Mpare wa Gonja
Member
- Feb 26, 2014
- 52
- 46
Habari,
Nawaandikia nyie nyote mliopata dhamana ya kuteuliwa kutuongoza katika teuzi kuanzia Ukuu wa Mikoa,Ukuu wa Wilaya hata nyie Wakurugenzi wa Majiji,Halimashauri za Miji n.k.
Nawaandikia Mwendemkasome Kitabu kiitwayo FUNGATE LA UHURU,tena niwakumbushe wakati nyinyi mkisoma hicho kitabu cha FUNGATE LA UHURU,sisi tutakuwa tukisoma Kitabu kiitwacho WASAKA TONGE.
Nawaandikia kuwakumbusha kwamba sisi wenzenu hiki Kitabu cha WASAKA TONGE,tulikielewa,tunakielewa na tutaendelea kukielewa hata kabla ya kukisoma.
Nawaandikia kuwaelewesha kwamba wakati ule wa vuguvugu la kuelekea mapinduzi ya Nzazibar wezenu walisomana tena kwa ufasaha kabisa kile kitabu cha VUTA N'KUVUTE,ama kwa hakika kilieleweka fika matokeo yake sina sababu ya kuyaandika humu.
Nwaandikia kuwauliza kwamba mnakumbuka kwamba wezenu walisoma kwa umaridadi tena umaridadi mzuri mno Kitabu cha ZAWADI YA USHINDI,kwakuwa alichokipata Nduli AMINI kule UGANDA,hakuna asiye kifahamu kwa kuwa mpaka leo nialama ya ushujaa tunao jivunia.
Nawaandikia kuwajuza wenzenu tunakasi ya ajabu katikakukariri na kuelewa yaliyomo katika Kitabu chetu cha WASAKA TONGE,tukitambua sana, kwamba FUNGATENI pana vinono,lakini halahala,ule Wimbo wa TUMBUA TUMBUA MAJIPU,haujawahi kuwa mtamu masikioni mwenu.
Nawaandikia tena kwa kumalizia kwamba wezenu huku tumekariri na kusadifu kwa ustadim kubwa Wimbo wetu maridhawa wa HAPA KAZI TU.