Kwenu ndg zangu waislam

Kwenu ndg zangu waislam

Ushasema India siyo Tanzania, kwanza hata huu utamaduni wanaoenda nao waislm ni wakiarabu kwasababu waarabu wao wanaoana wao kwa wao hivy hawaoni hasara hata wakimpa msichana bure muoaji kwani wanaamini ni ndg

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona wakristo wameshindwa kufanya wepesi kama wenzio ili nao waoane wenyewe kwa wenyewe tu kama bure?

Mi navyojua dini zote hazifurahii kuona mtu anahama dini yao kwenda kwenye dini ingine kwa kigezo cha ndoa

Hata wakristo hawafurahishwi kuona mkristo kabadili dini kua muislam

Lakini kwenye ishu ya mali waislamu wamejitahidi kulegeza kamba kisela, kwa mkristo hata uende kuoa mtoto wa askofu lakini kupeleka biblia kama ni kielelezo cha mali utaonekana umewadharau sana
 
Mbona wakristo wameshindwa kufanya wepesi kama wenzio ili nao waoane wenyewe kwa wenyewe tu kama bure?

Mi navyojua dini zote hazifurahii kuona mtu anahama dini yao kwenda kwenye dini ingine kwa kigezo cha dini

Hata wakristo hawafurahishwi kuona mkristo kabadili dini kua muislam

Lakini kwenye ishu ya mali waislamu wamejitahidi kulegeza kamba kisela, kwa mkristo hata uende kuoa mtoto wa askofu lakini kupeleka biblia kama ni kielelezo cha mali utaonekana umewadharau sana
Haya bhana hapa sina hoja ila waambie wapunguze kulialia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa anaongelea laki mbili mbona kubwa hivyo! mahari elfu 30,000 tu inatosha. baada ya miezi 10 hivi ndoa hakuna, kila mtu anakwenda kuoa mwingine kuolewa!.
 
Kwanza sioni umuhimu wa mahari hawa wazee wanatuibia

Kama walipata tabu kukuza binti hata wanaume wazazi wao walipata tabu kuwakuza nao wanaitaji pongeza

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata mimi nakubaliana na wewe katika hili siku hizi mahari haina maana yoyote. Mahari ilikuwa na maana zamani na hasa mahari ya kweli ilikuwa inatolewa mfano uchaggani na/au uhayani.

Kule ilikuwa inapelekwa zaidi zaidi pombe alafu mkishakubaliwa mnainywa wenyewe kwa pamoja na wenyeji, kisha mnarudishiwa madumu yenu matupu mnaondoka.

Siku hiyo ya mahari ilikuwa kama siku ya wazee wa pande mbili kufahamiana (get together flani). Siku hizi ujanja ujanja umekuwa mwingi nao wanatozana pesa nyingi, utafikiri wanauza binti yao.

Ndiyo maana hata heshima ya ukwe/mkwe imepungua sana kama siyo kuisha kabisa. Zamani mkwe alikuwa mkwe kweli kweli siyo haya ya siku hizi ambapo baba/mama mkwe analewa pamoja mke/mme wa mtoto wake kisha wakishalewa wanakokotana kwenda nyumbani. Hakuna heshima kabisaa.

Sasa mtu unamtoza mamillioni ya pesa eti mahari, mwisho wa siku anaichukulia kama biashara nyingine kama vile kanunua gari showroom ataanzia wapi kukuheshimu kama mkwe??
 
Kama wewe kweli ni.mwanaume basi uko na shida mahali kama sio brain yako ina shida basi jinsia yako iko na shida.. mwanaume rijali

Hapana mkuu nimtazamo tuu pia ukiona mambo bado nibora ukajipanga na siyo kulialia
 
Hata mimi nakubaliana na wewe katika hili siku hizi mahari haina maana yoyote. Mahari ilikuwa na maana zamani na hasa mahari ya kweli ilikuwa inatolewa mfano uchaggani na/au uhayani.

Kule ilikuwa inapelekwa zaidi zaidi pombe alafu mkishakubaliwa mnainywa wenyewe kwa pamoja na wenyeji, kisha mnarudishiwa madumu yenu matupu mnaondoka.

Siku hiyo ya mahari ilikuwa kama siku ya wazee wa pande mbili kufahamiana (get together flani). Siku hizi ujanja ujanja umekuwa mwingi nao wanatozana pesa nyingi, utafikiri wanauza binti yao.

Ndiyo maana hata heshima ya ukwe/mkwe imepungua sana kama siyo kuisha kabisa. Zamani mkwe alikuwa mkwe kweli kweli siyo haya ya siku hizi ambapo baba/mama mkwe analewa pamoja mke/mme wa mtoto wake kisha wakishalewa wanakokotana kwenda nyumbani. Hakuna heshima kabisaa.

Sasa mtu unamtoza mamillioni ya pesa eti mahari, mwisho wa siku anaichukulia kama biashara nyingine kama vile kanunua gari showroom ataanzia wapi kukuheshimu kama mkwe??
Ukishashatambua thamani ya mwanamke hautafikira hayo uliyoyaandika

Kama hela ipo owa kama huna endelea kusugua banch la ubachela na siyo kulialia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe kama hutaki kuolewa kwa hiyo laki 2 ni juu yako,sisi haituhusu kitu,acha kuzunguka eti umesikia watu wakiongea,hivi ni nani aliyekuaminisha kua thamani ya mwanamke inapimwa kwa mahari? kama huyo mumeo mtarajiwa hataki kukuongeza hiyo mahari inamuhusu yeye na wewe na sio kuingiza na kulaumu dini yote,mahari ni mapatano na sio bei kama bei ya vitu dukani.
 
Back
Top Bottom