mr pipa
JF-Expert Member
- Jul 26, 2021
- 4,345
- 9,316
Sote tunafahamu kuhusu maumivu waliyopata wakulima msimu uliopita
Kutokana na bei za mbolea kuwa juu
Licha ya hali ya hewa kubadilika na baadhi ya sehemu kuwa na mvua chache ila haikuwa hivyo kwa kila mkoa mfano ruvuma msimu uliopita mvua zilikuwa za kutosha sana
Ila wakulima walishindwa kuzalisha kwa wingi kutokana na hizo pembejeo kuwa juu
Licha ya bajeti ya serikali ya 2022)/2023 kuwekeza % kubwa kwenye kilimo ila sizani kama utekelezaji wake utakuwa na ufanisi
zaidi ya hiyo pesa kupitia mikononi mwa wajanja
Wenyewe tunajionea kwenye suala la pesa iliyoongezwa kwenye mafuta
Ushauri wangu ni huu kwanini tusichague baadhi ya mikoa inayo zalisha kwa wingi mazao ya chakula na tukaipa punguzo, au tukaingiza kiasi kikubwa huko,?
Mfano mbolea ikifika dar es salama ikiwa mfuko ni elfu 80 basi tuangalie mikoa gani inalima sana na tukaingiza kiasi cha bajeti kwenye hiyo mikoa ili huko inakwenda ikauzwe tsh elfu 50? alafu huku kwenye mikoa mingine ingebakia hivyo hivyo ili kumpa nguvu huyu mzalishaji maana mikoa inayozalisha kwa wingi si tunaijua nazan haizidi hata minne, je serikali itashindwaje kuwekeza hata kwa hili
Kuliko sasa kutoa ruzuku alafu matokeo ya hiyo ruzuku wanakula wachache,
Nakumbuka raisi wa awamu ya nne alikuwa akitoa ruzuku kwa wakulima vijijini ila matokeo yake viongozi wake walikuwa wakijiandikisha wao na watoto wao na hadi makaburi ya babu zao ili kufaidi ile ruzuku matokeo yake mkulima hanufaiki moja kwa moja
Kwa sababu nchi yetu watu wake hawana uzalendo rais utakuwa na nia njema ila watu wako watapigana wajinufaishe matokeo yake lawama zitarudi kwako