Kwenu TFF; Ubabaishaji huu utaisha lini??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwenu TFF; Ubabaishaji huu utaisha lini???

Discussion in 'Sports' started by Balantanda, Apr 13, 2010.

 1. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Hivi TFF kwa nini hawabadiliki?,wataachana lini na tabia hii ya kuahirishaahirisha mechi za ligi kuu ya VodaCom na kuvuruga ratiba?,soma habari hii hapa chini toka gazeti la MwanaSpoti,inakera...

  AIBU YA MWAKA
  FRANK SANGA
  KWA neno jepesi unaweza kusema ni aibu. Lakini kukosa mipango, ubabaishaji na kuendesha mambo kienyeji kumedhihirika tena katika soka ya Tanzania.

  Kama televisheni ya Skysport ambayo ina haki ya kuonyesha Ligi Kuu England ingekuwa na mkataba wa kuonyesha mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, kesho Jumapili wangevunja mkataba huo.

  Skyports ina mkataba wa kuonyesha laivu mechi 92 za Ligi Kuu England huku ESPN ya Marekani ikipewa haki ya mechi 46. Na hakuna shaka kama wangekuwa wanaonyesha mechi za Ligi Kuu Tanzania kesho Jumapili ingekuwa ndio mwisho wao.

  Hata wadhamini wa Ligi Kuu Bara, Vodacom wakiamua kujitoa hakuna ambaye atawalaumu kutokana na ubabaishaji ulionyeshwa jana Ijumaa katika medani ya soka Tanzania.

  Mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga ambayo imetangazwa kwa zaidi ya miezi saba kuwa ingefanyika kesho Jumapili, imeahirishwa ghafla na sasa itafanyika Jumapili ya Aprili 18 huku baadhi ya mashabiki wakiwa wamesafiri kuja Dar es Salaam kutoka mikoa mbalimbali.

  Kwa mara nyingine, Serikali imedhihirisha haijifunzi na kurudia makosa yake ya miaka ya nyuma baada ya waziri aliyekuwa na dhamana ya kusimamia michezo wakati huo, Profesa Juma Kapuya alipolazimisha timu nane kushiriki ligi ya "Nane Bora' wakati makubaliano na wadhamini yalikuwa ni timu sita 'Sita Bora'.


  Ni miaka hiyo ya mwishoni mwa tisini wakati misimu miwili timu hazikushuka daraja kutokana na msimamo wa waziri huyo.
  Hatua hiyo ilisababisha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kujiondoa kudhamini ligi hiyo kutokana na kuona hatua hiyo ilikuwa kinyume cha makubaliano yao na kilichokuwa Chama cha Soka Tanzania (FAT).

  Mmoja wa wachambuzi wa soka nchini aliliambia Mwanaspoti kuwa hiyo ni aibu kubwa na inaweza kuathiri matangazo ya televisheni, redio, wadhamini na kupunguza mashabiki wa soka.

  "Kama Supersport wangetoka Afrika Kusini kuja kuonyesha mechi hii, ingewaje iwapo wangefika na vifaa vyao na kuambiwa mechi imeahirishwa? " Alihoji mchambuzi huyo maarufu wa soka.
  "Makampuni yanafanya biashara, hayataki kujihusisha na ubabaishaji, hivyo iwapo wadhamini wakijitoa hakuna wa kulaumu, kwani huu ni ubabaishaji," alisema.

  Habari kutoka ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zinadai kuwa serikali imetoa shinikizo kuahirishwa kwa mechi hiyo ikitaka ifanyike kwenye Uwanja wa Taifa, licha ya kujua kuwa Simba na Yanga zilitangaza tangu mwanzoni mwa wiki kuwa wangefanyia mechi hiyo Uwanja wa Uhuru kukwepa gharama kubwa Uwanja wa Taifa.

  Kuahirishwa kwa mechi mara nyingi hutokana na sababu za msingi na zisizokwepeka mathalani maji kujaa uwanjani, barafu au majanga mbalimbali.

