Kwenda Zanzibar sasa lazima uwe na Kitambulisho, Cha Makazi, kura au cha uraia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwenda Zanzibar sasa lazima uwe na Kitambulisho, Cha Makazi, kura au cha uraia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Return Of Undertaker, Aug 15, 2012.

 1. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,528
  Trophy Points: 280
  Source Majira

  Mamlaka ya usafirishaji wa majini na nchi kavu Sumatra imetangaza kuwa kwa raia yeyote anayetaka kwenda Zanzibar ni lazima awe na kitambulisho ama cha Makazi, cha mkazi au kura ili upewe tiketi ya kusafiria kwenda Zanzibar.
   
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  EWURA??? You sure about that?
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Ndo matumizi ya vitambulisho! au unataka kusema kuna dalili za ubaguzi? Vipi kuhusu wale wanaoishi Zanzibar, wakitaka kuja bara vitambulisho siyo lazima?
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Ni UWURA au SUMATRA? Huku ni kuchanganya habari jamani!!!!
   
 5. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,134
  Likes Received: 7,383
  Trophy Points: 280
  Yaani usafiri wake uko shakani kiasi cha kwamba lazima ubebe kitambulisho mfukoni ili ukizama watu wakaipoa maiti yako itambulike mapema.

  Pia ikizama basi register ya waliopata ajali iwepo.

  Nahisi hizi ndizo sababu, kama ndizo basi kazi ipo, yaani tunawaza kuzama tu badala ya kufikiria kuzuia
   
 6. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,375
  Likes Received: 3,139
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni kwa sababu zanzibar ni nchi kamili au kwa ajili ya usalama tu?
   
 7. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Duh! This country is full of wonders!
   
 8. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Je hii ni kwa raia wote (WAGENI) au ni kwa raia wa Tanganyika na Zanzibar tu. Je ni lini raia wa kigeni walikuwa na vitambulisho vya mkaazi au kupiga kura?. Je hii sheria ni one way traffic? Vipi kwa raia wanaotoka Zanzibar kuja Tanganyika?

  Hivi hawa Wazanzibari wakiweke hizi sheria za kipumbavu ndiyo ZANZIBAR ITAKUWA NCHI KWELI? Mimi nimechoka na UKENGE wa Wazanzibari bora hili limuungano LIVUNJIKE TU.

  Ninaomba wabunge wangu MAKINI wa CDM kesho Alhamisi kwenye kipindi cha Maswali na majibu cha papo kwa papo kwa Waziri mkuu, muulize swali hili PINDA. Mnyika, Msigwa Please Do us Tanganyikas a favour.
   
 9. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  natamani viongozi wangesema ukweli kuwa kinachohitajika ni passport. Wabara mtaisoma znz huru.
   
 10. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  both mkuu
   
 11. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,848
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Maumivu ya kichwa huanza poole pooole mungano kwa heri
   
 12. N

  Nonda JF-Expert Member

  #12
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Makala ipo hapa http://www.mwananchi.co.tz/habari/4-habari-za-kitaifa/25467-smz-yabadili-utaratibu-usafiri-majini

  Kaimu Mkurugenzi wa ZMA, Abdallah Hussein Kombo alipoulizwa jana kuhusu hatua hiyo alisema lengo lake ni kudhibiti abiria na kujua taarifa za watu wote wanaosafiri katika vyombo vya baharini.
  “Hakuna malengo zaidi ni hayo tu ya kudhibiti abiria na kujua ni nani wanasafiri,” alisema Mkurugenzi huyo.
   
 13. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mi naona ni utaratibu mzuri, Azam Marine walishaanza siku nyingi sana kuuza ticket kwa kitambulisho. hii inasaidia hata wale walanguzi wa ticket kupungua, maana walikuwa wanazinunua nyingi kiasi cha kuzimaliza zote na kuziuza mtaani kwa bei kubwa, kule zanzibar wanaitwa papasi hawa. kwa Bakhresa huna kitambulisho huna tikiti. Iendelee ivyo ivyo tu
   
 14. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #14
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,289
  Likes Received: 1,436
  Trophy Points: 280
  any way, si shida kwani hata bank huwezi chukua pesa zako bila kitambulisho. Hata wakitaka twende kwa passport poa tu wasisahau kuweka na Duty free shops kwa wageni na hasa Watanganyika.

