Tanganyika jeki
JF-Expert Member
- Jun 12, 2011
- 243
- 87
CHADEMA imepata uungwaji mkono mkubwa toka kwa umma wa Tanzania kwa miaka ya hivi karibuni. Hali hiyo imeenda sambamba na kuporomoka kwa kasi kwa chama tawala, CCM.
Chadema kimetumia udhaifu wa serikali na chama tawala kujiongezea wanachama na wafuasi wengi. Ubadhirifu wa mali ya umma, utoroshaji na usimamizi mbovu wa raslimali za umma, matumizi mabaya ya ofisi, upendeleo na ufisadi kwa jumla vimekuwa mtaji wa Chadema. Haya yote yanatokana na SABABU MOJA KUU - UONGOZI MBOVU na MFUMO MBOVU wa kutafuta viongozi.
1. Je, Chadema ina sera, kanuni na mikakati gani za kuwapata na kuandaa viongozi bora waadilifu, wenye tija na wazalendo?
2. Ni njia zipi na taratibu mnazo za kuongoza michakato ya kuwapata viongozi wa chama na wagombea uongozi katika ngazi mbalimbali za taifa?
3. Je, Zitto na shibuda wapo sahihi kutangaza nia ya kugombea urais kwenye majukwaa nje ya chadema' yaani bungeni na kwenye mkutano wa ccm?
4. Je, mmeweka wazi - ili jamii ijue - sifa, muda na taratibu za kumpata mgombea urais?
5. Je, ni sahihi kwa mwanachama wa chadema kutengenea mtandao unaojumuisha wanachadema wenzie, wanachama wa vyama vingine na makundi mengine ya kijamii kwa kwa ajili urais.
6. Je, chama ni imara kwa kiwango gani kiuongozi kupambana na propaganda, usaliti,hila na siasa chafu na za kibaguzi za ccm, serikali? Na mwisho
7. Je, ni vizuri kwa mwanachama akawa na nguvu kuliko chama? Chadema inafanya nini kujenga chama-taasisi kinachofikika na kuwafikia watanzani wote kiurahisi?
Asante!