Kwenda Zanzibar sasa lazima uwe na Kitambulisho, Cha Makazi, kura au cha uraia

Kwa utunzaji wa kumbukumbu ni utaratibu mzuri,lakini kinachosikitisha ni kuamua kuanza ghafla bila
taarifa,utaratibu huu umesumbua sana watu jana waliotaka kusafiri ZNZ,ghafla unafika kukata tiketi
unaambiwa bila kitambulisho hakuna tiketi,kwa nini wasingetangazia watu mapema ili waende na vitambulisho?
au ndo kama kawaida ya Tanzania kila kitu kinafanywa kama zoezi la zima moto!!!!!
 
Mkuu Nonda nimekuelewa, lakini ninayo maswali mawili madogo ya nyongeza

1. Je utaratibu huu pia unawahusu Wasafiri/raia wanaosafiri kutoka Zanzibar kuja Tanganyika?

2. Kwa kuwa hili Tangazo limetolewa na SUMATRA je sheria/utaratibu huu unahusu usafiri wote wa majini? eg Unguja na Pemba and vice versa, Mwanza na Bukoba and virse versa, DSM na Mafia and vice versa na kule Lake Tanganyika na Lake Nyasa?

Nitashukuru kama nitapata ufafannuzi wako.

Bobuk

Pitia post #12 Ipo link ya makala inayotoa habari/taarifa na maoni ya mwandishi pia yamechanganyika humo.

Kwa bahati iliyoje, mimi si msemaji wa hizo mamlaka ziliripotiwa na mleta mada wala mamlaka iliyoripotiwa katika hiyo link. Ukiingia link utapata baadhi ya majibu unayoyahitaji mkuu.

Maswali ambayo hutapata majibu yake yaelekeze kwa mamlaka husika ili upate majibu sahihi.

Mimi binafsi, naona ni utaratibu mzuri wa kuhifadhi kumbukumbu ya idadi ya wasafiri na taarifa zao. Ni jambo zuri ikitokea dharura kuwezesha kutambulikana kwa urahisi.
 
Mimi naomba kuuliza tu hivi ukiwa Uingereza na ukitaka kwenda Ireland pale kwenye ferry yao kuna huu upuuzi wa vitambulisho? Na je hapa kwetu ukikata tiketi ya hivi vindege vya Coastal unaulizwa vitambulisho?

Nawashauri Watanganyika wote ambao wanapenda kutembelea hiyo nchi ya kipuuzi Zanzibar ni bora wawe wanatumia usafiri wa ndege za chater maana inaonekana dhahiri sasa usafiri wa bahari ndio kaburi lenu hivyo wanataka wawatambuwe vizuri?

Wacha ujinga wewe kama hujui uliza wenzako.watanganyika ni washamba kweli hebu tembeeni mujifunze kama wenzenu wa visiwani wanavotembea.
 
source majira

mamlaka ya usafirishaji wa majini na nchi kavu sumatra imetangaza kuwa kwa raia yeyote anayetaka kwenda zanzibar ni lazima awe na kitambulisho ama cha makazi, cha mkazi au kura ili upewe tiketi ya kusafiria kwenda zanzibar.
mbona ghafla....nahisi kuna jambo hapa......
 
Kwa utunzaji wa kumbukumbu ni utaratibu mzuri,lakini kinachosikitisha ni kuamua kuanza ghafla bila
taarifa,utaratibu huu umesumbua sana watu jana waliotaka kusafiri ZNZ,ghafla unafika kukata tiketi
unaambiwa bila kitambulisho hakuna tiketi,kwa nini wasingetangazia watu mapema ili waende na vitambulisho?
au ndo kama kawaida ya Tanzania kila kitu kinafanywa kama zoezi la zima moto!!!!!

Tangazo lilitolewa,mimi nilisoma ktk magazeti,lakini kama kawaida Watanzania wengi tunasoma udaku na kusikiliza miziki ya mipasho!
 
Wacha ujinga wewe kama hujui uliza wenzako.watanganyika ni washamba kweli hebu tembeeni mujifunze kama wenzenu wa visiwani wanavotembea.
Wewe kuwadi wa Sultani unataka kusema nini!! Wapemba wanatembea wapi?
 
Ni utaratibu mzuri sana. Ila kwa nini wanaacha mpaka janga linatokea ndio wanatilia mkazo?

