Kwenye suala la Wamachinga, Rais Samia umevunja ahadi na umewasaliti Wamachinga

Hili zoezi ni kipimo tosha kwamba sera zetu hazina tija, nizile zinazo badilika badilika(uncertainity policies). CCM hawana mfumo wezeshi wa kufanya biashara kisheria ,kwakinyakyusa tunasema :Business enabling environment (BEE) which will follow regurations and rules of the state
 
Yaani wewe unaona fahari ya majengo ya mji kuliko shibe ya watu?

Hivi nyie watu mna utu kweli?
Mkuu hawana na hawajawahi kuwa na utu hata siku moja hawa ndio katili kuliko kiongozi yeyote aliyewahi kuwepo kwa taifa la Tanzania na mkoa wa Dar es salaam.

Kulikuwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam hapo zamani ajulikanaye Mustafa Nyang'anyi alitesa sana wananchi wenye itikadi tofauti na mawazo ya kijamaa, but he is no longer sitting at the helm!!!
 
I fully concur with you Benny Haraba, you nailed on the fresh wound!!!!
 
Nimepita relini kuna mama amenambia na TRC wametoa Notes wanaofanya biashara za pembezoni hasa kina mama ntilie wasepeeeeeee,Ukiangalia huyo mama ntilie alipo labda kama reli wanajenga Barabara sita za treni hivi karibuni
 
Zoezi linaenda vizuri na miji yetu tunayoijenga kwa gharama kubwa inaenda kuonesha value for money

Hakuna machinga aliyekatazwa kufanya biashara! Ni wewe ndo ubadili akili yako kwa kujifunza kwenda sokoni kununua bidhaa!

Lazima kila kitu kiende kwa utaratibu! Sisi sio wanyama ni binadamu
 
Maadamu matajiri wamemuhakikishia atakuwa Rais milele hawa machinga na bodaboda ni takataka.
 
Nimepita relini kuna mama amenambia na TRC wametoa Notes wanaofanya biashara za pembezoni hasa kina mama ntilie wasepeeeeeee,Ukiangalia huyo mama ntilie alipo labda kama reli wanajenga Barabara sita za treni hivi karibuni
Yaani kuna ukatili na roho mbaya ajabu katika nchi hii.
Labda huu ndo utakuwa mwanzo wa Watanzania waliolala kuamka, maana ugali wao sasa unamwagiwa mchanga
 
Maadamu matajiri wamemuhakikishia atakuwa Rais milele hawa machinga na bodaboda ni takataka.
Na hili ni tatizo.
Naona akina Majaliwa wanakazana kusema yeye ndo raisi hadi mwaka 2030.

Hawana hofu tena ya wananchi maana watafanya magumashi yao tu wanayoyajua kwenye chaguzi
 
Usimtishe Rais kwa hoja zako zisizo na mashiko

Kwanza unatakiwa ujibiwe kihuni kama ulivyoletwa kihuni.
1. Machinga wnaoweka makazi sio machinga halisi. Machinga ni mtu wa kutembeza vitu,haitaji kukutana na serikali kwani ni mtu wa mwendo. Hawa wamebaki wauza ulembo, vitana, soksi. Sasa machinga gani anamiliki duka hangani la vipodozi, shehena na vinywaji.
2. Machinga ni source ya bidhaa feki zilitotapakaa mjini. Huyu uhuza pombe feki, simu feki, vitu vya umeme feki.
3. Machinga anauza mali iliyoiibiwa madukani, hatoi risit kwa kuwa yupo free.
4. Machinga anasababisha ajari za magari kwani wanapanga vitu njiani kuziba wapita njia mpaka wanaingia njia kuu.
5. Machinga anazalisha taka asizohudumia mfano anakamua juice ya miwa, anauza matunda kama mabasi, machungwa taka anaacha pale bila kufikia.
6. Machinga alikuwa anazuia parking system, sehemu ya magari wanayolipa elf tatu kwa siku anachukua yeye kwa kuweka takataka zake.
7. Machinga maficho ya vibaka, ile kangomba inafanywa sana, unauziwa viatu vibovu kwa kufungiwa feki.
8.achinga wanauza bidhaa zote zilizowekewa zuio wanauza kwa magendo, uuza bidhaa zilizoisha muda.
9. Machinga wanazuia maduka halali wasifanye biashara na wanakiburi sana wanapoambiwa wasogee.

Kuna mengi mabaya wafanyayo ila tuishie hapa
 
Na hili ni tatizo.
Naona akina Majaliwa wanakazana kusema yeye ndo raisi hadi mwaka 2030.

Hawana hofu tena ya wananchi maana watafanya magumashi yao tu wanayoyajua kwenye chaguzi
Sasa ndo naelewa kwanini waziri mkuu ni ngumu kuwa rais,ni Nyerere tu alipenya.
Kumbe unafiki na kujipendekeza kwa rais kunawafanya waonekane wa hovyo
 
Baadhi yenu tayari mitaji mizuri mnayo
Kwani mlikua maeneo mazuri rent free tax free
Ni muda sasa mpangishe fremu muendelee na maisha rasmi kama watanzania wengine wengi
 
Ukipata sheria ya kitambulisho cha machinga elfu 20 ntakupa zawadi

Lile lilikua ni tamko sio sheria
Na ndo mana leo hii hamna anaeviulizia...
 

Machinga ni mtanzania ambae humlishi, humtibu,humpi malazi na elimu
 
Busara na sheria kipi ni sahihi kutumia kwa ajili ya kufanya maamuzi sahihi kwa uelewa wako?
 
Naona CCM wametoka mafichoni kulaani zoezi linavyoendeshwa, yaani wanaibuka leo baada ya uharibifu mkubwa wa miundo mbinu ya wamachinga na hata uporwaji wa mali zao, Hii ni aibu kubwa sana kwa serikali hii ya Samia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…