kanjuki
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 209
- 95
Habari ndugu watanzania wenzangu, sera ya elimu kwa sasa katika shule za umma ni elimu bure yani wewe mzazi jukumu lako mzazi ni kumuandaa mtoto na kuhakikisha mtoto anafika shule, lakini katika uhalisia ulivyo kwa uchunguzi wangu unakuta michango ambayo unatoa ili mtoto apokelewe shule ukipiga hesabu unashangaa
Hebu fikiri unampeleka mtoto na unatakiwa kutoa michango ifuatayo
Mchango wa kiti na meza 100000/=, mchango wa choo 100000/=, rangi ndoo 2, rimu 2, mchango wa chakula mahindi kg 60, maharage 40, na bado hapo hujapigwa fyekeo, jembe, hela ya mpishi, mlinzi na mengine mengi.
Hebu fikiri hivi mzazi mkulima, mjane, na mlala hoi anawezaje kupeleka mtoto shule ?
Lakini pia kumekuwa na shule za umma viongozi wake kujifanya miungu watu tena wanatumia kanuni ya kuitisha vikao vya wazazi na kuwapanga wazazi wachache waibue hoja na ajenda zenye maslahi kwao, kisha wanazipitisha ajenda na wanazigeuza kuwa sheria wanazozisimamia kwa nguvu na mabavu mengi, kumbe kuna mchongo umetengenezwa kuanzia kwa mkurugenzi, afisa elimu, na vitengo kibao...inakuwa sehemu ya upigaji. Wananchi wenzangu tuamke.
Nina ushahidi wa shule kadhaa ndani ya wilaya hapa nilipo.