ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 643
- 1,603
Katibu Mkuu Kiongozi wa Baraza Kivuli la Mawaziri wa ACT Wazalendo, Ndugu Idrisa Kweweta, leo Mei 18, 2025, amechukua rasmi fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Kilwa Kusini kupitia tiketi ya chama hicho, katika hafla ya kisiasa iliyojaa matumaini na hamasa ya mabadiliko.
Fomu hiyo alikabidhiwa na Katibu wa Jimbo, Ndugu Twahir Bingwe, mbele ya wanachama, viongozi wa chama, na wananchi waliokusanyika kwa wingi katika ofisi za Jimbo Kilwa Kusini.
Kweweta, ambaye pia ni Mtafiti Mwandamizi Chama hicho, alieleza kwa msisitizo kuwa dhamira yake ni kulinda kura ya kila Mwanakilwa, kupigania demokrasia ya kweli, na kuondoa mifumo kandamizi iliyojengwa na utawala wa muda mrefu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Tunaingia kwenye pambano la kweli la kidemokrasia. Niko tayari kupambana na CCM na dola kuhakikisha kila kura ya Mwanakilwa inathaminiwa. Lengo langu ni kurejesha heshima ya Kilwa—heshima ya maendeleo, heshima ya sauti ya wananchi, na heshima ya utawala wa haki,” alisema Kweweta.
Mbali na dhamira yake ya kisiasa, Kweweta aligusia changamoto kubwa zinazoikumba Kilwa Kusini — ikiwemo ubovu wa miundombinu ya barabara, huduma duni za afya, na mfumo dhaifu wa elimu. Alisema hali hiyo ni matokeo ya moja kwa moja ya uongozi usiojali wa CCM.
Katika hotuba yake, Kweweta pia alitumia nafasi hiyo kuikumbusha jamii kuhusu Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2023/24, ambayo ilionesha upotevu wa zaidi ya shilingi trilioni 2.56 kupitia ubadhirifu, miradi iliyokwama, na uzembe wa serikali.
“Kilwa haikupaswa kuwa nyuma hivi. Tunapoteza fursa za maendeleo kila mwaka kwa sababu ya watu wachache wanaotumia madaraka kwa maslahi yao binafsi. Hatuwezi kunyamaza tena!” Aliongeza.
ACT-Wazalendo imekuwa mstari wa mbele kusisitiza kwamba ushiriki wa wananchi katika uchaguzi ni njia halali ya ukombozi, na kwamba kura ni silaha halali ya kuiondoa CCM madarakani ili kuweka msingi wa uwajibikaji na matumizi bora ya rasilimali za taifa.
Hatua ya Idrisa Kweweta kuwania ubunge imepokelewa kwa shangwe na matumaini makubwa miongoni mwa wananchi wa Kilwa Kusini, huku wengi wakisema huu ndio mwanzo wa zama mpya na damu mpya.