Kwenye swala la mapenzi wanaume hawana mzaha...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwenye swala la mapenzi wanaume hawana mzaha...!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Sep 29, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Sep 29, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Inasemwa kwamba wanawake ni viumbe wa ajabu lakini naamini wanaume ndio viumbe wa ajabu kupindukia. Kwa nini ninasema hivyo? Ninasema hivyo kwa sababu, wanawake kwa ujumla wao wanavyo vibweka vyao katika swala zima la mapenzi, lakini ukija kwa wanaume naamini nao wanavyo vibwekwa vyao tena vya hatari ukilinganisha na vile vya wanawake.Kwa mfano, hivi ni mara ngapi tumeshawahi kusikia baadhi ya wanaume wakiamua kujinyonga kwa sababu ya kushindwa kuwashawishi wanawake wanaowapenda?Namini kuwa matukio ya aina hiyo yapo sana na sio kwa hapa nchini tu bali pia hata katika nchi zilizoendelea.

  Linapokuja swala la mapenzi kuna baadhi ya wanaume wanakuwa kama Nyati waliojeruhiwa, na ndio sababu unaweza kukuta baadhi ya wanaume wanajiingiza kwenye vitendo viovu kama vile vya wizi au ujambazi kwa lengo la kuwashawishi wanawake wanaowapenda ili wawakubali. Wakati mwingine hujiingiza kwenye matumizi ya Pombe kupita kiasi au hata matumizi ya Bangi na madawa ya kulevya kutokana na kuachwa na wanawake wanaowapenda.
  Tabia hii ya wanaume kuhatarisha maisha au hata kupoteza maisha ni la tangu enzi za kale. Kuna simulizi nyingi tulikuwa tukisimuliwa enzi za utoto wangu huko nyumbani kwamba kuna wakati wanaume walikuwa wakipigana ili kumgombea mwanamke na shujaa anayeshinda katika ugomvi ndiye anayemchukuwa mwanamke anayegombewa.Inaonekana wazi kwamba uwezekano wa mwanaume kufa mapema au kuhatarisha maisha yake ni mkubwa ukilinganisha na ule wa wanawake.

  Na hiyo inatokana na wanaume kupenda sifa na kutaka kuwamiliki wanawake wawapendeo. Kuna matukio mengi ya kusikitisha ambayo huwa tunayasoma katika vyombo vyetu vya habari ambapo matukio kama yale ya mwanaume kumuua mwanaume mwenzie ili kumpata mwanamke ampendae ni vya kawaida kabisa.
  Hivi kumekuwa na uhaba wa wanawake kiasi cha kupelekea baadhi ya wanaume kuhatarisha maisha yao au kupoteza maisha kutokana na kumgombea huyu kiumbe mwanamke au kuna kitu kingine kinachotafutwa hapo?

  Ni nadra sana kusikia mwanamke kamuua mume baada ya kumfumania au kumuua mgoni wake tofauti na wanaume. Kama ukipima jambo hilo kitakwimu basi utapata idadi ya wanaume ya kutosha ukilinganisha na ile ya wanawake. Kimsingi wanaume wamewageuza wanawake kama mali zao wanazozimiliki na hiyo ndio sababu inapotokea kumfumania mkewe au mchumba wake akiwa na mwanaume mwingine mambo mawili yanaweza kutokea, kwanza atamuadhibu mgoni wake au hata kumuua kisha mke naye atasulubiwa au hata kuuawa.

  Lakini, pale anapofumaniwa mwanaume mambo huwa ni tofauti sana. Kuna uwezekano mkubwa wa mke huyo kusulubiwa kwa sababu amemfumania mume na wakati mwingine hata huyo mgoni anaweza kushirikiana na mume huyu kumuadhibu huyo mwanamke aliyefumania.Nadhani kuna haja ya wanaume kujikagua upya na kubadili mwenendo wao mzima juu ya matendo yao ili kuepuka kupoteza maisha kwa jambo ambalo wangeweza kuliepuka.
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  nakaa mbaali kuangalia hii sredi itakavyotiririka....nione wanaume mtakiri?
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  wanamme wa leo hawa, apigane sababu ya mwanamke labda.
   
 4. A

  AGNETH Member

  #4
  Sep 29, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  kweli mtambuzi ulichokisema ni kweli wanaume ndiyo viumbe dhaifu wanamaamzi ya ajabu kweli wanawake wana msimamo wa kujiamini.:frusty:
   
 5. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi unayoyasema ni ukweli kabisa..na mimi nikiwa mwanaume mpaka sasa huwa sielewi kwa nini inapotokozea mwanamke kukucheat inakuwa unbearable kuliko ambavyo yeye akikukuta..Pengine inaweza kuwa ni manhood syndrome ambapo urijali wa mwanaume unapimwa kwa namna anavyoweza kummliki mke?..au ni jamii tu ndiyo ambayo imemjenga mwanaume kuamini hivyo anavyoamini???..kiukweli sina jibu..ngoja wengine waje pia wamwagike!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  mmmhh, manhood syndrome? Interesting. .
   
