- Thread starter
- #481
Uko sawa, kwenye ule mchanga ni ni vigumu sana kuwekwa 500g/t.Nimefanya kazi katika moja ya migodi mikubwa Tanzania inayozalisha mchanga wa dhahabu kwa zaidi ya miaka 2 so najua at least 90% ya kinachohusiana na mchanga wa dhahabu
Mchanga unaosafirishwa nchi za nje kutoka katika Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu ni mchanga wenye mchanganyiko wa dhahabu, copper, silver, iron na vinginevyo. Process inayofanya ili kutengeneza mchanga wa dhahabu ni flotation ambayo nia yake ni kupunguza uwepo wa copper katika material ambayo hupelekwa katika Carbon In Leach (CIL) circuit. Uwepo wa copper katika CIL circuit uwa unaathiri uzalishaji wa dhahabu maana cyanide uwa inareact sana na copper than dhahabu na mwisho dhahabu hutoka katika makapi. Hii ndio sababu pekee ya inayofanya migodi kupunguza copper katika circuit.
Kiwango cha dhahabu katika kontena moja la Mgodi XXX uliopo Kahama uwa ni around 150 - 270 g/t, Copper uwa ni 12 – 18% (1% = 10,000 ppm, 1 ppm = 1 g/t) na silver ni around 200g/t. For example katika mwaka wa 2011, Average gold iliyozalishwa na kuwekwa katika makontena ilikua ni around 262.031 g/t na copper ilikua ni 16.532 %. Pia September 2013, Average gold ilikua 186.83 g/t na copper ilikua ni 12.58 %.
Tanzania Minerals Audit Agency (TMAA) ni agency ya serikali ambayo uwa inachukua sample za mchanga kwa ajili ya analysis ili kucompare majibu ya huo mchanga na majibu ya mgodi kwa ajili ya kodi. Cha kujiuliza ni je watu wa TMAA wanachukua sample kwa usahihi? Uwa wanachukua spear ngapi katika kila kontena ili wapate representative sample? Je watu wa TMAA wanafanya Analysis kwa mashine ambazo zinakua calibrated kila baada ya muda? Je ni muda gani wanacalibrate hizo mashine zao? Je wamewahi kuchukua sample zao na kupeleka katika Laboratory nyingine ili kumake comparison ya majibu yao na ya wengine ili kuona kama wako sahihi au lah?
Baada ya sample kuchukuliwa, ni wakati wa maafisa wa mgodi husika, TRA, MEM na TMAA kuyafunga yale makontena kwa kutumia seal.
Napenda kusema kua kauli iliyotolewa na Engineer mmoja pale bandarini kua ndani ya makontena hayo asilimia 90 ya mchanga ni dhahabu na sio shaba ni ya UONGO kwa asilimia zaidi ya 100. Napenda kusema kua alikosea sana na alistahili kutoa kauli ya kuunda tume ili kuhakikisha walichoreport TMAA na Migodi kama viko sahihi au lah. Kauli yake inaonesha kua TMAA na Migodi uwa wanatupa report za uongo kuhusiana na kiwango cha madini kilichopo ndani ya makontena. Kauli ya aliekua Katibu Mkuu wa Wizara kua iundwe Tume ilikua ni njia sahihi kuthibitisha kua kilichomo ndani ya Makontena ni kitu sahihi kama report zilivyowasilishwa na TMAA na Migodi au lah.
Note: 1. Calibration is the process of calibrating an instrument or experimental readings.
2. Spear ni kifaa maalumu cha kuchukulia sample katika yale makontena
No research.. No right to speak Ndg. Engineer Kakonko