Lushoto wapata dawa ya kinga ya Corona, mganga wa tiba mbadala ndugu Shaban ameseme wabunge wengi wameshakunywa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
42,017
2,000
Mganga wa tiba mbadala ndugu Shabani wa Lushoto mkoani Tanga amesema amegundua dawa ya kinga ya Corona ambayo imewasaidia watu wengi mkoani Tanga.

Shabani amesema dawa hiyo ni kinga kwa magonjwa yote ya mfumo wa kupumua na kwamba hadi sasa wabunge wengi wameshakwenda hapo Lushoto kunywa kikombe cha dawa hiyo.

========

Mamia ya wakazi wa Lushoto mkoani Tanga wamefurika kwa ajili ya kunywa kikombe cha dawa inayodaiwa kuwa ni kinga ya virusi vya Corona inayotolewa bure na Mbunge wa jimbo hilo, Mh. Shabani Shekilindi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo.

"Wabunge walitumia sana dawa hii, nadhani we mwenyewe ni shahidi, tangia mwaka jana mpaka leo hii ninavyoongea, kwa uwezo wa Mungu hakuna Mbunge aliyefariki kwa ugonjwa wa upumuaji, mfumo wa upumuaji -- kukosa hewa.", alisema Mbunge huyo.

"Wito wangu ni kwamba wanachi waje wapate dawa, na dawa hii ni nzuri. Dawa hii inatibu magonjwa ambayo ni nyemelezi katika mfumo wa hewa kama pnemonia na mengineyo. Kwahiyo tunawashauri wananchi waje wapate dawa hii kwakuwa ni faida ya wao na jamii. Wananchi wakiwa na afya njema, basi ni bora zaidi kwakuwa watajumika katika shughuli za maendeleo." alisema mwananchi mmoja

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama.
 

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
4,919
2,000
Wakati nchi za wenzetu wataalamu wanakesha maabara kutafuta suluhu ya changamoto za magonjwa ya Korona, Bongo tunategemea miujiza ya kuchemsha mizizi matokeo yake tunaishia kufa kama kuku wa kideri.
Kwa sababu virusi wametengeza wenyewe kwenye maabara zao, hizo wanazoita chanjo zilizozalishwa chini ya mwaka mmoja ni kwa ajili ya makampuni yao kupiga hela kupitia hizo chanjo, ngoja tuone hili litatufikisha wapi....
 

jonas amos

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
2,383
2,000
Wakati nchi za wenzetu wataalamu wanakesha maabara kutafuta suluhu ya changamoto za magonjwa ya Korona, Bongo tunategemea miujiza ya kuchemsha mizizi matokeo yake tunaishia kufa kama kuku wa kideri.
Kama hawafi poa wanafaida sana Ila kama wanadanja acha tutetee uhai wetu kwa namna ambayo tu naweza

Mungu aliweka siri nyingi katika mimea hasa mizizi na majani na baadhi magome yake
 

ayb

Member
Oct 17, 2012
22
45
Kwa sababu virusi wametengeza wenyewe kwenye maabara zao, hizo wanazoita chanjo zilizozalishwa chini ya mwaka mmoja ni kwa ajili ya makampuni yao kupiga hela kupitia hizo chanjo, ngoja tuone hili litatufikisha wapi....
Wakina nani hao?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom