Kwenda Zanzibar sasa lazima uwe na Kitambulisho, Cha Makazi, kura au cha uraia

Sasa hawa wanaofunga mipaka inakuwaje ? Au ndio na wao wanataka na wameanza kuuvunja Muungano ,unapodai pasi ,bila ya shaka utakuwa unakwenda nchi nyingine ,je mmepaona hapo ,mbona kule Mwanza unaposafiri kwenda Nansio Ukerewe hutakiwi kuwa na makaburasha yote hayo ? WaBara mnafunga mipaka kinyemela ! hili jambo liwepo kwenye wasafiri wa treni au garimoshi na hata wale wa mabasi maana wengine huvurugika mpaka nyuso.
 
Huo ni utaratibu ulioko dunia nzima na inasaidia kupunguza ulanguzi wa tiketi na kuweza na pia usalama katika kipindi hiki ambapo ugaidi umeshamiri duniani kote.
 
Huo ni utaratibu ulioko dunia nzima na inasaidia kupunguza ulanguzi wa tiketi na kuweza na pia usalama katika kipindi hiki ambapo ugaidi umeshamiri duniani kote.

Haiwezekani ikawa dunia nzima ,au sisi waTz hatumo humo duniani ? bro inasemwa hii ndani ya Nchi moja ya Tanzania ,hapa passport imehusu nini ,ukitilia maanani pale gatini DSM kuna ukwapuaji wa hali ya juu ,huoni kama pasi zitakuwa zikiibiwa na kuchomolewa kila siku, sidhani kama suala la vitambulisho ni muhimu ,ikiwa hawa sumatra watajipanga na huku wakijua chombo kinabeba watu kumi basi wao ndio wa kuhakikisha tiketi walizokusanya ni kumi na zenye majina waliomo ndani ya chombo ni kumi.

Hili la pasi ni katika juhudi za kufunga mipaka.
 
..bora utaratibu wa passport urudishwe.

..lakini iwe kwa pande zote za muungano.
 
Mimi naona ni jambo jema maana nchi inatakiwa kuwa hivyo, siyo watu kuingia kisiwani kama wanakwenda kwenye bar
 
zanzibar unaenda kufanya nini? labda kujifunza uchawi wa kipemba na other wizardly arabic rituals.
 
Sasa hawa wanaofunga mipaka inakuwaje ? Au ndio na wao wanataka na wameanza kuuvunja Muungano ,unapodai pasi ,bila ya shaka utakuwa unakwenda nchi nyingine ,je mmepaona hapo ,mbona kule Mwanza unaposafiri kwenda Nansio Ukerewe hutakiwi kuwa na makaburasha yote hayo ? WaBara mnafunga mipaka kinyemela ! hili jambo liwepo kwenye wasafiri wa treni au garimoshi na hata wale wa mabasi maana wengine huvurugika mpaka nyuso.

Lazima uwe na kitambulisho cha ukaazi ,kupigia kura au passport,sijaelewa ina maana mtu ambaye si mkazi wa znz na ambae hana kitambulisho cha kupigia kura lkn anacho cha mwajiri mfano halmashauri ya wilaya hana ruksa ya kwenda znz na kuja bara,je watanzania wote wanavitambulisho vya kura na ukazi? Kwa tanzania paspoti ni anasa je hii si ndio mwanzo wa kuvunja muungano? Hivi hii nchi huwa tunaamuliwa mambo au tunaamua wenyewe? Ili upate kitambulisho cha ukazi ni lazima uwe mkazi wa znz na hata wengine huko wamenyimwa vyote cha kura na ukazi je wao ndio mwisho wao wa kusafiri?
 
zanzibar sijui huwa wanaringia nini sijaona kabisa,kwanza kifo kiko njenje niende kufanyanini?
 
..bora utaratibu wa passport urudishwe.

..lakini iwe kwa pande zote za muungano.
China na Hong kong wana utaratibu unaoupendekeza.

There's a border between Hong Kong and Mainland China and each side administers separate immigration controls; Hong Kong is part of China but crossing the border is like traveling from one country to another for immigration purposes. Thus, if you arrive in Hong Kong and want to visit the Mainland, you'll need a Chinese visa when you cross to the Mainland, though you can return to Hong Kong visa-free. And if you start on the Mainland, visit Hong Kong, then return to the Mainland, you'll need a new (or double/multiple entry) Chinese visa to re-enter the Mainland.

Link
Hong Kong and Macau FAQs - Lonely Planet travel forum

Difference Between Hong Kong and China | Difference Between | Hong Kong vs China
 
zanzibar sijui huwa wanaringia nini sijaona kabisa,kwanza kifo kiko njenje niende kufanyanini?
Chameli

Sifikiri kuwa wanaringa au wanaringia kitu. Mimi naona wamejawa na hofu ya kumezwa na Tanganyika tu.

Kwa bahati mbaya, Tz haina watawala wazuri. Zanzibar ni brand name kama ulivyo Mlima Kilimanjaro na mbuga zetu.
Tungeweza kuinyanyua na kuifanya Zanzibar kuwa "gate way" to Tanzania.

Lakini unajua nini kinaendelea katika nchi hii, si madini,si mbuga, si bahari ,si utalii, si kilimo, si ardhi..nada nada.

Kitu pekee ambayo ni maarufu ni ubinafsi usio kikomo,ufisadi na rushwa.

Tunasema Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, kwa maana ipi? We "screw" Zanzibar kama tunavyo "screw" Mafia na kila kitu chetu.

So sad!!! Usanii wa serikali yetu ndio unajenga hizi chuki sasa.
 
..bora utaratibu wa passport urudishwe.
..lakini iwe kwa pande zote za muungano.
Mkubwa, si umesikia kitambulisho tu watu wanahaha mpaka umefungwa! kuvunja je! Unafikiri serikali 3 au mkataba ni kuhusu nini! Umesikia wimbo wa taifa, bendera na kiti UN, umeshawahi sikia passport!
This is just a prelude
 
Nadhani ni vema kuwa na vitamburisho.
Wazanzibar pia wanahitaji vitamburisho kuja kwetu Tanganyika au ni sisi tukienda kwao?
Ni vema hata katika Mabasi ya Mikoani tungekuwa tunatoa vitaburisho,
Just in case, watu wote waliokuwemo ndani ya basi wanajulikana ni akina nani.
 
Zanzibar ni eneo dogo na kuna semi-autonomy state. Usipoweka control visiwa vile vitajazana kila aina ya watu
 
Kile kinachoonekana muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar haupo kivitendo bali kwenye maandishi na midomo ya viongozi wa nchi inaendelea kudhihilika kwa kasi kubwa.

Sasa wakazi wa inayoitwa Tanzania bara aka Tanganyika kwa raia wanaotoka Tanganyika kuishi Zanzibar ni lazima kuwa na vitambulisho ambavyo vinatolewa na serikali ya Zanzibar ambavyo raia wengine wa nchi nyingine hupewa kama vile Kenya, Uganda Au mgeni yoyote aingiapo Zanzibar kuwatofautisha Wanzibar na Watanganyika au Wakenya.

Sasa kwa mpango huu Vitambulisho vya Utanzania naona havina maana tutafute vya Tanganyika
 
Hawa wazanzibar tumewakoloni vya kutosha. Tuwapeni uhuru wao sasa. Otherwise watatusumbua sana.
 
Back
Top Bottom