 7. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Wewe unahisi ni kwa nini?..manake kuna kipindi hapa jukwaani unakuwaga mwanaume ati!!
   
 8. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Kadri siku zinavyo kwenda mambo yanabadilika ni kama mabadiliko ya teknolojia yanavyokua, mengi ya ajabu tuyategemee huko mbeleni...:frusty:
   
 9. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  leo ndyo leo!enhe hebu mtuambie kisa cha kutungangania watoto wa wenzenu hata kama hatutaki nakwambia mnatuwekea bifu kisa nimekataa au nimekuacha ,jamani kwani kipochi manyoya si changuuuuuuuuuuuuuu!ah hebu semeni leo hapa!
   
 10. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Nadhani mahari na mshahara wangu vinahusika hapa! lol!
  As long as nakuhudumia lazima nihakikishe siibiwi hiko kipochi!
   
 11. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,262
  Trophy Points: 280
  hamna cha mahari wala nini. Tena ukuta jitu limemuacha gf wake kwa mbwembwe na matusi kibao. Hufai, kahaba, una bwawa, mchafu, mvivu na sifa lukuki. Na akimuona na mwanaume mwingine anawasha moto tena! Eboooh, akili zenu hazinaga akili atii.
   
 12. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  King'asti binti Mtambuzi taratibu mama!
  Kusema ni rahisi sana ila kusikilizia maumivu ni habari nyingine ati..
  Binafsi naamini ili niishi kwa amani lazima niende mbali na alipo my ex-gf/wife..
  I cant wait to see her chilling out with a stranger in front of my eyes!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  mahari yenyewe utakuta mliomba discount kibao,mshahara wenyewe unasema eti tugawane matumizi kisa na siye twafanya kazi, untakuta jitu lilikuacha lenywe lakini likisikia unaolewa oh naua!kha kwani aliyewaambia tukishawaonjesha siku moja au mbili tatu mnatumiliki milele ni nani?au jitu uliachana nalo siku nyingi tu likikuona linajipa uhakika kuwa huruki kamba lazima likakufungue zipu ya sketi madai yenu mtalaka hatongozwi !nyie vipi banaaa hebu mtuambie hapa leo kipi hasa kinachowapa hicho KITENZI KIMILIKISHI?
   
 14. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  unakuwa unakumbukia yale mavitu enh kuwa nakula mwenzio sa hizi!ahahahhahahhah ila sijui huwa kwanini huwa inawauma hivo,kwani huwa mnajisikiaje?
   
 15. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #15
  Sep 29, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ukweli utabaki kuwa ukweli wanaume tukowadhaifu sana kwenye hili swala ndio maana tunakuwa na maamzi ya ajabu pengine hata kuua au kujiua bilasababu yoyote ya maana
   
 16. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Unajua nini pacha?..wakati mwingine inategemea na sababu za break up yenyewe
  Kuna wakati mnaachana na mtu sio kwamba humpendi ila ni kwa sababu ameshindwa kupendeka..
  Yaani unamuacha kimwili lakini roho inakuwa bado inamkumbuka..kwa sababu kama hzi lazima karoho kawivu kataendelea kuwepo as unakumbukia those old fine days na mapochopocho tele alokuwa anakupa. Sasa inakuwa mbaya kama ndio unamfumania yaani from nowhere unambaba live..anakomaje???..There is no single word to explain this scenario..ila elewa tu mke anauma sana aiseee!!
   
 17. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  ndo msitufanyie mbofumbofu sasa!
  mtuleee kama mayai,
  mtudekeze kama mabinti wafalme,
  mtupende kama mioyo yenu,
  mtulee kama lulu,
  mtulinde kama maisha yenu,
  mtupe raha kama mahulain,
  mtuenzi kama mboni zenu,
  mtuheshimu kama nafsi zenu,
  mtuelewe kama miili yenu na
  mtupe mapenzi kama uhai wenu!
   
 18. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,262
  Trophy Points: 280
  baelezee! SnowBall, sema hivi: hatupendi kuona ex akiwa na furaha. Afu wanawake wajanja, akiachwa ndo anapendeza balaa. Hehehe, mnalooo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  walahiiiiiiiii mwanamke unanikuna (kiganja) weyeeeee
  neno kuntu hilo
  loh!!!! mie msomaji tu hapa
   
 20. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  neno hilooooo.....
  SnowBall upoooooo?

  Na hiimiwaendee wanaume woooote wasiojua majukumu yao kwa wanawake.......
  Na iwaendee wooooote wanaodhani wanawake ni vyombo si binadamu.......

  Na iwaendee wooooote wanaopenda hatimiliki burebure bila jasho.......
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...