  Tatizo ni muda kuanzia kutangazwa kwa hitajio hilo na utekelezaji.
   
 15. N

  Nonda JF-Expert Member

  #15
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Waraka huo umevitaja vitambulisho vinavyotakiwa kuwa ni kitambulisho cha Mzanzibari, leseni ya udereva, kadi ya benki, vitambulisho vya kazi, pasi ya kusafiria, barua ya Sheha na kadi za ZSSF/NSSF na Mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii.

  Nafikiri lengo ni kuhifadhi kumbukumbu za wasafiri na utambulisho wao.
  Ni orodha ya wasafiri. Hata unapokwenda kukata tiketi ya ndege, lazima utoe jina la msafiri na unapo-check in kabla ya kupata boarding pass ni lazima uoneshe kitambulisho, iwe ni National card au pasi ya kusafiria.

  Mleta mada/ taarifa ameileta kwa njia ya kutekenya watu tu.
   
 16. N

  Nonda JF-Expert Member

  #16
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Kuna wananchi walilalamika baada ya ajali ya boti. Walisema:

  Wakizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita baadhi ya wananchi walisema kumekuwa na mchanganyiko wa idadi ya abiria kila meli inapopata ajali, hali inayoonesha kwamba Sumatra hawana utaratibu mzuri wa kuelekeza wamiliki wa vyombo vya majini jinsi ya kutunza kumbukumbu za abiria wanaopanda melini.

  "Hakuna utaratibu mzuri wa kutunza kumbukumbu wanaoingia katika meli na hii inachangia watu wengi kuingia katika chombo bila shaka kupita uwezo wake." Alisema Saidi Kilopwa Saidi aliyekuwa akisafiri kwenda Zanzibar aliyekuwa bandarini Dar es Salaam.

  Link Ajali ya Meli Zanzibar; Sumatra yabebeshwa lawama - Global Publishers

  Kama tumejifunza kitu baada ya ajali hizo, basi ni mwanzo mzuri.
  Ikitokea ajali, itapatikana idadi ya wasafiri halisi waliokuwemo katika chombo cha usafiri na sio makisio. Hilo litawezekana kama hakutafanyika uchakachuaji.
   
 17. peri

  peri JF-Expert Member

  #17
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kama ni kwa sababu ya usalama itakuwa vzr.
  Na ni lini utaratibu huo utaanza kutumika?
   
 18. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #18
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Mkuu Nonda nimekuelewa, lakini ninayo maswali mawili madogo ya nyongeza

  1. Je utaratibu huu pia unawahusu Wasafiri/raia wanaosafiri kutoka Zanzibar kuja Tanganyika?

  2. Kwa kuwa hili Tangazo limetolewa na SUMATRA je sheria/utaratibu huu unahusu usafiri wote wa majini? eg Unguja na Pemba and vice versa, Mwanza na Bukoba and virse versa, DSM na Mafia and vice versa na kule Lake Tanganyika na Lake Nyasa?

  Nitashukuru kama nitapata ufafannuzi wako.
   
 19. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #19
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Ni mambo ya "nchi huru" ila wanajificha ktk mwavuli wa "kudhibiti taarifa za abiria"
   
 20. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #20
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Mimi naomba kuuliza tu hivi ukiwa Uingereza na ukitaka kwenda Ireland pale kwenye ferry yao kuna huu upuuzi wa vitambulisho? Na je hapa kwetu ukikata tiketi ya hivi vindege vya Coastal unaulizwa vitambulisho?

  Nawashauri Watanganyika wote ambao wanapenda kutembelea hiyo nchi ya kipuuzi Zanzibar ni bora wawe wanatumia usafiri wa ndege za chater maana inaonekana dhahiri sasa usafiri wa bahari ndio kaburi lenu hivyo wanataka wawatambuwe vizuri?
   
Loading...