Kyela: Wananchi waililia Bandari ya Itungi

Kyela: Wananchi waililia Bandari ya Itungi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
141,582
Reaction score
284,132
Wananchi Wilayani Kyela wamesikitishwa na kusononeka baada ya kuambiwa kwamba Bandari yao waliyoitunza na kuipenda kwa miaka yote , nayo imechukuliwa na Waarabu wa DP WORLD

Huku wakibubujikwa na Machozi , wananchi waliopakana na Bandari hiyo kutoka vijiji vya Bujesi , Njisi , Ngonga na Kajunjumele wameonekana kukata tamaa kuhusu uwekezaji huo , hasa wakizingatia kwamba ni hivi karibuni Serikali ilitumia hela nyingi kujenga meli mbili za kisasa zilizotengenezwa na Kampuni ya Songoro Marine ya Ilemela Mwanza , Taarifa zaidi zinasema kwamba wananchi hao kwa umoja wao wanatafakari hatua za kuchukua ama Wamuachie Mungu aamue.

Taarifa za Bandari za ziwa Nyasa kubinafsishwa kwa Waarabu zimefichuliwa na Mwenyekiti wa Chadema , Freeman Mbowe alipoongea na Waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya Chama chake jana na kwamba Bandari za Mbambay , Manda na Itungi nazo zimekwenda na maji kwa muda usiojulikana .

Mungu Ibariki Kyela .
 
We jamaa kwenye issue ya bandari nakuungaga mkono sana tatizo wewe ni keybord worries sana kyela yenyewe unaitetea kwenye kishikwambi chako tuu
Badala uje ukiamshe huku unapambana kwenye simu tuu. Shauri yako watauza na masyeto huku msalimie Mwanyamaki
 
Niko kajunjumele kwa wiki 3 sasa , naendeleza CHADEMA DIGITAL
 
Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaruhusu rais kuongoza mihula miwili (2) mfululizo ya urais kwa maana ya miaka 10.. ila ikiwapendeza wabunge wetu wanaweza wakafanya namna kurekebisha hicho kifungu ili kukidhi mahitaji yetu kwa sasa.. Mama Samia aongoze hadi 2040.
 
Aliyekuloga naye kalogwa
 
Kuanzia hapo Kyela mjini
Hapo Kyecu nyumba kibao za tope

Nenda Ipinda, Ipande kote huko tope tupi
Pale Ipande kuna maendeleo sana kwa sasa , kuanzia Pale Mpiki Kimbwala hadi Njugilo ni nyumba za kisasa tupu !

wewe ulienda huko miaka mingi .
 
Pale Ipande kuna maendeleo sana kwa sasa , kuanzia Pale Mpiki Kimbwala hadi Njugilo ni nyumba za kisasa tupu !

wewe ulienda huko miaka mingi .
Ujue mi nitembea pote huko hakuna kitu ndo kwanza wanachonga barabara.
Kyela ndo makao makuu ya wilaya ila pa hovyo sana
 
Back
Top Bottom