Jana nimeona kwenye TV inaelezwa kuwa kumbe ni utaratibu unaopaswa kufuatwa na wasafirishaji. Lakini wao walikuwa hawafuati na mamlaka inayohusika ikawa imepumzika tu bila kuchukua hatua.

Mpaka Watanzania wafe ndio wanaanza kufungua makabrasha ya taratibu za uendeshaji. Wake up serikali ya Tanzania.
 
kutoka zenji kuja huku Wapemba wote wanaoleta bidhaa zao pale kariakoo wao itakuaje?

Yaani hii Tanganyika sio tu tunatawaliwa na makaburu na wazungu kutoka Ulaya bali tunatawaliwa mpaka na wapemba duuhh!
 
any way, si shida kwani hata bank huwezi chukua pesa zako bila kitambulisho. Hata wakitaka twende kwa passport poa tu wasisahau kuweka na Duty free shops kwa wageni na hasa Watanganyika.

Tatizo ni muda kuanzia kutangazwa kwa hitajio hilo na utekelezaji.
Hapo penye wekundu umeongopa ,huenda benki ya poasta ndio unafanya hivyo,unachotakiwa pale benki nikuandika account yako,kwani kwenye kompyuta pana picha zako ,na taarifa zote.pia huo utaratibu una kasoro kwani TZ hatuna official vitambulisho,hata hivyo vya kura sio kila mtu anavyo.hebu fikiria usiku unapigiwa simu usiku na kuambiwa kuna msiba unaokuhusu huko Zanzibar na ni siku ya jumapili ,wewe huna kitambulisho chochote na hata serikali za mitaa zimefungwa utafanyaje.Mi nadhani mambo yote haya yanatokana na Zanzibar si Tanzania,si watumie utaratibu wa kwenye mabasi ,abiria waandikwa majina kwenye register maalumu.Jamani hawa wazanzibar hawaishi hila ,bora kieleweke tu kuwa sasa basi
 
Kwani unaweza kuchukua pesa bila card? ile card sio kitambulisho?

Hapa napiga TZ 11 kwenda bank kuchukua kuchukua fedha zangu bila kuwa na utambulisho wowote.
 
15th August 2012

Mamia ya Watanganyika waliotarajiwa kusafiri jana kwenda visiwani Zanzibar, jana walikwama kuondoka kutokana na utaratibu mpya wa vitambulisho unaodaiwa kutolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini Nchini (Sumatra).

Kwa mujibu wa utaratibu, Mtanganyika haruhusiwi kukata tiketi ya kusafiri kwenda visiwani humo iwapo hatakuwa na kitambulisho, kikiwamo cha uraia.

Vitambulisho vingine ambavyo Mtanganyika anatakiwa kuwa na kimojawapo, ni pamoja na cha makazi, kupiga kura, kazi, leseni ya dereva, utambulisho kutoka serikalini au pasi ya kusafiria.

Baadhi ya WaTanganyika waliokwama kusafiri, walisema wamechelewa kupata taarifa hizo kwa kuwa hawaujasikia utaratibu huo katika chombo chochote cha habari.

Utaratibu huo ambao maelezo yake yamebandikwa kwenye kuta za ofisi za kukatia tiketi katika bandari za meli zinazokwenda visiwani humo, umeelezwa kuwa ulianza kutumika rasmi Agosti 13, mwaka huu.

Happy Eid to everymember of JF from Mwiba.
 
Mnaenda kufanya nini huko? Tanganyika yenyewe kubwa na iko less populated (though economically overpopulated because of unequal distribution of natural resources) mnakazana kwenda kisiwani? I'm sure we can live and do without Zanzibar!
 
Mnaenda kufanya nini huko? Tanganyika yenyewe kubwa na iko less populated (though economically overpopulated because of unequal distribution of natural resources) mnakazana kwenda kisiwani? I'm sure we call live and do without Zanzibar!
Bila ya Zanzibar Tanganyika itasambaratika ,au hilo hamlioni ?
 
Hizi ni sheria za usalama. Ni mara mbili katuika kipindi cha mwaka mmoja meli zimezama na kuna abiria kadhaa ambao maiti zao hazijapatikana hadi leo. Nchi yoyote ile lazima iwe na utaratibu wa usafiri lakini kwetu uzembe ndio uliotawala usafiri kwa muda mrefu. Hili la kudhibiti watu ni kwa masalahi ya abiria wenyewe. Vinginevo ni propaganda.
 
Back
Top Bottom