  Kutokana na hilo, kocha wa Yanga, Kosta Papic amegeuka mbogo baada ya kuambiwa mechi yao dhidi ya Simba imeahirishwa na ameiita kuwa ni hujuma, lakini Kocha wa Simba, Patrick Phiri akasema: "Ndio maisha haya."

  Papic na Phiri walizungumza na Mwanaspoti jana Ijumaa kwa muda tofauti kuhusu kuahirishwa kwa mechi hiyo.

  Papic kutoka Serbia aliiambia Mwanaspoti kuwa, kitendo hicho ni aibu kubwa na kinatia hasira kwani si uamuzi sahihi kuahirisha mechi kubwa kama hiyo.

  "Nina hasira, tumefanya maandalizi siku zote kwa wiki nzima, halafu watu wengine wanakutana na kuahirisha mechi," alilalamika kocha huyo aliyezaliwa mwaka 1960.

  Papic maarufu kwa jina la Bill Clinton alisema aliandaa timu yake vizuri na wachezaji wake walikuwa katika morali ya juu, hivyo kitendo hicho kimewakatisha tamaa kwani ni muda mrefu Yanga haijacheza mechi ya mashindano.

  "Tumekaa muda mrefu bila kucheza mechi, hii inaweza kutuathiri. Tumejiandaa vizuri, wachezaji na mimi, wote tuna hasira sana kwa uamuzi huu, hatuelewi tufanye nini. Gharama hizi nani atalipa hotelini? " Alihoji Papic mwenye watoto wawili kwa mke wake, Milka.

  Papic ambaye alikuwa anazungumza kwa hasira alisema haelewi kama awarudishe nyumbani wachezaji wake au aendelee kuwaweka katika kambi iliyopo kwenye Hoteli ya Holiday Inn, Dar es Salaam.

  Lakini Phiri alizungumza kwa hadhari na ufupi na kusema kuwa suala hilo ni la kiutawala, hivyo hawana jinsi ya kufanya.
  "Hatuwezi kufanya lolote, ndio tayari imetokea, tunachotakiwa ni kukaa chini na kujipanga upya, ingawa tulikuwa tumemaliza mandalizi yetu," alisema kocha huyo wa Zambia.

  Phiri aliyezaliwa mwaka 1956 alisema katika maisha ya binadamu kuna mambo mengi yanayotokea kila mara na hii ni sehemu ya maisha hayo.

  "Ndio maisha," alisema Phiri: "Tulijiandaa kwa mechi ya Jumapili, lakini kila kitu kimebadilishwa kwa hiyo tunatakiwa kujiandaa kwa mechi ya Aprili 18, hatuna jinsi," alisema Phiri kutoka Zanziba
   
 2. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  TFF yamchefua El-Maamry kuhusu kubadili ratiba

  Vicky Kimaro
  MJUMBE wa heshima wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Said El Maamry amelishutumu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa kubadili ratiba ya ligi kila mara ikiwa ni pamoja na kitendo cha kusogeza mbele pambano la watani wa jadi Simba na Yanga.

  Awali mechi hiyo ilikuwa ichezwe Jumapili iliyopita kwenye uwanja wa Uhuru, lakini TFF wameisogeza mbele na sasa itachezwa usiku kwenye Uwanja wa Taifa Jumapili ijayo.

  Akizungumza na Mwananchi, El Maamry alisema TFF wanatia kichefuchefu kwa maamuzi yao ambayo wanaonyesha wazi kuwa hawana msimamo na wanaendeshwa na Simba na Yanga na ndio maana wamekuwa wakiziabudu na kusahau kuwa Ligi pasipo timu nyingine haiwezi kuwa ligi.

