Kwikwi za huduma ya m-pesa; kulikoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwikwi za huduma ya m-pesa; kulikoni?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by KAPONGO, Jun 14, 2011.

 1. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,374
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  Juzi, jana na hadi hivi sasa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa kutumia M-Pesa imekufa "kwishney' kabisa hapa jijini Dar es salaam, na nadhani nchini kote. Kila wakala wa huduma hiyo niliyemtembelea maelezo yake yalikuwa yaleyale- HAKUNA MTANDAO. Na ukiuliza sababu ya kuwepo kwa tatizo hilo wanasema hawajui na wala hawajaarifiwa kulikoni. Pamoja na usumbufu huo wanaopata wateja cha ajabu ni kuwa hata Voda wenyewe ama kwa kiburi, ukiritimba, ama dharau za maksudi, hawajatoa maelezo yoyote kwa wateja kuhusu tatizo hilo, kiasi cha baadhi ya wateja niliowakuta wakisotea huduma hiyo katika vituo vya mawakala, kuingiwa na hofu kuwa waje wakaingizwa mjini kama ile habari ya DECI. Mmoja alikwenda mbali kwa kusema kuwa kama watu waliaminika katika jamii ndio waliotuingiza mkenge katika mambo mengi ya uchumi, Voda watashindwaje kutu-deci. Voda toeni ufafanuzi kuhusu kadhia hii!:A S cry:
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Hizi transactions za via mobile nafikiri wamiliki hawajajipanga vizuri. Ukiacha network kusumbua unaweza ukaenda kwa wakala akakwambia hana hela subiria hadi watu watakapoenda kudeposit.
   
 3. F

  FUSO JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  mimi nimelizwa pesa zangu hadi leo sijazipata, zimetolewa na mtu kaenda bila kitambulisho lakini cha ajabu wakala kampa as simple as that. nafika naambiwa zimeshachukuliwa, kwenye simu bado hata sijapata sms kusema zimetolewa -- watch out this system, hasa unapotuma M-PESA kwenda TIGO pesa hapo kuibiwa ni rahisi sana then wanasingiziana, mara nenda TIGO, mara Nenda M -PESA.
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  SEACOM ipo down - Nairobi ipo down - MPESA ipo down - Hakuna System!
   
 5. charger

  charger JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 2,327
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Yani imeshakuwa tatizo,minafikiri hawa jamaa wanapenda pesa tu kabla ya kujipanga,inaonekana kama vile system imezidiwa.Au ndio DECI nyingine maana huko kuna hela kibao za wateja pengine kuliko hata DECI.
   
 6. m

  mwananchi2007 Member

  #6
  Jun 14, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mmiliki wa server za M_pesa yupo kenya, sasa voda fone wanunuzi wa leseni ya M-pesa hawawezi kuwa na jibu la moja kwa moja wakati kuikwa na tatizo la m-pesa. ili jua kuwa pesa zako zipo salama.
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  nashukuru kwa kunijuza, ngoja nipunguzve jazba

  hata mwili wa binadamu wakati mwingine hupata hitilafu na kusababisha homa
   
 8. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kama nilivyobandika hapo juu - SEACOM Link to Nairobi (from Mombasa) is currently down na ndiyo maana M-PESA service haipatikani kwa sasa.. Nina ofisi jijini Nairobi ambazo hadi sasa tuna-run kwenye secondary link (VSAT) kutokana na tatizo hilo la SEACOM .. so far no ETA!
   
 9. F

  FUSO JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  Tumieni mabenki kutuma pesa zenu hasa zikiwa zaidi ya laki tano, hizi systems za fasta fasta zina majuto yake, mawakala wenyewe elimu darasa la saba utata mtupu hata elimu ya mwanzo ya utunzaji pesa hawana. wakala kama muuza duka.
   
 10. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Bora hata muuza duka,wakala hawa kama wauza kalanga

  mbali ya hili mie nimelizwa pesa mara2,ya kwanza 30 nilimtumia mama (wa kunizaa),akanambia hata meseji hakuipata na wakati M-pesa wanasema imetumwa,paka leo nilipoteza

  mara ya pili kituo tofauti nikatuma 10elfu nikaituma kwingine,hakupata meseji lakini salio linasoma,alivyoongea na voda akaambiwa mimi nirudi kwa wakala a-resend kwa maana wakati inatumwa mtandao ulifeli,kufika kwa wakala akawa mbogo,akawa mkali,akakataa katakata ku-resend,nikamuuliza kwani hajawahi kupata hasara kwa nini anakataa kuresend?akasusa,basi nikaamua kuipotezea nikaondoka

  ila frankly speaking,M-PESA ina matatizo sana pamoja na mawakala wao,wanajua kuandika tu,hawawezi kuhandle wala kusolve out contingencies,binafsi sina imani tena na mambo yao
   
 11. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mkuu, nami wiki 4 zilizopita nilipoteza hivyo hivyo, nilimtumia dogo kijijini lakini bahati mbaya siku hiyo hiyo akapoteza simu na jamaa aliyechukua simu kaenda kutoa pesa bila kitambulisho.
   
 12. F

  FUSO JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  mimi wamenilamba laki 700,000 sitaki hata kusikia kitu kinaitwa MPESA in my life - kuna vijana wanjanja wanjanja wanachezea network - nimefuatilia makao makuu hapa mlimani city wananizingua na kunipotezea muda wangu. sababu hata message kwamba pesa imetolewa sijawahi ipata, na jamaa kaenda kwa wakala kalamba pesa zote eti bila kitambulisho - inaingia akililini kweli?
   
 13. F

  FUSO JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  system inaweza kuwa genuine ila watu wenyewe ndyo matatizo matupu kuanzia wanaoangalia network pamoja na mawakala wao - na mbaya zaidi ukituma MPESA kwenda TIGO PESA basi hapo andika ni maumivu.
   
 14. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Sure Mkuu!
  Mi ni mmoja wa waathirika sana wa hii shida!...
  Nilitumia MPESA jana kwa minajili ya kununua umeme, na hadi leo sijarudishiwa hata delivery msg. Na hata nikiuliza salio hakuna majibu....sIELEWI KAMA SALIO LANGU LIMEPUNGUZWA AU LIPO.
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Jana niliwaachia laki mbili ilikuwa mida ya saa sita wamefanikiwa kunitumia leo asbi ebu imagine.
  Alafu sio mara moja mara nyingi tuu mmpesa ni issue kama yamewashinda si mbwage manyanga
   
 16. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #16
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  Pole sana, hiyo ni hela nyingi. Mi nakushauri uende TCRA, kuna fomu za malalamiko kwenye website yao (TCRA|Tanzania Communications Regulatory Authority). Jaza hiyo fomu peleka TCRA na nakala wapelekee wao-M-Pesa.Hata kama hutapewa pesa zako, ni lazima uonyeshe unatambua haki yako. Hii itawasaidia hata ndugu na rafiki zako wa karibu wasipatwe na madhila kama yako. Hiyo pesa ni nyingi na kosa ni lao (wamekiuka utaratibu kwa kutoa pesa bila kibali), don't go down without a fight!
   
Loading...