Angalizo la serikali kuhusu tiba mbadala ni sahihi kabisa

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,692
Monday, December 28, 2015
Serikali Yasema Tamko Lake La Tiba Mbadala na Asilia Liko Palepale [/paste:font]

tmp_20457-unnamed%2B%252810%25291982859619.jpg


Serikali imesema kwamba tamko lake lilitolewa hivi karibuni kuhusu matangazo ya Tiba Asili na Tiba Mbadala liko palepale kwa kuwa lengo lake ni kuboresha huduma hiyo. Hivyo kama kuna mtoa huduma ambaye amekwazika na tangazo hilo Wizara ipo tayari kuzungumza naye.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamko hilo kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam.

Tamko hilo lilitolewa Desemba 24, mwaka huu,ambapo limepiga marufuku matangazo yote yanayohusu tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Kwa wale wenye vibali wanatakiwa kuviwasilisha vibali na matangazo yao kwenye Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ili vifanyiwe mapitio.

Tamko hilo liliendelea kufafanua kwamba utoaji wa elimu ya afya kwa umma unaofanywa na watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii umepigwa marufuku hadi hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa.

‘Watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini kote wanaagizwa wawasilishe kwenye Baraza nyaraka zote muhimu ndani ya wiki mbili kuanzia leo Desemba 2015. Baadhi ya nyaraka hizo ni zile zinazohusu kuuza dawa za asili na tiba mbadala, nyaraka za kumiliki mashine zinazotumika katika kufanya uchunguzi katika tiba asili na tiba mbadala,’ lilieleza tamko hilo.

Tamko hilo lilifafanua kwamba Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala linaagizwa katika kipindi cha siku 14 kuanzia 24 Desemba 2015, lipitie nyaraka zote zikapowasilishwa zinazohusu usajili wa watoa huduma, usajili wa vituo vyao, ikiwa ni pamoja na maduka ya dawa za asili na dawa za tiba mbadala, usajili wa dawa zote zinazotumika katika huduma hizo na usajili wa mashine zote zinazotumika katika huduma za tiba asili na tiba mbadala.

Aidha akizungumzia kuhusu tangazo hilo, Waziri Ummy alisema ‘Mimi niko tayari kuzungumza na mtoa huduma ambaye amekwazika na tangazo hili, ili aweze kueleza ni sababu zipi zinazomfanya asisajiliwe. Tunafanya hivi kwa mujibu wa sheria ,kanuni na taratibu,’ alisisitiza.

Aliongeza kwamba Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala Namba 23 ya Mwaka 2002 inaeleza wazi.

Kwa mujibu wa Waziri huyo alitaja idadi ya watoa huduma hiyo kuwa wako 75,000 kwa takwimu za nchi nzima.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dkt. Edmund Kayombo alisema hadi sasa hawajapokea mrejesho wa tamko hilo la Serikali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama Vya Tiba Asili Tanzania(SHIVYATIATA), Abdulrahaman Lutenga alisema hakuna mganga yoyote aliyepinga tamko hilo na Serikali, hivyo tamko lililotolewa hivi karibuni la kupinga agizo hilo si halali kwa kuwa halikupitia katika shirikisho hilo.

‘ Hatutambui kampuni hii iliyotoa tamko la kupinga tangazo la Serikali kwani ya mtu binafsi yenye wanahisa 11,’ alisema Lutenga.

Akizungumzia kuhusu hatima ya tamko hilo, Dkt. Kayombo alisema baada ya siku walizotoa kumalizika watatangaza hatua zipi zitachukuliwa kama vile kuwaondoa wasiofuata sheria.

====

Wadau je! hamjajifunza tu ya Mzee wa Loliondo?

Kabla ya kutoa maoni yangu I must declare interest I a am qualified Medical Doctor of more than 30 years in the profession.

Mgongano tuliokuwa nao kwa muda mrefu na wenzetu hawa ni mgawanyo wa kazi, kwanza hata utambilisho wao tuliwaboreshea katika vikao vyetu na wao hapo nyuma tukasema jamii isiwaite waganga wa kienyeji bali iwaite waganga wa jadi kwa nia nzuri kabisa ya kuubali mchango wao , sasa tuanzie hapo.

