Kweli Pombe ni Mwanaharamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli Pombe ni Mwanaharamu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 9, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kweli pombe si maji na unapoiendekeza basi inaweza kukuaibisha kama sio kukutoa roho kabisa, mwanaume huyu wa nchini Uingereza alikuwa miongoni mwa waalikwa katika sherehe ya kugawa tuzo kwenye hoteli ya kifahari ya jijini London, lakini pombe alizok
  Akiwa ameulamba vizuri na tai yake, mwanaume huyu mwenye umri wa miaka 40, alikuwa miongoni mwa watu wachache waliopata nafasi ya kualikwa kwenye sherehe ya kugawa tuzo za sanaa kwenye hoteli ya kifahari ya watu matajiri ya Savoy Hotel jijini London.

  Kutokana na pombe alizokunywa, mwanaume huyo alitolewa nje ya ukumbi baada ya kudondoka chini kwasababu ya pombe mbele ya mgeni wa heshima.

  Safari ya kurudi nyumbani kwake iliyorekodiwa na kamera za ulinzi CCTV za jijini London, imemfanya mwanaume huyo ambaye jina lake bado halijapatikana awe maarufu kuliko walevi wote duniani.

  Mwanaume huyo alidondoka na kujipigiza kichwa chini miguu juu wakati akishuka chini kwenye ngazi. Aliendelea na safari yake huku akidondoka na kujipigiza kwenye vitu mbalimbali kuanzia mistimu ya simu mpaka kwenye viambaza vya barabara.

  Safari yake yote ilirekodiwa na kamera za ulinzi barabarani, video ikimuonyesha jinsi alivyokuwa akianguka chini na kujipigiza kwenye vitu mbalimbali.

  Kwa bahati nzuri, mwanaume huyo hakuvunjika kiuno, shingo wala mikono yake katika safari yake hiyo ya kuelekea kwake.

  Ilimchukua siku 10 mlevi huyo kuweza kukumbuka amepoteza wapi waleti yake na jaketi lake. Alirudi kwenye hoteli ya Savoy kuulizia kama wameiona waleti yake lakini kwa bahati mbaya haikupatikana.

  Shikilia mbavu zako vizuri kabla ya kuangalia video hii chini.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...