Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,674
- 149,860
Kama mlivyoonyesha kuguswa na sakata la Mbowe kuitwa Polisi kinyume cha taratibu,Melo kushitakiwa na mwanadada Weme Sepetu kutendewa vivyo sivyo kiasi kwamba mkaripotiwa mko tayari kuwatetea hawa wote kwa nyakati tofauti bila kulipwa chochote, nawashauri mjitoe hivyo hivyo katika kutetea wafanyakazi wanaokatwa makato ya asilimia 15 kwa ajili ya kulipia mikopo ya Bodi ya Mikopo.
Watumishi wa umma na wasio wa umma ni kundi kubwa sana na kundi hili linagusa mpaka tegemezi wa watumishi hawa waliosambaa nchi nzima mijini na vijijini.Mbali na ubinadamu mtakaounyesha,hatua hii itakuwa ni mtaji mkubwa sana kisiasa kwenu binafsi na kwa vyama vyenu.
Ingependeza sana na kwakweli mngeandika historia iwapo tungeona jopo kubwa la mawakili kutoka vyama vya siasa mkifungua kesi kama hii katika Mahakama ya Kazi au Mahakama nyingine mkipinga makato haya yasiyo rafiki kwa watumishi na ambayo yanaturudisha nyuma enzi za ujira mdogo na wa kinyonyaji kama ule wa mkoloni kabla ya uhuru.
Najua ile mikataba ya Bodi hawaifungu Bodi kutoongeza kiwango cha makato kadri wanavyotaka (mapungufu makubwa ya huu mkataba) lakini sidhani kama mkataba huu pamoja na ubovu wake unaweza kutumika kukandamizi wanufaika pasipo kujali sheria za kazi, haki na msalahi ya wafanyakazi.
Nawaomba muende Mahakamani mkatumie umahiri wenu kutetea wapiga kura wenu kwani naamini uwezo wa kujenga hoja mnao na nyinyi ni "Big Brain" linapokuja swala la sheria.
Kitu kingine nachowashauri katika kesi mtakayowawakilisha watumishi muiombe pia Mahakama itamke wazi kuwa Mkataba kati ya Bodi na Mwanafunzi /Mnufaika una mapungufu makubwa na muiombe Mahakama ilekeze mkataba huo upitiwe upya na uondoe mamlaka ya bodi/serikali kuongeza makato bila kushirikisha wanafuika na ikiwezekana sheria ikataze kabisa kuongeza makato tofauti na yale yaliyokubaliwa awali kati ya Mnufaika na Bodi hiyo wakati wa kuingia/kusaini mkataba husika.
Kinachohitajika ni nyie mawakili kuonyesha utayari wenu then watumishi hasa wa private sector wasio na hofu ya kufanyiwa "figisufigisu" kwa kuishataki serikali watajtokeza kufungua kesi na kuwaomba nyinyi mawakili muwasimamie mahakamani.
Tukumbuke kuna watu walisoma bure kabisa na hili jukumu bado ni la serikali inayokusanya kodi hivyo serikali haina sababu ya kukwepa wajibu wake.
Haingii akilini serikali kupitia Bodi ya Mikopo kukata asilimia 15 ya mshahara ya wafanyakazi wakati serikali hiyo hiyo inajenga Airpot kubwa katika maeneo yanayozua maswali.