Waganga wa jadi wa mwanzo ambao waliwahi kukaa kikao na serikali walikuwa wanatibu kwa mizizi na ramri ndio ilikuwa ni diagnostic procedure yao, mpaka pale Mhimbili mimi niliacha kuna kitengo kabisa cha uchunguzi wa matibabu ya miti shamba na ilionekana dawa zao nyingi ambazo ilikuwa ni mizizi na magome ya miti ilikuwa na ACTIVE INGDRIDIENT, ila utunzaji wao ulikosolewa maana mizizi ilikuwa inakaa mda mrefu mpaka inakauka kwa lugha ya kiganga cha zaidi tunasema ilikuwa ime-xpire .

Mgawanyo wa kazi tuliokubaliana hapo nyuma ilikuwa kama ifuatavyo;-
Kama mgonjwa akienda kwenye clinic zao ana ugonjwa wenye dalili za Malaria,kipindupindu, uti wa mgongo au dalili za kifua kikuu (kukohoa makohazi yaliyochanganyika na damu) basi haraka warufae mgonjwa huyo kwenye hospital za serikali kwa maana zahati, vituo vya afya au hospital za wilaya kwa mantiki kwamba wakiendelea kukaa na mgonjwa huyo huko kwenye clinic zao na magonjwa hao wenye magonjwa ya kuambukiza wanaweza kuambikizwa wenyewe au kuambikiza jamii nzima.

Ila na sisi kwenye hospital za serikali tulikubaliana katika mgawanyo wa kazi huo tukipata wateja ambao wanataka Nkenkewa za biashara, mwanaume apendwe na mwanamke, zindiko la nyumba au dawa za kuvuta bahati basi haraka tuwalufae kwa waganga wa jadi maana ndiyo wenye uwezo huo
Sasa hivi karibuni makubaliano hayo yamevurugika kabisa badala ya kujiita waganga a jadi wanajiita ni Madaktari au Profesor au badala ya kujiita ni waganga wa jadi wamebadilisha na kuwa ni Tababu wa tiba mbadala na kuvaa makoti meupe na stetoscope shingoni.

Badala ya kupiga ramri wanatumia any electronic device kama ni diagnostic tools zao.

Madhara yake:
Ieleweke kwamba mpaka sasa haijagundulika computer yenye uwezo wa kufikiri ila Computer zinarahisisha kazi tu, kwa mfano unaituma Computer au any electronic divice kama CT- SCANNER, Utra sound iangalie kiasi cha sukari kwenye damu, vifaa hivyo vyote vitakutajia kiasi tu cha damu lakini kamwe haviwezi kukuambia kwamba mwenye sample hii ya damu ana KISUKARI. Kazi ya kutafisiri ni ya kwako wewe uliyetuma kipimo hicho au ni wajibu wako ukipata majibu uwapelekee wenye uwezo wa kutafisiri.

Sasa hawa wa Tiba mbadala wamenunua vipimo hivyo na wanavitumia lakini je! nani anawatafisilia ? Wakati waganga wa serikali wanajua wazi kabisa hawawezi kutafisiri? Serikali iache tu wananchi waendelee kutapeliwa na kujiweka katika umaskini wa kutupwa maana huwa wanawachargi bei za ajabu?

Muingiliano huo wa majukumu ya kazi kati ya waganga rasmi na waganga wa jadi unafanya kitu kingine kibaya sana, nacho ni kuna namna zinazoeleweka za kujikinga na magonjwa ndio maana kuna usemi unaosema kukinga ni bora kuliko tiba. Waganga wenzetu wa tiba mbadala hawazingatii hili suala la kinga ni wepesi sana wa kumwambia mtu ana TYPHOID kuwa ugonjwa huo dalili zake haziko wazi, ila hawawezi kumwambia mgonjwa ana kipindupindu kwa sababu mgonjwa atakataa maana atasema siharishi uhalo unaofanana na maji ya kuoshea mchele. Na hupenga kupachika wateja ugonjwa huo maana matibabu yake ni ghali. Madhara yake makubwa katika jamii kuhusu kupachika watu magonjwa ni KU-CREATE FORCE SENCE OF SECURITY,jamii haizingatii kujikinga tena bali inazingatia imani ya matibabu mbadala toka matangazo yanayotolewa kwenye TV.

Mfano matangazo hayo yamesababisha ugonjwa wa UTI ( Uambukizo kwenye mfumo wa mkojo-Urinary Tract Infection) eti unasababishwa na kuchangia vyoo, huu ni uwongo , uwongo ,uwongo wa hali ya juu kimsinngi any urinary tract infection kama gonorrhoa, Kaswende asilimia kubwa husababishwa na kujamiiana kusiko salama, sasa ona badala ya kuielekeza jamii iepukane na ngono nzembe ili isipata UTI wana matibabu mbadala wanaielekeza jamii isichangiane matundu ya vyoo. Hili hali Dr. Kigwang
ala hawezi kukubaliana nayo kabisa ni heri asiwepo.

