Kwenu TANROADS kwa ajali hizi mnapaswa kuwajibishwa

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,854
35,860
Hiki ni kipande cha barabara 90km kati ya Rusahunga na Rusumo. Kumekuwa na nyuzi nyingi miaka nenda rudi. Bado hali ni mbaya na yaonekana yote wamekuwa yanaangukia kwenye masikio viziwi.

Katika picha ni sampuli tu ya visa katika barabara hii kuu.

Pana sehemu inaitwa Nyabugombe (Biharamulo) yakiwapo manyunyu tu kwa mashimo na utelezi uliopo hapo basi barabara ndiyo inakuwa hakuna tena.

Jana pia magari kibao yamelala hapo kwa kimvua cha rashasha tu kilichopita.

Hii ni barabara kuu. Hali kama hii ni aibu kubwa. Mpaka wafe wangapi? Sehemu yenu ya uwajibikaji nyie kama serikali iko wapi? Mbona kodi zote mnachukua tena kwa deadlines zenu na kama mtakavyo nyie? Hivi ile tume ya FCC kuhusu usawa na uwajibikaji katika mikataba nanyi inawahusu? Au ile ni mkuki tu kwa nguruwe?

Mpaka wafe wangapi ndipo mgutuke tokea usingizini mnamoonekana kuwamo?

IMG_20200119_185459.jpg
IMG_20200109_115731.jpg
 
Kwa shinikizo zao, tumekubali. Tutakutana nao ana kwa ana kunako ballot boxes. Si ni mwaka huu huu? Stay tuned.
 
Ni maneno ya wapiga kura kila uchaguzi ukikaribia. Tutakutana kwenye sanduku la kura..kura mtapiga lkn mambo ni yale yale hakuna mnachoweza kubadili.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hii ni ajali nyingine njiani. Hili lorry limetereza liko njia moja kwenda. Tupo wengi ambao huwa hatususii kwa sake ya kususia halafu pasi na sababu za msingi tunadai hatususii tena. Tutakula nao sahani moja yapo mengi ambayo wao wanajifanya viziwi.
IMG_20200121_095329.jpg
IMG_20200121_095334.jpg
IMG_20200121_095334.jpg
IMG_20200121_095349.jpg
IMG_20200121_095329.jpg
IMG_20200121_095349.jpg
 
Wakati kwa wenzetu kunajengwa daraja la salenda kupendezesha jiji. Kwingine hali ni kama ajali Kila leo sababu ubovu wa barabara usioangaziwa macho.
 
Wakati kwa wenzetu kunajengwa daraja la salenda kupendezesha jiji. Kwingine hali ni kama ajali Kila leo sababu ubovu wa barabara usioangaziwa macho.
 
Wakati kwa wenzetu kunajengwa daraja la salenda kupendezesha jiji. Kwingine hali ni kama hii ambayo ajali ni kila leo sababu tu ya ubovu wa barabara usioangaziwa macho.

IMG_20200127_092640.jpg

IMG_20200127_092643.jpg
 
Back
Top Bottom