Kwenu bodi ya mikopo [heslb]

Natafuta kiki

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
911
1,284
Poleni na majukumu ya kujenga taifa: Sisi wanafunzi tuliosoma Chuo kikuu cha Sekomu kilichopo Lushoto Tanga tuliomaliza mwaka 2015; tunayo masikitiko makubwa kwa tuliyofanyiwa na nyinyi bodi pamoja na chuo cha Sekomu.

1. Mwaka wa masomo 2013/2014 na mwaka wa masomo 2014/2015 bodi mlitukata hela ya ada kwa wanafunzi wote bila sababu. Tukamtuma kiongozi wetu yaani waziri wa mikopo kufuatilia jambo hilo na tunashukuru mlimpa majibu kuwa mtarudisha hizo fedha za ada kwa miaka yote miwili.

2. Kwa miaka yote hiyo sisi wanafunzi tuliendelea kulipa ada mliyotukata bila sababu na tunamshukuru Mungu alituwezesha tukamaliza madeni yote.

3. Mwaka 2015 mwezi July tulihitimisha/ kumaliza masomo yetu kwa ngazi ya shahada ya kwanza.
Baada ya sisi kuondoka mwezi Octoba tukapewa taarifa kuwa mmerejesha fedha mlizokata. Hivyo chuo kikabandika majina ya wanafunzi wote waliorejeshewa hizo fedha na kututaka twende chuoni kurudishiwa fedha kwani ada tulikuwa tumemaliza na kufanya UE.

Kwa kuwa tulikuwa tunatokea sehemu mbalimbali za Tanzania kila mtu alikuwa anaenda kwa wakati wake chuoni kuitikia wito.

Cha ajabu tulipokwenda chuo kikaanza kutupa sababu zisizoeleweka mfano chuo hakina fedha kwa sasa; wengine wakienda wanaambiwa leteni risiti zote za kila muhula ili hali hawakuwaambia waende na risiti; hata kama risiti mtu hana mfumo wa malipo ulikuwa unafanyika au kuhifadhiwa kwenye system yaani mfumo wa computer. Hivyo ilikuwa rahisi tu kucklik jina data zote zinajionyesha.

Wamefanya hivyo mara nyingi na kutuzungusha kiasi kwamba mtu anatumia nauli kwenda na kurudi mfano kutoka Mtwara to Tanga au Mbeya to Tanga tumepoteza nauli zetu bila mafanikio. Hata tulipopeleka risiti kama walivyotaka bado wakatuambia chuo hakina fedha.

OMBI KWENU BODI YA MIKOPO:

1. Tunaomba mfuatilie hizo hela mlizorudisha zilitumikaje maana wahusika wahakusaini popote kama zimepokelewa.

2. Kwa kuwa hela zipo Sekomu na hawataki kuwarudishia wahusika waambieni warudishe huko bodi ili mtupunguzie deni maana deni ni kubwa.

3. Hatua stahiki za kinidhamu kwa wote waliohusika zichukuliwe kwani huu nao ni ufisadi na uhujumu uchumi wa nchi.

Nawatakia kazi njema.

N. B
Hili suala tumefuatilia kutoka mwaka 2015 hadi kufikia leo bila mafanikio hivyo tumeamua kuwapa taarifa ili mtusaidie kwani baadhi wameajiriwa mnawakata fedha ambazo hakuzitumia toka kwenu.
 
Sasa msomI shida hapo sio Bodi shida ni chuo ulichosoma ndugu....
Pambanani chuo kiwarudishie hela..
Hilo deni bora hata msingeomba maana lina kuwa zaidi ya uyoga
 
Sasa msomI shida hapo sio Bodi shida ni chuo ulichosoma ndugu....
Pambanani chuo kiwarudishie hela..
Hilo deni bora hata msingeomba maana lina kuwa zaidi ya uyoga
Umeandika UFALA.
Wangesomaje sasa bila mkopo wa bodi. Unadhani kila mtu anaweza kujilipia mamilioni ya pesa za ada na kujikimu.
 
Back
Top Bottom