Hii inafanana kabisa na Kinjekitile aliwadanganya watu kwamba wakinywa maji yake risasi za mjerumani zitageuka maji kwa hiyo askari wakawa wanasonga mbele tu kwa imani hiyo bila kuchukua tahadhari ya kujificha au kuka-maforage au ambush wakawa wanaenda kichwa kichwa tu , kilichotokea kula mtu anajua.

Sasa na wenzetu hawa wa tiba mbadala wanatengeneza kitu hicho kwa sababu matibabu yao ni business oriented na wala siyo ethical oriented kama ya hospitali, Sasa je! serikali iache tu hii hali iendelee , watu waendelee kujitajirisha tu kwa njia ambazo ni za uwongo kabisa kama za babu wa Loliondo?

Wanabodi karibuni tuchangie mjadala
 
Last edited:
Ni wajinga tu ndio wanaotetea ujinga unaofanywa na hao watu.
Alafu kuweka mambo sawa, ultrasound na CT scan ni imaging studies na haziwezi kupima kiwango cha sukari kama ulivyosema, kingine kuna tofauti Kati ya urinary tract infections na genitourinary infections, gonorrhea na syphilis ni genitourinary infections.
Japo kuwa ni kweli urinary tract infections is not transmitted by sharing toilets and is neither transmitted by unprotected sex as you have stated, husije hukaachanisha ndoa za dada zetu.
 
Ni wajinga tu ndio wanaotetea ujinga unaofanywa na hao watu.
Alafu kuweka mambo sawa, ultrasound na CT scan ni imaging studies na haziwezi kupima kiwango cha sukari kama ulivyosema, kingine kuna tofauti Kati ya urinary tract infections na genitourinary infections, gonorrhea na syphilis ni genitourinary infections.
Japo kuwa ni kweli urinary tract infections is not transmitted by sharing toilets and is neither transmitted by unprotected sex as you have stated, husije hukaachanisha ndoa za dada zetu.
Ni vizuri watu wote tuungane kupinga utapeli huu unaofanywa na watu wa tiba mbadala.Gazeti la jana tarehe 28-12-2015 la Mwananchi limeelezea vizuri kuhusu dhuluma, ulaghai,utapeli na maovu mengine yanayofanywa na jamaa hawa wa tiba mbadala. Tukitaka kuelewa juu ya hili fuatlia mfumo wa matangazo yao kwenye TV na pia google kwenye mtandao aina za diagnostic tools mfano, quatum magnetic analyser, wanazotumia na bei zake na hapo hapo linganisha na bei wanazowatoza wateja wao ambao hawajitambui.
 
Last edited:
Nakubaliana na hili asilimia zote kabisa...... huu ni utapeli na uongo mtupu na hakuna ubadala wowote hapa
 
Yeyote anayechangia kupinga huu utapeli wa hawa waganga wajadi mimi nitampenda kufa, hawa watu ni wezi, tena matapeli waliobobea......nina rafiki yangu yupo pale Malapa, huyu alikuwa anafanya biashara za DVD na CD miaka kadhaa nyuma, tulipoteana miaka kama mitatu hivi, siku tulipokuja kuonana akaniambia amekuwa Dr......ana clinic yake hapo Malapa lwenye ile Ghorofa ya njano, kweli kuna siku nilimtembelea nilipofika hata hatukuweza kuongea vya kutosha maana alikuwa busy na simu kila saa akipigiwa kupewa oda ya daea huko mikoani, kazi yake ilikuwa ni kutaja bei tu na kuwaambia watume hela kwa njia ya simu........kwa hakika muda niliokaa pale japo sikuwa makini sana ila nadhani jamaa alishasema atumiwe hela sio chini ya mil 2 na point kadhaa......sasa nikajiuliza mpk siku inaisha anatumiwa kiasi gani.....na kilichonishangaza ni kuwa hapo mtu hajapimwa anafanya kumuambia tu sijui mgongo unauma, jamaa utasikia anajifanya kuuliza maswali mawili matatu halafu anaibuka na jibu......hapo ni misuli, sijui imejifunga kutokana na hiki na hiki.....dawa ni 250,000/=
Pamoja na kuwa hawa mawaziri wa JPM wanataka na sifa ndani yake, ila kwa hili nawaunga mkono 100%.
 
Back
Top Bottom