Kweli serikali imejishindwa kabisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli serikali imejishindwa kabisa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Expedito Mduda, Jun 8, 2012.

 1. Expedito Mduda

  Expedito Mduda JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kuchukiwa kwa serikali hii kunatokana na kutowajibika hata katika masuala madogo sana. Hivi nyie watu mliopo serikalini hamjajua kwamba vitu vidogo mnavyoshindwa kusimamia kunawafanya mchukiwe na kila mtu?
  Kwa mfano, hii michango wanayochangishwa wanafunzi wa shule za msingi eti iliwafanye mitihani ni sahihi? Kama ni sahihi mbona watoto hawapewi risiti ya hiyo michango? Hebu angalieni mambo kama hayo. Hilo si swala la kusubiri mzungu aje asaidie. Hebu angalieni shule za manispaa za Iringa muone kama hii michango uko kwenye utaratibu wa kiserikali. La sivyo muamini hakuna mchawi anawaloga mchukiwe ila ni ninyi wenyewe. Eti mtoto aende na fedha shule halafu mwalimu anamwandika kwenye karatasi bila risiti. Mtoto anarudishwa nyumba mkachukue fedha ya mtihani. Hivi matumizi ya hizo fedha nani anaratibu. Mtoto wa darasa la tano mtihani Tsh. 2000. Imekaaje hapo?
   
Loading...