Leo nilikuwa namuangalia Ngosha alipokuwa akiongea na wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi, Kweli mzee Kazeeka ghafla. Ile nuru aliyoipata baada ya miezi michache ya kuingia magogoni imepotea, Ngosha kawa mzee aisee!.
Nimeangalia kichwa chake kile, Japo kina Kauarazo ka asili kule juu, lakini leo nimeona hata zile nywele za pembeni japo kaziparuza, lakini Mvi zinaonekana waziwazi!. Kimoyomoyo nikasema yeees, sasa dozi inaingia kisawasawa!.Uraisi umemzeesha aisee. Kweli kazi ya Uraisi siyo mchezo!.
Lakini nikawa naangalia, nikastuka Ngosha anaposema kuwaonea huruma wafanyakazi kwa kuishangaa ile sheria ya kikokotowo!, Lakini nikajiuliza, SI NI YEYE NDIYE ALIYEITIA SAINI ILI IWE SHERIA AU AMESAHAU?, Wakati natafakari hilo nikagundua kuwa Wazee huwa wana kawaida ya kusahausahau!!
Anyway pamoja na hayo: Kusimamisha utekelezaji wa sheria iliyokwisha sainiwa kwa kauli ya raisi siyo kinga thabiti juu ya masilahi ya mfanyakazi, Wafanyakazi tunataka hiyo sheria irudishwe bungeni Itenguliwe kwanza halafu ndo tukae upya wadau tutengeneze sheria nyingine!. Sidhani kama Raisi ana mamlaka ya kusitisha utekelezwaji wa sheria fulani hadi tarehe fulani ya mwaka 2023, la sivyo huu huenda ni mtego wa kisiasa wa kusubiri uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka kesho na ule uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 upite halafu serikali iendelee kumkamua mfanyakazi kupitia sheria hiyohiyo Waliyoitunga, kuipitisha na kuisaini, Halafu leo wanajifanya KUIKANA LAKINI HAWATAKI KUIFUTA!
Wafanyakazi wameipokea gesture ya mheshimiwa raisi, lakini wanasema kuwa bado haitoshi, kusitishwa utekelezaji wa sheria haimaanishi kuwa sheria hiyo imeondoka. Maana yake ikitokea wakashindwa kuelewana na serikali katika mazungumzo basi hiyo sheria kandamizi bado iko palepale inasubiri kuwanyonga!,
Maana kama sheria imetungwa na serikali, Ikapitishwa kwa kura za wingi za ndiyo na wabunge wa chama kinachounda serikali, kama ilijadiriwa kwenye kikao cha baraza la mawaziri ambacho raisi ni mwenyekiti kisha Ikasainiwa na Raisi huyohuyo ambaye leo "anawaonea huruma wafanyakazi kuwa hiyo sheria ni mbaya" Je ni ipi guarantee kuwa Usitishwaji wa utekelezaji wa hiyo sheria una nia njema kutoka upande wa serikali?.
SERIKALI ITENGUE HIYO SHERIA KUPITIA BUNGENI KWANZA ILI MAZUNGUMZO YAANZE!