  "Hatukatai kuwa Simba na Yanga ni timu kubwa zina wachezaji wazuri zinapendwa na watu wengi, lakini pia wanatakiwa wajue ni klabu kama zilivyo klabu nyingine, ligi haiwezi kuchezwa na Simba na Yanga tu wazifikirie na hizi timu nyingine wajue kuna haki wanazinyima kwa kuziegemea Simba na Yanga tu.

  "Fikiria Ligi inasogezwa mbele kwa ajili ya Simba na Yanga kigezo tunachoambiwa eti wamebadilisha uwanja ili serikali iweze kujipanga, hivi ratiba ya ligi si imekuwa ikipangwa mapema, hizi timu si zilikuwa zinajua zitacheza sasa kwa nini kama suala ni makato makubwa kwenye Uwanja wa Taifa wasikae wakajadili hilo suala mapema, hadi wasubiri mechi karibuni ndio waibuke na kujifanya makato makubwa siku zote si walikuwa wanajua makato yanayokatwa?"alisema kwa kuhoji.


  " Kitendo walichofanya sio kizuri hata kidogo wanazinyima haki klabu nyingine, hata ingekuwa sikukuu mchezo ungechewa wenzetu Uingereza utakuta sikukuu ya Pasaka na watu wanacheza, lakini kwetu sikukuu hakuna mechi tena wangeweza kupata mapato mengi kwa vile watu wengi wanakuwa nyumbani, TFF kwa hili wanapaswa kuomba radhi kwa kitendo chao cha kutokuwa na msimamo na ratiba yao ya ligi."

  Hata hivyo El Maamary aliipongeza TFF kwa kusimamia vizuri ligi ya mwaka huu na kudai kuwa imeenda vizuri tofauti na siku za nyuma pamoja na kasoro ndogo zilizojitokeza.

  "Waamuzi kidogo walitaka kuvuruga ligi, naipongeza TFF kwa kuchukua uamuzi wa haraka wa kuwaondoa waamuzi waliodaiwa kula rushwa Songea, ni wajibu wa TFF kutoa mafunzo zaidi kwa waamuzi na ligi ijayo mwamuzi atakaonekana kuwa na harufu tu za rushwa haondolewe mara moja hakuna hata haja ya kuunda kamati kuchunguza," alisisitiza.

  Chanzo: Gazeti la Mwananchi
   
 3. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,019
  Trophy Points: 280
  Hata uingereza mechi kibao zilihairishwa kutokana na sababu mbali mbali kama hali ya hewa, kama FA wanahairisha sembuse TFF? Its happen man most of the time for good reason.

  Shamba la bibi halitoi fursa watu wengi kuona soka na mambo ya kufika uwanjani saa nne kuwahi nafasi yamepitwa na wakati baada ya kuzindua uwanja mkubwa labda wasimamizi wapunguze gharama za uwanja mkubwa ili tupate fursa watu wengi kuona soka.

  El Maamry ni maoni yake na haina maana yeye ndio mtoa haki mbona CAF ambayo yeye ni mjumbe wameshindwa hata kuguswa na msiba uliowapata Togo badala yake kuwafungia na jana Adebayor ameamua kuachana na mipira ya kiafrika
   
 4. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  TFF ni wababishaji..period..Wako kimaslahi zaidi,hilo shamba la bibi mbona tumechezea miaka nenda rudi hakuna maafa yaliyotokea bana,mbona mechi nyingine za ligi zachezewa pale..Tatizo hapa ni tamaa za TFF,Simba na Yanga walikubaliana mechi ichezwe shamba la Bibi...Yaani ligi isogezwe mbele eti tu kwa sababu Simba na Yanga inatakiwa ihudhuriwe na watu wengi!!my foot!..After all,FA Japo huahirisha mechi lakini Ligi huisha kwa wakati ule ule uliopangwa(na hawaahirishi kwa sababu eti wanataka watu wengin wahudhurie mechi fulani)...TFF ni wababaishaji tu..Pia wanyonyaji wakubwa..Full Stop
   
Loading...