kwa sababu wangependa zaidi wapokee pesa kuliko miradi ya ujirani mwema (CSR) anayowapa!

Matumizi yote haya yamepunguza eneo la malisho zaidi na zaidi kwa wafugaji. Hivyo, eneo pekee wanalolitegemea ni hilo la kilometa za mraba 1500. Ukiwazuia kwenda huko 100% maana yake hakuna maisha tena hapo. Kama hautaki kuwahamisha Loliondo basi ni lazima uweke utaratibu wa wafugaji kuingia kulisha kwenye eneo hili walau kwa kipindi cha miezi minne ya majira ya ukame kila mwaka.

Mbinu za kiethnografia zinataka tusiiweke kando jamii kwenye maamuzi na hatua tunazochukua hususan kwenye mambo yanayohusu maisha yao ya kila siku. Bado naamini suluhu pekee ya mgogoro huu ipo kwenye ushirikishwaji wa wadau wote wa Loliondo na mazungumzo ya mezani.

Hakuna utalii na uwekezaji kama tunatajwa kimataifa kuwa miongoni mwa maeneo yenye fujo.

Tuwaite mezani viongozi wa kimila na kisiasa wa kimasai tukae nao, twende nao pamoja, tusiwatenge. Tusiwaone ni adui wa uhifadhi. La hasha.
Hongera Dr kigwangala kwa hili darasa PhD imefanya kazi .mm binafsi nimekuelewa.elimu elimu elimu elimu elimu.
 
Atoe lecturer kama hiyo kuhusu Qnet labda na sisi tutakuwa good morning billionaire.
 
Wamasai waliopo Mtwara, Lindi na Zanzibar walifikaje? Nani kasema mmasai hawezi ishi nje ya Loliondo?

Huu ni upuuzi kuendekeza cheap popularity na hapo ndo Kenya anafaidika akiona kumbe mitanzania yenyewe haijielewi

Loliondo lazima ilindwe kwa mslahi ya utalii ambacho ni moja ya vyanzo vikuu vya mapato ya Taifa
 
Ukimsoma Prof Shivji utaona utaratibu mzima umekiukwa! Hizi hoja zingine ambazo Kingwa amezungumza kwa urefu ni sehemu ya tatizo tu. Nchi hii ni yetu sote, watu wajadiliane muafaka upatikane badala ya ubabe.
 
Back
Top Bottom