Kwenye Royal tour tumepata hasara! Rais Samia hakupaswa kuwa peke yake filamu ilipaswa aongezewe mtu mwenye ushawishi! Washauri mmemdanganya Rais

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,210
42,072
Ukweli ni kwamba kwenye sekta ya utalii lazima tukubali kuwa Rais Samia awezi kuwa na ushawishi wa kuwavuta watalii au kuvuta watu kuangalia filamu ya royal tour maana hakuna kitu ambacho anawezi kuwavutia wengi hasa duniani kuitazama!

Washauri wa Rais walipaswa kujua kuwa ili watu watazame filamu fulani lazima kuwe na sababu nyingi ikiwemo umaarufu wa mtu aliyeshiriki kwenye filamu hiyo! Walitakiwa kujua kama wanataka Samia aonekane kwenye Tv basi wangemuacha aonekane lakini watafute mtu mwingine mwenye ushawishi duniani kote na kwa watu wengi ili filamu iwe na mvuto si kwa wamakonde tuu bali dunia nzima!

Mfano kama Samia angekuwa na Ronaldo kwenye filamu unafikiri kingetokea nini?

Kama Samia angekuwa na Mess kwenye Filamu kingetokea nini?

Kama Samia angekuwa Kanye west kwenye Filamu kingetokea nini?

Hii ni moja ya mifano ambayo nimejaribu kuifikiri kwa haraka ambayo naona ingelipa zaidi kuliko Rais samia kushiriki peke yake kwenye filamu hii kitu ambacho hakitakuwa na effect yeyote kwa nchi zaidi tutajikuta tunalishwa propaganda kuwa watalii fulani wmeletwa na Royal tour kumbe siyo!

Kwenye ulimwengu wa watu mashuhuri na wenye ushawishi duniani lazima tukubali ukweli mchungu kuwa Rais Samia sio mmoja wao hivyo hakufaa kuwepo au kushiriki pekee kwenye hiyo fialmu kama tunataka matokeo kweli na sio siasa!

Kama swala ni hela ukweli ni kwamba nchi hii haiwezi kushindwa kutumia hata zaidi ya billion hata 30 kuwekeza kwenye utalii na matangazo kwani tumekuwa na matumizi mabovu zaidi ya mabillion na mabillion!

Hivyo ni ukweli usio pingika katika hili la kuitumia filamu kutangaza vivutio tumepata hasara kwa kuwa tumeshindwa kujua tumtumie nani kuwafikia wakina nani!
 
Leak usiwe kama wale waliokuwa wanampinga Dkt Magufuli 24/7, hoja zako hazina maana sana kwa sababu kuwaleta hao watu ni too expensive. Mama alichokifanya ni sawa kulingana na hali yetu. Kosa tu kubwa la Mama ni kuendeleza vijembe kwa Dkt Magufuli
 
Ungefupisha tu kusema kwamba, hii movie ilipaswa kua chini ya director Mell Gibson na Harrison Ford ambao ni ma-director wakubwa kule Hollywood.... Movie ingebamba sana.
Ungekuwa tayari hao ( hawa ) Walipwe Matrilioni ya Pesa ili Filamu ikamilike utakavyo na Tanzania ( hasa Hazina ) iishiwe Pesa kabisa na tuanze kupiga Miayo na Kushindia tu Maji na Uji wa Chumvi?
 
Hao unaowataja,lazima wangetaka kulipwa na kutaka mikataba minono,wangesema kila pesa ya utalii,itakayoingia wanataka 10%,pia ungekuja kulalamika,kama pesa inatumika ovyo.

Hakuna mtu maarufu,atakayeshirika Tangazo la biashara,asilipwe,lazima atataka alipwe,tena pesa nyingi tu.
 
kumbe hiyo filamu wewe umeshaitazama tupe basi yaliyojiri humo in summary alafu mkuu hiyo royal tour si kwa ajili ya kuuza sura lengo ni kuonekana maliasili zetu na mbuga zetu adhimu
 
Ungekuwa tayari hao ( hawa ) Walipwe Matrilioni ya Pesa ili Filamu ikamilike utakavyo na Tanzania ( hasa Hazina ) iishiwe Pesa kabisa na tuanze kupiga Miayo na Kushindia tu Maji na Uji wa Chumvi?
Filamu gani tena ifike Trillion kaka
Kikwete aliwahi kusema ' Ukitaka kula lazima uliwe'

Uwekezaji mkubwa katika utalii utakuja kuleta positive impact katika kupunguza hasara za ndege zetu hapa nchini.

Wewe unahis Rwanda wanatoa gharama gani katika kutangaza nchi yao ndani ya ulimwengu wa soka huko ulaya..?

Alichofanya Rais ni sawa kabisa lakini kama kuna shida lazima tuzungumze ili baadae yafanyike yaliyo bora zaidi.
 
Au wangeweka vipande vipande vya hotuba za Mwamba Magufuli alizokuwa anatoa kwenye ziara zake za barabarani. Mwanangu hata Putin na Zelensky wangeitazama!
 
Mfano kama Samia angekuwa na Ronaldo kwenye filamu unafikiri kingetokea nini?

Kama Samia angekuwa na Mess kwenye Filamu kingetokea nini?
Kaka tungeweza kuwalipa? kumbuka ukitaka kumtumia hawa ma Super Staa kwenye matanganzo yako mziki wake ni wa balaa, nenda kawaulize Adidas ama Nike watakueleza.
 
Back
Top Bottom