Kweli tawala zinatofautiana:JK-kikombe cha babu kinatibu;JPM-waganga tiba mbadala wamulikwe!

jzm-teak

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
1,770
321
Tukijaribu kuangalia enzi za JK na kwa sasa(JPM) utaona kuna tofauti kubwa sana hasa kwenye swala la afya za watu. kipindi cha utawala uliopita ilisikitisha sana kuona afya za watu hazikuweza kutiliwa maanani sana hasa kuhimiza watu kutumia tiba/dawa zisizodhibitishwa kisayansi.
Nilishangaa sana enzi za kikombe cha babu kikombe kimoja tu kilichoaminika kutibu magonjwa sugu ambayo hata sasa bado dawa haijagundulika, serikali ilisaidia kueneza propaganda kuwa dawa ile inaponya!. viongozi wakuu walikunywa, sijui kama walipona.
Kwa serikali ya JPM imekuja na style ya kuwamulika wanaojiita WAGANGA WA TIBA MBADALA , ili kubaini kama dawa zao zinatibu kweli ama ni njia ya kujitengenezea pesa. Kuna dawa asili zinaibu kweli na zinajulikana kwenye makabila yetu. Lakini ili la kuibuka waganga hawa, ambao wengine wanajiita maprofesa halikubaliki kabisa maana walio wengi wanatapeli watu kwa nia ya kutengeneza pesa.
Hapa inaonyesha kuwa utawala uliopita ni tofauti kabisa na utawala wa sasa.
 
Wanamsingizia tu Ndugu Magufuli!

dkmagupombe.jpg
 
Una ugomvi na waluther wewe sio bure, waluther na babu yao wa samunge walikuwa wanamtetea na kuwa anatibu uwezo wa yesu, hata pale waziri wa afya muislamu dr haji mponda alipopeleka taarifa bungeni kuwa dawa hiyo ni uzushi, mlikuwa wa kwanza kimsakama, jk hakuwa na uwezo wa kuingilia mambo ya kiimani,wagala mnaamini sana katika miujiza ndo maana kila siku mnapotezwa na wachungaji feli
 
Muhanga wa kikombe JPM hakupata nafuu au kupona labda ndio maana kaamua kuwatokomeza, ila ni uamuzi usiofaa kabisa.
 
Kumulikwa kwa waganga wa tiba mbadala kunafaa sana lakini sio kwa kukomoa baadhi ya watu ambao tiba zao zimesaidia wengi.
 
Back
Top Bottom