Kwenu Dr. W. Slaa, Zitto Kabwe, John Mnyika na viongozi wa Chadema mliopo JF

Tanganyika jeki

JF-Expert Member
Jun 12, 2011
243
87
CHADEMA imepata uungwaji mkono mkubwa toka kwa umma wa Tanzania kwa miaka ya hivi karibuni. Hali hiyo imeenda sambamba na kuporomoka kwa kasi kwa chama tawala, CCM.

Chadema kimetumia udhaifu wa serikali na chama tawala kujiongezea wanachama na wafuasi wengi. Ubadhirifu wa mali ya umma, utoroshaji na usimamizi mbovu wa raslimali za umma, matumizi mabaya ya ofisi, upendeleo na ufisadi kwa jumla vimekuwa mtaji wa Chadema. Haya yote yanatokana na SABABU MOJA KUU - UONGOZI MBOVU na MFUMO MBOVU wa kutafuta viongozi.

1. Je, Chadema ina sera, kanuni na mikakati gani za kuwapata na kuandaa viongozi bora waadilifu, wenye tija na wazalendo?

2. Ni njia zipi na taratibu mnazo za kuongoza michakato ya kuwapata viongozi wa chama na wagombea uongozi katika ngazi mbalimbali za taifa?

3. Je, Zitto na shibuda wapo sahihi kutangaza nia ya kugombea urais kwenye majukwaa nje ya chadema' yaani bungeni na kwenye mkutano wa ccm?

4. Je, mmeweka wazi - ili jamii ijue - sifa, muda na taratibu za kumpata mgombea urais?

5. Je, ni sahihi kwa mwanachama wa chadema kutengenea mtandao unaojumuisha wanachadema wenzie, wanachama wa vyama vingine na makundi mengine ya kijamii kwa kwa ajili urais.

6. Je, chama ni imara kwa kiwango gani kiuongozi kupambana na propaganda, usaliti,hila na siasa chafu na za kibaguzi za ccm, serikali? Na mwisho

7. Je, ni vizuri kwa mwanachama akawa na nguvu kuliko chama? Chadema inafanya nini kujenga chama-taasisi kinachofikika na kuwafikia watanzani wote kiurahisi?

Asante!
 
Hoja nzuri ingawa haijazingatia taaluma ya uandishi i.e no para.....
 
Yote hayo yameelezwa kwenye document za chama na zinapatikana kwenye website yao pamoja na pale makao makuu ya Chama. Mkuu punguza uvivu kidogo kupitia kabla ya kushobokea na maswali ya kimagamba hapa jamvini
 
Chadema si mali ya mtu mmoja bali ni chama cha watanzania na wanachadema,Kinawasomi na watu wenye fikra pevu na wenye kukubali kujifunza na kushaurika toka katika jamii ya watanzania wote bila kujali dini,kabila, rika wala kipato,Watalifanyia kazi wazo lako ni zuri.:flypig:
 
Tanganyika Jeki hebu Edit kidogo hiyo hoja ni nzuri...unatupa taabu kuisoma
 
Chadema imepata uungwaji mkono mkubwa toka kwa umma wa Tanzania kwa miaka ya hivi karibuni. Hali hiyo imeenda sambamba na kuporomoka kwa kasi kwa chama tawala, CCM. Chadema kimetumia udhaifu wa serikali na chama tawala kujiongezea wanachama na wafuasi wengi. Ubadhirifu wa mali ya umma, utoroshaji na usimamizi mbovu wa raslimali za umma, matumizi mabaya ya ofisi, upendeleo na ufisadi kwa jumla vimekuwa mtaji wa Chadema. Haya yote yanatokana na SABABU MOJA KUU - UONGOZI MBOVU na MfUMO MBOVU wa kutafuta viongozi. 1. Je, Chadema ina sera, kanuni na mikakati gani za kuwapata na kuandaa viongozi bora waadilifu, wenye tija na wazalendo? 2. Ni njia zipi na taratibu mnazo za kuongoza michakato ya kuwapata viongozi wa chama na wagombea uongozi katika ngazi mbalimbali za taifa?3....

Mkubwa weka paragraphs bandiko lako lisomeke vizuri.
 
Mkuu labda tuelimishane. Natumia cm nokia E63. Nimejaribu kuruka 'space' kwa ajili ya paragraph lakini wapi?
Pole sana mkuu lakini nimekusoma vema hofu kwa wanajamvi wengine... ukitulia uta edit unless otherwise well done kamanda.
 
Ama kweli ZZK ni zaidi ya CHADOMO yaan anawashughulisha vibaya na wakimchachawangwe CHADOMO kwishney
 
Kinachotokea sasa hv CDM ni matokeo ya siasa za makundi na kukosekana kwa maamuzi ya busara kwa viongozi wake.
 
Ama kweli ZZK ni zaidi ya CHADOMO yaan anawashughulisha vibaya na wakimchachawangwe CHADOMO kwishney
Nadhani hujanielewa. Pole. Na tafadhali usikariri. Tatizo langu ni vyama hivi kutekwa na mtu au watu wachache na kuvitumia kwa maslahi binafsi. Vyama vya siasa vinatakiwa kuwa taasisi imara. Nadhani ulifuatilia ya malema na anc. Anc ilidhihirisha ni taasisi imara. Unukumbuka mrema na vyama vyake? Iangalie ccm inayotekwa.
 
napata tabu sana kufikiria nani atachaguliwa kugombea nafasi ya uras kupitia chadema nikiwaza naogopa kwani kuna uwezekano mkubwa kukatokea mpasuko wa ajbu sana ndani ya chama ikiwemi vibaraka walijipenyeza katika kukivuruga. binafsi naona mazingira magumu kwa kiasi fulani inabidi tuongozwe sio na akili tu bali busara na hekima katika kufanya maamuzi la sivyo chama kinaonekana kinaweza kunyemelewa na ukabila na udini wa kutengenezwa katika kutuvuruga.
sina wasiwasi na kuongeza viti vya ubunge na udiwani ambayo mimi binafsi napenda vyama vya upinzani vijikite zaidi sehemu hii ili jamii iweze kuwaamini na kuwakubali kwa karibu zaidi hasa waishio vijijini.
hivyo bado muda tunao tusipaparuke kwa nafasi hii na kutukasahau wajibu wetu wa kujenga uaminifu kwa wanachi
 
Kinachotokea sasa hv CDM ni matokeo ya siasa za makundi na kukosekana kwa maamuzi ya busara kwa viongozi wake.
Mkuu sina hakika na suala busara viongozi kwa sababu sina ushahidi wa kutosha ila unajua vyama vingi vya siasa vinaiga katiba, kanuni, mikakati na utamaduni wa hv vyama vikongwe. Sasa siasa makundi wasipoangalia zitaigwa na kuimaliza chadema
 
Wahusika nadhani wametoka humu nadhani wakirudi watatupa majibu ya hizo hoja kama kweli wanajua wanachotaka kulifanyia taifa hili. Tuwasubiri warudi na majibu
 
Kwa afya ya chama watu domo kaya km zitto inabidi wawepo tu kwani tuna mbinu nyingi za kuwadhibiti wasiharibu upinzani km walivyofanya zamani akina wasira na wengine.....
 
Back
Top Bottom