Kwenu wanawake mlioolewa na mnaotarajia kuolewa

Kwenu wanawake mlioolewa na mnaotarajia kuolewa

bachelor sugu

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
2,689
Reaction score
3,651
Amani ya Muumba iwe juu yenu wote.

Ujumbe wangu leo uwaendee wana wake wote mlioolewa na mnaotarajia kufanya hivyo siku yoyote,Hv ndugu zetu nyie hii roho huwa MNAITOA WAPI?????. Mmekuwa msumari mchungu sana tena ulio imara yaani usiopinda mkigongelea huwa unaingia panapolengwa.

Mmekuwa changamoto kubwa sana kwetu sie wanaume hasa katika ndoa zetu pale ambapo huwa mnaonyesha chuki za dhahiri za kuwabagua ndugu wa waume zenu huku waume zenu wakiwapenda sana tu ndugu wa upande wenu.Nalizungumzia hili nikiwa na ushahidi tosha maana nililelewa na mama wa kambo yaani mke wa baba yangu mdogo ambaye alinichukua kwa wazazi wangu nikiwa na miaka 4 tu na yeye akiwa bado bachelor na muda ulipofika akiniambia twende tukamchukue mama mdogo,dah nilifurahi sana na tukaenda kulikamilisha jambo hilo na kurudi na mama mdogo nyumbani.

Shughuli ilianza pale mama mdogo aliposhika madaraka ya mama mwenye nyumba doooooh sitamsahau kwa kweli japo amenilea mpaka nimeota ndevu lakini mateso aliyonipa kamwe sitaacha kumkumbuka.

Dingi yangu mdogo huyo Mola amlaze MAHALA PEMA PEPONI alijitahidi kuneutralize roho mbaya ya mkewe kwa kuzidisha upendo kwangu na ndugu wengine wa upande wake pia wa mkewe ili tu tusijisikie vibaya but ukweli ulibakia kuwa mkewe alikuwa no ROHO KUUUBWAA TU.
Unakuta mwanaume anakupenda,anakupa kila kitu utakacho ww na ndugu zako but wakija ndugu zake ww kununa shavu limekutuna utadhani mimba ya kurogelezewa vitimbi mtindo mmoja taarabu haziishi hv kweli hayo ndo huwa mnafundishwa huko kwenu kabla ya kuolewa????

Hata huu msemo shemeji ndiye mwenye nguvu nyie ndo mmeusababisha upate promo na kwa wanaume wasiojielewa wanautendea haki vilivyo ila kwangu aisee nitatoa talaka kwa wote kuanzia ww na familia yako yote bila kujali nakupenda kiasi gani na hao ndugu zako.

Mmewafanya mama zetu wawe ni wenye kukesha wakiomba Mungu awape watoto zao wake wema wataokaowapenda na kuwathamini lakini Mara nyingine wameangukia pua na kuona dua zao zimegonga Mwamba baada ya kukumbana na nyie ma Malkia mnaohisi kupendwa kuliko hata Mungu wenu.

Ushauri wangu kwenu Dada zangu kuweni na moyo ya upendo kwa ndugu wa waume zenu kwani hakuna mwanaume anayefurahia mama yake kunyanyaswa wala kusimangwa maana mama zetu nao walipata tabu kutukuza hivyo wapeni nafasi nao wabembelezwe na kupewa raha na watoto zao.

Nimemaliza.

Karibu ni kwa utetezi.
 
Hiyo ni tabia tu ya mtu na haichagui jinsia maana hata wanaume wenye tabia km hizo wapo
 
Hiyo ni tabia tu ya mtu na haichagui jinsia maana hata wanaume wenye tabia km hizo wapo
Mkuu wanaume ni 2% out of 100% wanawake ndo hasa majipu ktk hili na ndo maana unaona wanaugwaya Uzi
 
Moyo wa upendo na kuthamini haujengeki overnight, hiyo Ni tabia ambayo mtu anakuzwa nayo.vice versa pia ni hivo,ndomaana wahenga walisema tabia ni ngozi,ukipata mwanamke asiyependa ndugu wa kiume huyo ni tabia yake tu, Omba Mungu ambadili mkuu
 
Aisee huu msiba ni mzito sana mkuu
 
Ila umeongea ukweli mtupu wanawake tuna roho za ajabu mpaka shetani anashangaa
 
Lakini si zinabadilikaga km tukifanya maombi?
Thubutuuuuu tabia ya MTU haibadiliki hata iweje ....kile kitu kipo ndani ya damu ...kasome genetics utajua kua hakuna tabia inayoweza kubadilishika ispokua ya kuadapt kutoka katika mazingira unayoishi
 
Dah basi km ni hv mtihani wake ni mzito kuliko Maelezo hasa ukishakuwa umemuoa
 
Dah basi km ni hv mtihani wake ni mzito kuliko Maelezo hasa ukishakuwa umemuoa
Ila me huwa nawashauri mwanaume anapotaka kuoa aangalie MTU ambaye ana hofu ya mungu .....hii itasaidia baadhi ya vitu kua sawa kwenye ndoa
 
Ni kweli ...hapo ni kudra za mungu tu zinahitajika ili kumpata mwanamke sahihi katika maisha
Hv eti mwanamke ukishamjua mumeo msimamo wake kuhusu suala km hili hv bado unaweza kwenda kinyume pia?
 
Hv eti mwanamke ukishamjua mumeo msimamo wake kuhusu suala km hili hv bado unaweza kwenda kinyume pia?
Wanawake wa sikuhizi tuna kiburi cha ajabu .....na ujuaji mwingi....ndiyo maana nikasema ukioa oa MTU mwenye kumjua mungu itasaidia sanaaaaaa....ila ukioa sijui mwenye chura ...Mara sijui degree imefanya nini Mara vile kazi unayo
 
Back
Top Bottom