Juzi, jana na hadi hivi sasa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa kutumia M-Pesa imekufa "kwishney' kabisa hapa jijini Dar es salaam, na nadhani nchini kote. Kila wakala wa huduma hiyo niliyemtembelea maelezo yake yalikuwa yaleyale- HAKUNA MTANDAO. Na ukiuliza sababu ya kuwepo kwa tatizo hilo wanasema hawajui na wala hawajaarifiwa kulikoni. Pamoja na usumbufu huo wanaopata wateja cha ajabu ni kuwa hata Voda wenyewe ama kwa kiburi, ukiritimba, ama dharau za maksudi, hawajatoa maelezo yoyote kwa wateja kuhusu tatizo hilo, kiasi cha baadhi ya wateja niliowakuta wakisotea huduma hiyo katika vituo vya mawakala, kuingiwa na hofu kuwa waje wakaingizwa mjini kama ile habari ya DECI. Mmoja alikwenda mbali kwa kusema kuwa kama watu waliaminika katika jamii ndio waliotuingiza mkenge katika mambo mengi ya uchumi, Voda watashindwaje kutu-deci. Voda toeni ufafanuzi kuhusu kadhia hii!:A S cry: